Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png


Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Hapana mkuu siwezi kufanya hivyo hata siku moja. Mimi nikisema jambo huwa ninamaanisha. I am a man of my words. Ninahamishia uzalendo wangu katika kutafuta pesa sasa mkuu.

Uwepo wangu humu JF kwa sasa inatosha.
Mkuu Shiriki Shindano Lao Then Upumzike.
 
Hapana mkuu siwezi kufanya hivyo hata siku moja. Mimi nikisema jambo huwa ninamaanisha. I am a man of my words. Ninahamishia uzalendo wangu katika kutafuta pesa sasa mkuu.

Uwepo wangu humu JF kwa sasa inatosha.
Andika makala hapa my utashinda mchana kweupe na kura tutakupigia
 
Kwenye kutangaza mshindi, tumekuwa wazi: Kama hutaki ku-disclose your identity usishiriki shindano kwa jina la kificho.

Hatuwezi kutoa zawadi kimyakimya, washindi wataonekana na watapewa zawadi zao wazi na kutakuwa na sherehe kwa ajili ya tuzo hizi.

Asante
Aise hapa nilikuwa nimejipanga kuchukua huu ubingwa. Nilimuwa nimeandaa honge la makala. Lakini swala la kublow out my identity nikishinda limekuwa swala gumu kwangu.
Nimeahirisha.
 
Imeelezwa kwa uwazi kabisa (soma palipoandikwa ZINGATIA). Wewe andika kadiri uwezavyo, huenda ni miongoni mwa maandiko yako mojawapo likashinda.

Hata mtu angekuwa na ID 20, haziwezi kushinda zote. Wakati wa kufanya uamuzi washindi watakuwa contacted.

Asante
Ok sawa. Nataka kuanza sasa?
 
Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua
ANGALIZO:
Vigezo vya kumpata mshindi na ubora wa andiko vingefafanuliwa vizuri zaidi ya ilivyo sasa.
Je kutakuwepo na 'rubric' itakayofuatwa na majaji katika kutafuta andiko bora?

Maana yake hapa ni kwamba, endapo maandiko yatakayowasilishwa, kuwe na vigezo vya kutambua andiko linalokidhi kipimo cha kuwa na sifa za kuwa "Kichocheo...".

Inawezekana kabisa, katika maandiko yote yatakayowasilishwa yakawa hayafikii lengo la kuwa "Kichocheo..."; na JF ikalazimika kulipa zawadi zilizoainishwa..

Mfano wa 'Tuzo ya Mo Ibrahim' ni mzuri kuwa mfano. Kuna miaka hakuna viongozi wastaafu wanaostahili kupewa tuzo hiyo. Hapa pia inawezekana, kama maandiko yaliyowasilishwa hayafikii kiwango fulani, basi, zawaidi isitolewe.

Hili ni wazo tu katika kuboresha ushindani na kupata maandishi mazuri zaidi.
 
Hakuna kitu kizuri Katika jamii Kama kuwa muwazi hiyoo itakuondelea Changamoto utakazokumbana nazo Katika Jamii. Kwa Mfano Kama ukiwa kiongozi wa Jamii flani au hata serikalini kunachangamoto nyingi Sana ambazo Kama utazindekeza zitakugalimu kutoka na Jamii uliyonayo kutokuipa ushirikiano Wako Basi utaonekana adui wa hiyoo Jamii au kiongozi mbaya mbele ya Jamii.

Mimi naamini Katika Uhulu umuweka mtu salama kwa sababu like unachokifanya kinaonekana na Jamii uliyonayo Hata kama kunawatu wanapinga vile wewe unafanya jua hao madaui zako haikupaswi uwachukie Bali iwe Kama njia ya mafanikio yako pale wanapokukosoa. Jamii Forums niseme asanteni sna kwa kutupa habari zilizo Bora Japo mnapitia wakati Mgumu ktk kazi zenu tambue Mafanikio yenu ndio Mafanikio ya wa Tanzania wote
 
Back
Top Bottom