Shilole: 'V8 ndio gari ya Heshima sio Range Rover gari ya Kitoto hiyo'

Shilole: 'V8 ndio gari ya Heshima sio Range Rover gari ya Kitoto hiyo'

range ni yakifahari zaidi coz kuna moja niliona ya mheshimiwa ameinunua bilioni moja

lc V8 inapendwa na kuonekana ya heshoma coz ya uwezo wake wa kupita popote bila kukuletea shida
range inapenda ustaarabu haitaki fujo ukiipitisha kwenye madimbwi baada yasiku kazaa lazima ikuwashie taa kukujulisha kua kumetokea hitilafu.v8Lc haina ujinga huo

kwahio Lc V8 nibora kuliko range
 
Watu wanatakiwa kwanza wajue maana ya V8 ,

Kwani si Kuna RR v8,?

Pia Kuna Scania v8?

Mafundi magari njooni mtoe Elimu kuhusu four cylinders inavyofanya kazi pamoja na maana ya v8 , yaani eight cylinders.
hio v8 nishepu ya injini tuu ipo kwenye magari mengi ikiwemo lc na hio range.

pia zipo shepu mbalimbali Kama v6 na v4
halafu kuna hizi za kawaida kama 4 na 6 silinda
 
Ila ajue kuwa V8 ni engine na sio aina ya gari. Kwenye Range Rover pia kuna hiyo V8 engine.
Kibongo bongo V8 ni aina ya gari na inajulikana ni Toyota sasa wewe endelea kukariri kwamba V8 ni engine. Toyota inapendwa kwa sababu ya uimara wake kudumu / reliability kwa kiingereza hiyo Range huwezi kwenda nayo milimani namtumbo huko labda uishie humu humu Dsm.
 
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva na Mjasiriamali Shilole ameiweka wazi Gari ya ndoto yake anayotamani kumiliki.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari @officialshilole ameitaja “v8 new model” ndio gari ya heshima kwake na akiongeza kwa sema Gari aina ya Range Rover ni za kitoto.

View attachment 2591320
DOZEN SELECTION
Naunga mkono hoja
 
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva na Mjasiriamali Shilole ameiweka wazi Gari ya ndoto yake anayotamani kumiliki.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari @officialshilole ameitaja “v8 new model” ndio gari ya heshima kwake na akiongeza kwa sema Gari aina ya Range Rover ni za kitoto.

View attachment 2591320
DOZEN SELECTION


Vijana acheni kujikita kwenye vitu visivyo vya msingi. Tafuteni biashara Magari ya kutembelea ya wasanii yatakusaidia nini iga biashara sio matumizi!
 
V8 ni type ya engine ambayo LC wanayo kwa series zao kama 200, 300 lakini pia Nissan wana V8 , RR wana V8 shilole kutoka igunga anajua alphard tu ndio gari maana anabebea masufuria na hotpot zake labda na ubwabwa ukibaki,
 
Dawa ni kutafuta PESA unayanunua yote maana Gari zote hizo mbili ni za wenye Pesa

Land Cruiser ni ya moto,Range pia ni inatokota gari zote hizo haziitaji maneno zinahitaji

account iwe imenona kuanzia kuyamiliki mpaka kuyatunza,ila kibongo bongo Cruiser

ina HESHIMA yake,hatukatai Range ni kali ila Cruiser Muonekano wake unatisha umekaa

kishua mno mno,yani ukiliona unaweza OGOPA hata lisogelea,ila kuna huyu Mjomba RANGE

Yeye hana makuu,simple but SURE gusa unase,BINAFSI yangu nitayaendesha yote mawili

lakini nitaanza na LAND CRUISER ndugu zangu,hiyo Range ni baada ya kuizoea LC shilole

yupo sahihi ki heshima,LC ina adabu zote...RANGE unaweza hata itemea mate,Mpaka uambiwe

hayo mate yako kuyafuta yanahtaji dollar kadhaa ndio unashtuka kumbe umeyakanyaga.

Kimuonekano (nnje)Naipa LC 100% na RR (nnje) naipa 91% Huko ndani staki paongelea maana

nimepanda 1 tu LATEST hapo sijapanda la pili nikaweza linganisha,ila LC hawakukosea kuliita SHANGINGI.
 
“Unaijua v8 wewe” in pole pole voice [emoji1]

Hizi Gari bwana wengine washamba na hatuna tu uwezo. But ningekuwa na pesa ningechukua RR. Hiyo Land Cruiser nimeipanda Mara moja GXR Kwa kifupi niliapriciate. Range sikumbuki ya mwaka gani ya kiazmani but nilivulia kofia.
Wengine tumezoea IST, crown, alphard, harrier na prado.
Anyway inategemea perception ya mtu na hakatazwi kuona ujinga wake umeishia wapi.
 
Back
Top Bottom