Shinyanga: Askari watuhumiwa kuvujisha siri za Wananchi wanaotoa taarifa za wizi wa mafuta ya SGR

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Imebainika kuwa baadhi ya askari wa Shinyanga wanavujisha taarifa za siri zinazotolewa na wananchi juu ya wahalifu wakiwemo wezi wa mafuta katika ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.

Wakizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi baadhi ya Wananchi wamedai kuwa wizi unachangiwa na viongozi wa ngazi ya juu, wakipewa taarifa wanawakamata wezi lakini baada ya muda wanawaachia.

Robert Magisi mmoja wa mkazi wa eneo hilo amesema “Wanaficha mafuta kwenye familia zetu, tunawafahamu, ni miongoni mwa viongozi na wananchi wa kawaida."

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

Naye, Charles Mwiniwe ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwalugoye amesema "Ukitaka maisha yako yawe mafupi basi udili na mafuta ya SGR, haya mafuta yanaibiwa na kupelekwa Mwakitolio kule machimboni, nitoe rai kwa Wananchi wenzangu hizi mali zinazoibiwa ni mali za Watanzania si za Wachina.

Hali hiyo ACP Janeth Magomi kutahadharisha kuchukua hatua madhubuti za kinidhamu ili kukomesha hali hiyo kwa askari wake wasio waaminifu.

Amesema “Tutawalinda wananchi wote watakaotoa taarifa za wizi wa vitu vya mradi, hatutavujisha taarifa, huu ni mkubwa, ni mradi wa Watanzania wote.”

Chanzo: Azam TV
 
amna lolote sgr,daraja la Busisi wanaiba sana. fuso linabeba simenti,nondo au mafuta ya wizi chini ya ulinzi wa askari wachache wasio waaminifu miaka nenda rudi na akuna cha kuwakamata wala kuwachukulia hatua.
 
Imebainika kuwa baadhi ya askari wa Shinyanga wanavujisha taarifa za siri zinazotolewa na wananchi juu ya wahalifu wakiwemo wezi wa mafuta katika ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.

Wakizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi baadhi ya Wananchi wamedai kuwa wizi unachangiwa na viongozi wa ngazi ya juu, wakipewa taarifa wanawakamata wezi lakini baada ya muda wanawaachia.

Robert Magisi mmoja wa mkazi wa eneo hilo amesema “Wanaficha mafuta kwenye familia zetu, tunawafahamu, ni miongoni mwa viongozi na wananchi wa kawaida."

Naye, Charles Mwiniwe ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwalugoye amesema "Ukitaka maisha yako yawe mafupi basi udili na mafuta ya SGR, haya mafuta yanaibiwa na kupelekwa Mwakitolio kule machimboni, nitoe rai kwa Wananchi wenzangu hizi mali zinazoibiwa ni mali za Watanzania si za Wachina.

Hali hiyo ACP Janeth Magomi kutahadharisha kuchukua hatua madhubuti za kinidhamu ili kukomesha hali hiyo kwa askari wake wasio waaminifu.

Amesema “Tutawalinda wananchi wote watakaotoa taarifa za wizi wa vitu vya mradi, hatutavujisha taarifa, huu ni mkubwa, ni mradi wa Watanzania wote.”

Chanzo: Azam TV
police hawanaga siri
 
Back
Top Bottom