Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png


Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Jaman mm nimeandika Ktk ukurasa wa facebook andiko langu sasa nimeshindwa kulicopy ili nilipaste lije huku, mwenye ujuzi anisaidie Tutagawana hiyo 5 milion
 
Wakuu
Tuliambiwa shindano hilo lilianza tarehe 14 na kufika kikomo 15

sasa tunaitafuta tarehe 17 bila majibu yoyoete na ukiangalia kura hazikufungwa jana kipindi nikiwa miongoni mwa wenye kura nyingi

Naandika hivi sasa bado kura zinaendelea kupigwa kinyume na masharti na sheria za shindano,, naona kuna dalili zisizonzuri

Kwanini mpaka sasa mshindi hatangazwi?
 
Kwa hyo mkuu ulikuwa na kura nyingi. Bila Shaka unadhan wewe n mshind

Shindano Bado Lina muda wa kutosha chief hukusoma vizuri

Kura pekee haziamui mshindi chief

MWISHO .; njoo na bahasha kubwa sababu nipo kwenye kamati yakumchagua mshindi uamuz n wako PM sijaifunga inakusubiri wewe tuongee kiutu uzima

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mpaka sasa mimi naongoza kwa kura nyiiiingi.
 
Inaruhusiwa kuhamasishana kupigiwa kura hasa kutumia mitandao mingine ya kijamii...make naona itapoteza kile ambacho team ya jf inalenga au walaji kupata kile kinachostahili
 
Dah! Sasa nilikuwa wapi sijaona huu uzi muda wote hadi milioni inaanguka njiani?
 
Jaman mm nimeandika Ktk ukurasa wa facebook andiko langu sasa nimeshindwa kulicopy ili nilipaste lije huku, mwenye ujuzi anisaidie Tutagawana hiyo 5 milion
Tumia browser ya uc browser uingie Facebook inakuwezesha kucopy au uende Facebook kawaida upige bandiko lako screenshot uscroll mpaka mwisho usevu kisha rudi kwenye Google translate uende kwenye camera afu uimport kisha ucopy maandishi yako uyalete hapa
 
Kama jamii forum wasipokuwa makini kwenye uchaguzi was story bora, nahisi watampa zawadi mtu asiyestahili.

Kuna mnyamwezi kaandika kitu cha hatari ila wanyabe wanapita kama hawaoni so far nyuzi nyepesi ndo zinapigiwa kura.

Nahisi JF wangekusanya nyuzi ambazo ni nzuri halafu waziweke kwenye makundi kama uchumi siasa michezo n.k then wakishapata thread chache kila kundi watazi post hizo thread ambazo ni bora ili sasa watu wapate muda wa kusoma thread chache zilizochaguliwa na kama ni kura sasa ndo watapiga.

So far, mi naona ni kama disco limejaa wamasai... kila mtu anapost tu chochote anachojiskia. Naona very soon maana itapotea kwa sababu watu wanaanza kuposti mawazo ya kijasiriamali badala ya stories za kubadilisha jamii

Maxence Melo
 
Imeelezwa kwa uwazi kabisa (soma palipoandikwa ZINGATIA). Wewe andika kadiri uwezavyo, huenda ni miongoni mwa maandiko yako mojawapo likashinda.

Hata mtu angekuwa na ID 20, haziwezi kushinda zote. Wakati wa kufanya uamuzi washindi watakuwa contacted.

Asante
Kama hutojali mkuu naomba nifafanuliwe hili sharti.

Mtajuaje kwamba andiko hili limechochea mabadiliiko katika nyanja husika.

Je, mtajua limechochea mabadiliko kwa andiko hilo kuwa na likes nyingi ?

Mtajua limechochea mabadiliko kwa andiko hilo kuwa na comments nyingi ?

Au mtajua limechochea mabadiliko kwa andiko hilo kuwa na viewers wengi ?

Au mtajua limechochea mabadiliko kwa andiko hilo kuwa na votes nyingi ?

Ni sifa zipi hizo ambazo zitakuwa zimetafsiri kwamba andiko hili sasa limechochea mabadiliko ?

Naomba ufafanuzi Maxence Melo
 
Mods mjibu swali kuandika uzi zaidi ya mara 1 inaruhusiwa?

Na mmejipangaje kupambana na watu wenye ID zaidi ya 2 ktk shindano ilo?
Unafeli kabla ya kuanza mtihani... soma maelekezo mwanzo mpaka mwisho... umeambiwa unaweza kuandika mara nyingi uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda.
 
Back
Top Bottom