ibrah0102
JF-Expert Member
- Jul 21, 2023
- 384
- 642
Acheni soko lenyewe liamue bei @ alisikika Waziri Mmoja akisema
Cement mwaka jana mwezi wa nne 15200 sasa 18500_200
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Cement mwaka jana mwezi wa nne 15200 sasa 18500_200
Mchawi wa uchumi wetu ni huyu.Sasa mchumi anayetegemewa ni Mwigulu we unategemea miujiza gani!.
Kazi kwao mimi na wewe ipo siku tutakufa, kama Ilivyo watu ambao leo ni mamlaka ya teuzi na wao ni wafu watarajiwa.Wew umeongea ukweli ..blaa blaa za export ni kwa watu waliokosa hoja ..huweiz kuwaambia watu wale kwa urefu wa kamba zao halafu utegemee moujiza ufisadi ni wa kiwango cha juu sana
Ufisadi, rushwa, ubinafsi, kutowajibika na kutowajibishwa, teuzi, tenguzi za hovyo,undugu, udini,ushikaji kwenye serikali unaliangamiza taifa. Sijawahi kumsikia SSH akikemea ufisadi, rushwa au kufukuza mawaziri kwa kutowajibika kubadili kauli yake wale kwa urefu wa kamba zao.Mpango alikuwa chini ya kiongozi imara ..sasa wa kwetu anarembu na kusema mkalitizama ..basi unategemea miujiza gani
Unaonaee !,Eti Lipumba hawezi kuwa Waziri wa mipango kisa yeye ni CUF,Kwa kweli shillingi ya Tanzania inaporomoka kwa kasi ya kutisha dhidi ya sarafu nyingine. Ukitaka kujua kuwa shillingi yetu inaporomoka kwa kasi linganisha bei ya bidhaa kwa leo na ulinganishe na miaka mitatu, miwili na hata mwaka mmoja.
Chukua mfano wa nishati ya mafuta. Miaka mitatu iliyopita bei ya dizeli kwa lita moja ilikuwa wastani wa Tshs.1,500 leo hii lita moja ya dizeli ni wastani wa Tshs.3,300. Mfano mwingine chukua sukari. Miaka mitatu iliyopita sukari kilo moja ilikuwa Tshs. 1,300 leo hii kilo moja ya sukari ni Tshs.3,500.
Sasa tuje kwenye kichekesho. Jana nilikuwa kwenye mwalo moja hapo Ziwa Victoria na sikuamini macho yangu nilipoambiwa kuwa samaki moja aina ya sato ni Tshs. 30,000 karibia bei ya mbuzi wakati miaka mitatu iliyopita samaki wa uzito huo alikuwa akiuzwa kwa Tshs.8,000.
Tuna wachumi, tunaelezwa uchumi kwa Mama umepaa na mbona sisi wananchi hatuoni badiliko lolote. Huku kijijini kuna umaskini wa kutisha. Mtu kujaliwa kula balanced diet labda kuwe na harusi au sherehe fulani.
Tuwaulize wachumi wetu, Je uchumi umepaa kwa vigezo gani?.
Mshahara wa laki nane unalipa kodi 98100Kuishi Tz ni Kama drama hivi yaani sisi wananchi ndio mtaji wa serikali kwa sehemu fulani hivi yaani pamoja na kuwa na
Mbuga
Migodi
Bahari/Bandari
Lakini bado wananchi ndio pato lenyewe. Wananchi wanahela.
Mtumishi wa umma Tz analipa kodi kubwa wakati mwingine Sawa na wafanyabiashara wakubwa wakubwa. Hii yote ni katika kuimarisha uchumi wa nchi
Jinga kabisa unakuta waziri ndie anae husika na wizara nyeti kama nishati namadini hajui kuwa kutoa ruzuku katika eneo lake linaweza changia kudhibiti mfumuko wa beiAcheni soko lenyewe liamue bei @ alisikika Waziri Mmoja akisema
Nakubaliana nawe mkuuHaa hiyo awamu ya 5 inaonyesha ulikuwa umeipania kweli ya 6..naona umeitetea kweli kwa external factor. Lakini amna awam ya hivyo kama hii 6
Watu wananunua sukari kutoka maeneo tofauti. Unadhani wewe uliyepo Dar unanunua sukari kwenye maduka ya Dar ni sawa na mtu wa Mbeya anayenunua kwa Vendors wanaopata sukari yao tunduma?Sukari gani ambayo kilo ilikua 1300? Hata wakati wa Kikwete ilikua 1800, tatizo lenu wengi humu hamna majukumu ngumu hata kujua bidhaa zilikuwa zinauzwaje miaka kadhaa iliopita.
Bajaji ya kununua milioni 10 kweli? Bajaji? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Juzi tu toyota ist iliuzwa 12m, leo nasikia wananunua 17m. Yaani 2020 hadi leo, hii ni hatari.
Comment ya maana kuliko zote so far. Umeongea vizuri nimependa.Sisi tuna export malighafi tena kidogo, wao wana export finished product kwa wingi. Import/Export ratio. Wao wanatechnologia wanazalisha ndani zaidi, na ziada wanagawa nje, sisis technologia hatuna, tunazalisha kidogo, ili kukidhi mahitaji yetu ya ndani tunaagiza kutoka nje. Tunaponunua kutoka nje tunatumia pesa za kigeni.
Kumbuka Dollar ni moja ya sarafu zinazutumika kama sarafu za biashara kimataifa, bila kusahau Swiss Franc, Japaneese YEN, British Pound, pesa ya kijerumani, kifaransa na Italiano.
Madafu yetu hayawezi kupanda thamani wakati hatuzalishi bidhaa zinazouzika kimataifa.
Factor ni nyingi wataalamu wasomi wa uchumi watasaidia mengine.
Hafamu msamehe.Mbeya ilikiwa 1200 mpaka mwaka juzi
Kwa kweli shillingi ya Tanzania inaporomoka kwa kasi ya kutisha dhidi ya sarafu nyingine. Ukitaka kujua kuwa shillingi yetu inaporomoka kwa kasi linganisha bei ya bidhaa kwa leo na ulinganishe na miaka mitatu, miwili na hata mwaka mmoja.