Shindano la big brother lina maudhui gani?

Onhoo thank you hii nitaifatilia
 
Kama wale ni role models wa watoto wetu basi tumeishaaa
 
Hii imekaa kingono zaidi....na freemason
 
Wanasema ukiona Kipindi hukielewi, huenda haukuwa Mlengwa.

Kutokana na Umri, kwasasa nimekuwa sifatilii Big Brother tena, ingawa wakati nilipokuwa kwenye lika la adolescent nilikuwa muhanga wa kukitazama miaka ile ya Akina Mwisho Mwampamba, baadaye akina Richard n.k

==============
Kuna baadhi ya Filamu/Vipindi vya TV kutokana na maadili yetu havistahili kutazamwa.

Hiyo Program ya Big Brother na nyingine zenye mlengo huo, zimeanzishwa kwaajili ya ku-brainwash Vijana wetu ili waone mambo ya ngono na kukaa na vichupi chupi mbele ya Wazee wao ni jambo la kawaida.

Kama una vijana wako nyumbani, ni heri Remote ikafichwa chumbani kwa Baba.

Ni heri kuitwa Mzee Mnoko kuliko kuharibu kizazi chako kwa mikono yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…