Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png


Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Hilo jukwaa la ‘stories of change’ mbona atulioni au mpaka tufuate link humu.
 
Naomba niweke wazi je kuhusu mada ya mahusiano ya mapenzi hasa kwa jinsia 1? Japo bandiko litahusu pia uchochezi wa mabadiliko ya fikra kwa upana wake kuhusu jambo hilo, vipi inakubalika au?
Pacha hivi wewe ni mgumu kuelewa au kimuhemuhe cha milion 5...Umeshajibiwa kuwa ni RUKSA as long as linachochea mabadiriko....Pacha punguza mtero.
 
Carleen ulinambia ulivyokuwa chekechea ulikuwa fundi sana wa kuandika insha na risala...sasa uwanja wako huu
 
Tanzania ili kupaisha uchumi wa inchi tunapaswa kuboresha nyanja zifuatazo .Utawala Bora ,Afya,Kilimo,ukusanyaji wa kondi,Uhuru wa vyombo vya habari,bunge nk,Siasa safi,Amani. nk,
1.UTAWALA BORA;kuwa na uongozi unaozingatia sheria na misingi ya maadili,kukemea ubadhirifu,rushwa,unyanyasaji na kushirikisha wananchi katika maamuzi
2.AFYA; Kila mtanzania anahaki yakupata huduma bora za afya bila kubagu jinsia kabila,umri,rangi,itikadi ya kisiasa au dini,uremavu hivyo serekali iweke jitihada za maksudi kuimalisha upatikanaji wa dawa,vifaa tiba,miundombinu kwenye zahanati,vituo vya afya hospitali,kuongeza wafanyakazi pamoja na motisha,mishahara kwa wafanyakazi Ili kusaidia kutoa huduma nzuri na bora pamoja na kusimamia na kushawishi kila mtanzania apate bima ya afya Ili kuweza kupata matibabu kwa urahisi na kwa haraka bila upendeleo
3.KILIMO; kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa hivyo serikali haina budi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kilimo bora chenye tija,kama vile kilimo cha umwagiliaji ambacho hakitegemei msimu wa mvua,zana bora za kilimo,mbegu bora na mazao yenye kuinua uchumi wa mwananchi,kuweka usawa kwenye bei ya mazao ili kumpa mkulima hali na nguvu ya kuendelea kuzalisha mazao bora yenye ushindani kwenye soko la dunia.
4.TECNOLOJIA; watanzania wote kuishi kwa kutumia techologia ikiwa ni pamoja na kutumia vyuo kutoa wataalamu wa kila nyanja ya technology na kuwaajiri kwenye viwanda vyetu Ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa bora zenye ushindani kimataifa
5.ELIMU;swala la elimu ni mtambuka,mitaala ya elimu iboreshwe ili iweze kuzalisha wanafunzi na wataalamu watakao weza kujiajiri na hivyo kupunguza changamoto ya ajira nchini, hivyo nchi itasonga mbele kiuchumi.
6.UHURU WA HABARI;kimsingi kila mwananchi anayo haki ya kupata habari sahihi na kwa wakati,wandishi wa habari wawe na Uhuru wa kukusanya habari kwa kuzingatia taaluma,weredi na ufanisi,asanifu wa habari kabla haijamfikia mwananchi,kuwepo na Uhuru wa kupata habari bungeni mubashara
7.UKUSANYAJI KODI; ukusanyaji kodi ni nguzo muhimu katika kujenga uchumi imara wa taifa letu,hivyo elimu itolewe kwa mwananchi mlipa kodi,mfanyabiashara na watumishi wa umma,kuwepo kwa usawa katika ulipaji kodi, kuepuka matumizi ya mabavu na vitisho kwenye ukusanyaji wa kodi.
8.SIASA SAFI;taifa linapaswa kuwa na siasa safi inayohudumia haki,msingi,amani usawa kuheshimiana,ukweli na uwazi hizi ni tunu za siasa safi,hivyo mwanasiasa safi ni yule anaetambua dhamana na wajibu wake kwa jamii,kujenga na kudumisha umoja na mshikamano kwa jamii.
9.AMANI;amani ni tunu kubwa ni wajibu wa kila mwananchi kuilinda kwa nguvu zote amani tuliyonayo kwa kuepuka kuchochea vurugu,kutii sheria bila shuruti,dini na majukwaa yote ya kisiasa zi/ya hamasishe amani na upendo.
 
Imeelezwa kwa uwazi kabisa (soma palipoandikwa ZINGATIA). Wewe andika kadiri uwezavyo, huenda ni miongoni mwa maandiko yako mojawapo likashinda.

Hata mtu angekuwa na ID 20, haziwezi kushinda zote. Wakati wa kufanya uamuzi washindi watakuwa contacted.

Asante
popoma GENTAMYCINE umesikia hiyo?...maana tunakujua una ID kama 500 hivi hapa jf.

zingatia : washindi watakuwa contacted.
 
Buku tu!? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣

LOOoo, mkuu, 'Sky' hapo umeua kabisa!

Mtu anaweza akaandika maneno 750, na kuweka picha mbili tatu zinazobeba uzito wa maneno yote 1500!

Sijui hali hiyo wataichukuliaje?
 
Mashindano haya yatasaidia sana kupata elimu ya mambo mengi. Aidha wanaJF watakuwa makini sana katika uandishi, tutasoma hoja mzuri na kutakuwa na umakini sana katika uandishi. Hawapongeza sana Watendaji wa JF kwa UBUNIFU HUU
 
Mashindano haya yatasaidia sana kupata elimu ya mambo mengi. Aidha wanaJF watakuwa makini sana katika uandishi, tutasoma hoja mzuri na kutakuwa na umakini sana katika uandishi. Hawapongeza sana Watendaji wa JF kwa UBUNIFU HUU
 
[emoji16][emoji16][emoji16]hii sio ya kukosa hata kidogo .
 
NGOJA NIANDAE DAFTARI NA KALAMU. NAANDIKA STORI ZANGU NA KUZIHARIRI KABLA SIJAZITUPIA JF.
 
hii nafasi yangu sasa kuibuka mshindi, japo ndio nimepata taarifa muda huu
 
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).
Kura zinapigwaje?? Kwenye zile nyuzi kule sijaona option ya kupiga kura au ni likes, dislikes na replies anazopata mhusika.
Naomba ufafanuzi kweny hili , na kama ni hivo je shindano ndo litakua la wazi na watu wataona kura zao kutoka kwa sisi members waziwazi. (Kama ni hivi watu watasagiana sana kunguni 😂😂😂 wataulizana maswali konki kukuleti dauni 😂😂)
 
Back
Top Bottom