Shinyanga: Polisi wafanikiwa kuzuia ndoa ya binti aliyefaulu kwenda kidato cha tano

Shinyanga: Polisi wafanikiwa kuzuia ndoa ya binti aliyefaulu kwenda kidato cha tano

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Ikiwa ni tofauti ya siku mbili tangu kuadhimishwa siku ya mtoto wa Afrika ilikwend ana kauli mbiu ya Mpe nafasi msichana boresha sheria ya ndoa na kuchagizwa na mabango yenye jumbe mbalimbali kama USINIPE MUME NIPE ELIMU.

Huko mkoani Shinyanga hali ni tofauti kabisa kwani imejitokeza tukio la kuozeshwa binti aliyefaulu na kuchaguliwa kwenda kidato cha tano. Wazazi wameona ni bora mtoto huyo akaolewe na kukatiza ndoto zake za kuendelea na maso.

=====
Jioni ya jana timu ya wataalam mbalimbali ikiambatana na Mhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christine Mndeme na vyombo vya DOLA wamefika katika kijiji cha Mwawaza na kufanikiwa Kuzuia NDOA ambayo Bi Harusi ni Mwanafunzi aliyechaguliwa kuingia kidato cha tano ila wazazi wake wakaamua KUMUOZESHA Sasa Hawa Wazazi watajua kuwa Shinyanga ya Mndeme ni ya ELIMU na SIYO kuoa WANAFUNZI.

Kwani afisa maendeleo na polisi si walikua wanatosha? Huyo mkuu wa mkoa alifata nini?
 
Kwenye mambo ya kutumia akili tunatumia nguvu kubwaa polee Tanzania…..sasa bunduki za nn apo,Aya tuseme bint alikuwa na mpango wa kwenda chuo
Acha tu hivyo nguvu itumike,laiti ungejaribu hata siku moja kuingia kuzuia mambo kama haya,ndo ungejua umuhimu wa kuwa na askari karibu.
Nimeipenda hiyo
 
Acha tu hivyo nguvu itumike,laiti ungejaribu hata siku moja kuingia kuzuia mambo kama haya,ndo ungejua umuhimu wa kuwa na askari karibu.
Nimeipenda hiyo
Sasa unazuia ndoa….unaruhusu zinaa

..Kwa hiyo mnatuonyesha ziwa huku mmeziziba chuchu…

Na uku mtaani kuna kuna wasome wengi hawana kazi wa ubunifu…wamebaki kuwa machawa
 
Ikiwa ni tofauti ya siku mbili tangu kuadhimishwa siku ya mtoto wa Afrika ilikwend ana kauli mbiu ya Mpe nafasi msichana boresha sheria ya ndoa na kuchagizwa na mabango yenye jumbe mbalimbali kama USINIPE MUME NIPE ELIMU.

Bwana na bi harusi wamepanda lendikruza ya mkuu wa wilaya badala ya baisikeli, kamati ya harusi ilikuwa na maono ya mbali.
 
Back
Top Bottom