Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png


Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Kwenye kutangaza mshindi, tumekuwa wazi: Kama hutaki ku-disclose your identity usishiriki shindano kwa jina la kificho.

Hatuwezi kutoa zawadi kimyakimya, washindi wataonekana na watapewa zawadi zao wazi na kutakuwa na sherehe kwa ajili ya tuzo hizi.

Asante

Sijaelewa Maxence,kwa mfano mimi Becky siwezi kutumia ID kwa mfano Teresia 😉 😉 😉 kuandika makala humu,lazima iwe ID iliyozoeleka?
 
Hapa akiibuka mtu na andiko la kutuma pesa kwa App ya JF yenye makato nafuu anaondoka na zawadi ya washindi wote watatu hadi na ya mwakani kama shindano litakuwepo.
 
Hapa ndio utajua vyuoni kuna kazi kweli kweli watu wanaandika proposal badala la ku motivate watu wengine wafanye waliyoweza wao.

Ama kweli kila mtu ana tafsiri yake ya swali.
 
Sijasema hivyo. Just try your luck

Haya mkuu, ungepunguza maneno lakini,kwa anayetaka hata aende beyond 3,000 words ni sawa,ila kwa wengi waandike maneno yasiyozidi 300, itasaidia kubaki kwenye objectivity, lengo la shindano ni kuisaidia jamii yetu,itakuwa vibaya kama jamii haitaona huo msaada,namaanisha long essays/topics siku zote humu huwa zina muitikio hafifu/ignored.

Na hivyo kwenye hili shindano watu hawavote kabisaa sababu kusoma topic yote hawajasoma kwa sababu ni ndefu. mtu akishaona ndefu anaenda next one and next one without voting. Shindano ili kuifikia jamii yetu ni lazima tuwe short and precise, sio inasaidia voting peke yake but sending key message kwa jamii kwa ujumla
 
Kama leo sio mama yetu president Samia mambo ya kutuletea chanjo na nchi za uwarabuni kwani watanzania tupewe nini kiukweli watanzania hulalamika kila mda sijui wafanyeje serikali kila njia wanafanya ila watanzania wanaona nisiasa nashukuru Dorothy Gwajima kwakuwa mkali kwa madactari wazembe wasiojua kuhusu afya wananchi wao.

Kwa takwimu wanaosema kwasasa Tanzania Corona imepungua na hatawatu hawajali kitu chochote kuhusu Corona nisawa namwanajeshi kujitoa mwanga pale wakiona hali ijawa sawa inamaanisha wananchi wakikaa ndani bila kutafuta watakufa kwanjaa inabini watoke nje watafute huku wakipokea ushauri kwa madactari wao
 
haya mkuu, ungepunguza maneno lakini,kwa anayetaka hata aende beyond 3,000 words ni sawa,ila kwa wengi waandike maneno yasiyozidi 300, itasaidia kubaki kwenye objectivity...
Ukiandika something interesting people will read it all.
 
Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
Kama hutojali mkuu naomba nifafanuliwe hili sharti.

Mtajuaje kwwmba andiko hili limechochea mabadiliiko katika nyanja husika.

Je mtajua limechochea mabadiliko kwa andiko hilo kuwa na likes nyingi ?

Mtajua limechochea mabadiliko kwa andiko hilo kuwa na comments nyingi ?

Au mtajua limechochea mabadiliko kwa andiko hilo kuwa na viewers wengi ?

Au mtajua limechochea mabadiliko kwa andiko hilo kuwa na votes nyingi ?

Ni sifa zipi hizo ambazo zitakuwa zimetafsiri kwamba andiko hili sasa limechochea mabadiliko ?

Naomba ufafanuzi Maxence Melo
 
haya mkuu, ungepunguza maneno lakini,kwa anayetaka hata aende beyond 3,000 words ni sawa,ila kwa wengi waandike maneno yasiyozidi 300, itasaidia kubaki kwenye objectivity,lengo la shindano ni kuisaidia jamii yetu,itakuwa vibaya kama jamii haitaona huo msaada,namaanisha long essays/topics siku zote humu huwa zina muitikio hafifu/ignored, na hivyo kwenye hili shindano watu hawavote kabisaa sababu kusoma topic yote hawajasoma kwa sababu ni ndefu. mtu akishaona ndefu anaenda next one and next one without voting. Shindano ili kuifikia jamii yetu ni lazima tuwe short and precise, sio inasaidia voting peke yake but sending key message kwa jamii kwa ujuml

Kumbe thread ni ‘mnakasha’ na sio uzi, NYIEEE..!![emoji36]
Hili tamko walitakiwa walipitie vizuri. Sababu hili tamko humaanisha "Mjadala". Sasa kulipa maana ya "uzi" sijui wametumia vigezo gani au wamerejea wapi...?!
 
Imeelezwa kwa uwazi kabisa (soma palipoandikwa ZINGATIA). Wewe andika kadiri uwezavyo, huenda ni miongoni mwa maandiko yako mojawapo likashinda.

Hata mtu angekuwa na ID 20, haziwezi kushinda zote. Wakati wa kufanya uamuzi washindi watakuwa contacted.

Asante
Mimi nina swali la msingi kwenye vigezo na masharti hamkuandika. Swali lenyewe ni hili hapa.

Mmesema 'plagiarism' hairuhusiwi yaani kwa maneno mengi humu kwenye shindano huruhusiwi kuweka uzi ambao iliwahi kuchapishwa mahali kabla.

Je, kama aliyechapisha uzi wake akaamua kuleta uzi wake huo tena ki vingine ili kukidhi masharti ya shindano vipi ataruhusiwa?

Yaani, sawa na kusema mtu huyo kaaamua kushindanisha uzi wake mwenyewe aliowahi kuchapisha humu ama popote Je, ataruhusiwa??

NB: Kwa maoni yangu naomba jibu liwe ndio as long as yeye ndio mwenye uzi uliowahi kuchapishwa hapo awali. Nasema hivyo kwa sababu lengo kuu la shindano hili ni kupata 'solutions ya changamoto za jamii' na si vinginevyo. Hivyo msiweke restrictions kali kwenye kupatikana solutions za changamoto za kwenye Jamii.

Kwako, Mkurugenzi Maxence Melo JamiiForums na jopo zima la shindano hili.

Naomba jibu tafadhali.
 
Mtutangazie washindi sasa lakini huyo mtu aliyepigiwa kura nyingi sioni maajabu ya alichokiandika!

uzi wake wa kawaida sana, kuna mabandiko mengi sana mule yanakila kitu cha muhimu katika mabadiliko

Bandiko langu limeenda shule na lilihitaji ushindi moja kwa moja ila tatizo ni hawa member wa JF wanavyopenda nyuzi za wanawake..sijui huzitumia kinyapuka?
 
Mtutangazie washindi sasa lakini huyo mtu aliyepigiwa kura nyingi sioni maajabu ya alichokiandika!

uzi wake wa kawaida sana, kuna mabandiko mengi sana mule yanakila kitu cha muhimu katika mabadiliko

Bandiko langu limeenda shule na lilihitaji ushindi moja kwa moja ila tatizo ni hawa member wa JF wanavyopenda nyuzi za wanawake..sijui huzitumia kinyapuka?
Kwako,kunaweza lisilete tija ila ktk jamii likaleta tija,ukizingatia huu ndio wakati wa vijana kuomba kozi mbalimbali za chuo.

Muhusika kagonga kunakohusika..,na amejua kucheza na akili za watanzania wanataka nini sasa
 
Back
Top Bottom