Shilingi Milioni 500 Kujenga Barabara za Lami Lupembe

Shilingi Milioni 500 Kujenga Barabara za Lami Lupembe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amesema Serikali imedhamiria kujenga Barabara kwa kiwango cha Lami katika Jimbo la Lupembe ambapo amesema jumla ya shilingi Million 500 zimetengwa.

Katimba amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali la Mheshimiwa Edwin Enosy Swalle, Mbunge wa Jimbo la Lupembe aliyeuliza Je, Serikali kupitia TARURA ina mpango gani wa kujenga Barabara za lami katika Jimbo la Lupembe.

“Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitia TARURA imepanga kuanza ujenzi wa barabara katika Jimbo la Lupembe ambapo katika bajeti ya mwaka 2024/25 imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami. Barabara itakayoanza kujengwa ni ya Lunguya - Soko la Mbao yenye urefu wa kilomita 1.0 ambayo pia inapita katika Kituo cha Afya cha Mtwango.”

Aidha mhe. Katimba amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kutengeneza mpango maalumu ambao utatuka katika kugawa fedha za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara kutokana na manzigira ya Halmashauri husika ambayo utazingatia umhimu wa Barabara katika kilimo na urefu wa Barabara husika

GFR7Lk3W4AArz2Efrtyuio.jpg
GPLD2u2WcAA4owG.jpg
GPLD2u_XgAAPyB2.jpg
GPLD2uuX0AALWda.jpg
GPLD2u6WwAAvTRx.jpg
 
Back
Top Bottom