Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png


Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Idea n nzuri sema Jambo baya jf stori za kuhamasisha uchumi, afya njema au maadili huwa hazina viewrs Ila mada za connection mwenye picha uchi au flani katumbuliwa huwa ndo zao.

Jamii yetu ibadilike mie Nina andiko langu la pesa sema ndo hvyo tuu pesa yenyewe ya mshindi n kidogo uzuri Kama watu watalifanyia kazi Basi jamii inaenda kubadilika na kutengeneza malakinea wengi Kama sio milionea.

Moderator heading zinakuwaje iliniwe rahisi kuzipitia na kuzitambua kwa urahisi
 
Nasemaje
Natangaza kiama.
Yeyote ambaye hatanipigia kura

Mzee mpili babu yangu fanya mambo kuna pesa inanukia huku
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Watu wengi wamekuwa wakitamani kuanza biashara lakini wanafikiri namna ya kuanza kwani mtaji wao ni mdogo sana.
Usiogope; kuwa na mtaji mdogo au kutokuwa nao kabisa sio mwisho wako wa kutimiza malengo yako.

“Usilie juu ya kile ambacho huna; tumia vizuri kile ulichonacho.”

Reginald Mengi.

Zipo mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kukuwezesha kufanya biashara hata kama utakuwa na mtaji mdogo. Tafadhali fuatilia hoja jadiliwa hapo chini kwa ufafanuzi zaidi.

1. Kuwa mbunifu
Moja kati ya mambo ambayo yatakusaidia sana kwenye kuanza biashara kwa mtaji mdogo ni ubunifu. Kwa njia ya ubunifu utaweza kushinda biashara na bidhaa zilizoko sokoni kwa urahisi zaidi. Unaweza kufanya haya yafuatayo:
Chagua wazo la biashara unalolipenda na kuliweza vyema. Hili litakusaidia kukabili changamoto vyema.
Angalia tatizo au uhitaji uliopo sasa na uutatue kwa bidhaa au huduma yako.
Panga bei vizuri; unaweza kuweka bei ambayo ni tofauti kidogo na bidhaa au huduma ambazo tayari ziko sokoni ili uwavutie wateja.
Kwa kufanya mambo yaliyoelezwa hapa juu utaweza kukuza biashara na mtaji wako kwa muda mfupi zaidi.

2. Anza na unachokijua

Unapokuwa na mtaji mdogo huhitaji kuhusisha mambo mengi mageni au yanayotegemea sana watu wengine kwa kuwa huna pesa za kuyagaramia.

Kwa mfano kama unaanzisha biashara ya ushonaji basi anza kutengeneza mavazi yale unayoyaweza kwa kutumia vifaa ulivyonavyo; kwa njia hii utajenga mtaji wako kisha baadaye utaweza kuajiri wengine watakao kuwezesha kutengeneza aina nyingine zaidi.
Unapofanya kile unachokijua gharama huwa haziwi kubwa sana kwani ni kitu unachokimudu mwenyewe.

Soma pia: Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara.

3. Waambie watu unachokifanya
Waambie watu unachokifanya kwani hili litakuwezesha kupata wateja na kufahamika. Watu wakijua unachokifanya watatamani kukifahamu zaidi; hili litakuwezesha kupata wateja na kuongeza mtaji wako.

Usiogope kueleza kuwa unafanya biashara ya mboga, chakula, duka dogo la bidhaa n.k. Kwani hujui unaemweleza atakuwa nani kwenye biashara yako.

Ukiwa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii waeleze pia juu ya kile unachokifanya.

4. Epuka gharama zisizokuwa za lazima
Kwakuwa bado una mtaji mdogo jitahidi kuepuka garama zisizo za lazima kama vile ofisi ya kifahari, matangazo ya gharama kubwa n.k.

Kuwa na matumizi mazuri ya fedha hasa kwa mambo ya msingi tu. Watu wengi wameshindwa kwenye biashara kwa sababu wameanza biashara kwa mbwembwe za matumizi badala ya huduma bora zenye ubunifu.

5. Fanya kazi kwa bidii

Kamwe huwezi kuona mafanikio kama hutofanya bidii. Kumbuka wewe ni mjasiriamali anayeanza hivyo ni lazima ufanye bidii ili soko litambue kuwa upo pia unaweza.

Tumia muda vizuri, pia hakikisha unatoa huduma yenye ubora wa hali ya juu kwa bei ambayo wateja wataweza kuimudu. Jitese kwa muda mfupi kwa kipindi cha kuweka msingi wa biashara yako kwani hata kipindi cha kupanda katika kilimo huwa ni cha taabu.
Soma pia: Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa.

6. Tumia rasilimali na fursa zilizopo
Njia nyingine itakayokuwezesha kuanza biashara ukiwa na mtaji mdogo ni kutumia fursa zilizopo. Kumbuka kuwa huwezi kutengeneza fursa kama huwezi kutumia fursa zilizopo.

Tumia fursa kama vile mitandao ya kijamii ili kujitangaza. Pia unaweza kutumia udhaifu uliopo katika biashara nyingine za watangulizi wako kama fursa kwani unaweza ukarekebisha udhaifu huo kupitia biashara yako.

Zipo pia fursa za mikopo yenye masharti nafuu ambayo itakuwezesha kuongeza mtaji wako. Kumbuka unahitaji kutumia mkopo kwa makini kwani utahitajika kuurudisha pamoja na riba tena kwa wakati.

7. Jali wateja

Kujali wateja katika biashara ni jambo muhimu sana kama unataka kuona matokeo chanya. Siku zote ninapenda kusema “wateja hufugwa”. Wateja hufugwaje? Hufugwa kwa huduma nzuri.

Waheshimu wateja wako pia hakikisha unatimiza na kumaliza haja zao katika ubora wa hali ya juu. Kumbuka siku zote mteja huja kwanza kabla ya pesa; hivyo usitangulize pesa kabla ya huduma nzuri kwa mteja.

Ukilifanyia kazi hili utaweza kukuza biashara na mtaji wako kwa muda mfupi.

Hitimisho

Zilizojadiliwa hapa ni mbinu saba zitakazokuwezesha kuanza biashara na mtaji mdogo. Usiogope unaweza hata kama una kiasi kidogo sana cha fedha.

Thubutu, nza, fanya bidii, weka nidhamu, mtangulize Mungu na hakika utaona mafanikio chanya katika biashara yako.
“Anzia ulipo.Tumia ulicho nacho. Fanya unachoweza.”

Audax Jovinary +255767559477
 
HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA!
��Mama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.

��Lakini kwa bahati mbaya akiwa amefika katikati ya mlima alizidiwa kiafya na hatimaye akashushwa mlimani akiwa amezirai hadi hospitalini.

��Siku ya tatu alipozinduka hospitalini huku marafiki zake wakimpa pole, aliwajibu kuwa “Mlima Kilimanjaro hauwezi kuongezeka urefu, lakini mimi mwanadamu nina uwezo wa kuongeza maarifa, nguvu na mbinu za kupanda milima wowote duniani. Kwa hiyo nitarudi tena wakati mwingine mpaka nipande mlima Kilimanjaro hadi kileleni, ingawa nimepata changamoto wakati huu.”.

��Alivyorudi kwao Marekani, alianza kufanya mazoezi tena ya kukimbia na kupanda vichuguu na vilima kwa muda wa mwaka mzima, na kisha mwaka uliofuata alirudi tena Tanzania, akapanda mlima Kilimanjaro mpaka kilele cha Kibo na mawenzi, na hatimaye akapewa cheti cha kupanda mlima Kilimanjaro!.

��Je huyo mzungu angeamua kusubiri mlima Kilimanjaro upungue urefu ndipo aje Tanzania kuupanda, jambo hilo lingewezekana?
��Je unataka maisha yawe rahisi ndipo uyamudu? Je unataka viwanja vishuke bei ndiyo ujenge nyumba yako? Je unataka ada za shule ziwe chini ndipo usome? Je unataka gharama za hospitali ziwe chini ndipo utibiwe? Je unataka mahari iwe chini ndipo uoe? Je unataka vitabu vya mafunzo ya biashara viwe bei chee ndiyo ununue? Unataka mshahara wako uwe mkubwa ndipo ufanikiwe? Je unataka shetani auwawe ndiyo umche Mungu? Je unataka dunia irudi nyuma, ndipo uweze kuyamudu maisha? Je, unataka urudi tumboni mwa mama yako ili uwe unakula na kulala bure? Ebo!��

��Kama nia yako ni kufanikiwa hutakiwi kujionea huruma, nenda kwa wakati na ujitoe hadi kieleweke. Kila la kheri na pia nakutakia MAFANIKIO makubwa sana wewe na kizazi chako! Siri ya utajiri ni ubahil asikudang'anye mtu tumia hela ikuzoee hakuna aliyezaliw kuwa maskin!

Mapambano yaendelee ndugu zangu by Audax Jovinary +255767559477.
 
MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI
✍��Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.
����Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.

������ Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi �� na �� ��magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!).

����Wapo ������wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.

����Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.

Hii inachangiwa na mambo mawili:-
����
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli.

����Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio.

����Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

������Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.

���� II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

����Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

✋��Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

��Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani.

��Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.

��Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze
������ Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze
By Audax +255767559477.
 
Pacha hivi wewe ni mgumu kuelewa au kimuhemuhe cha milion 5...Umeshajibiwa kuwa ni RUKSA as long as linachochea mabadiriko....Pacha punguza mtero.
Pacha Mil 5 nyingi, ni maisha ya mtu milele ujue? Lazima nipagawe [emoji23][emoji23][emoji23]

Nimekumiss mno, iv umepotelea wapi wee?
 
Nasikitika uzi wangu nimeuweka sasa zaidi ya saa mpaka sasa siuoni

uzi ule ni jiwe la ushindi kabisa nahisi nahujumiwa
 
Bado ni siku ya kwanza aisee.. subiria subiria watu wanaushawishi humu hasa members wa zamani. Ndumba lazima zihusike kama kawaida yetu waswahili...
Tupigiene tu kumpeni wote tu wadau. Ila Mimi sijajua jukwaa lenyewe naandikia wapi?
 
Back
Top Bottom