Shinyanga: Polisi wafanikiwa kuzuia ndoa ya binti aliyefaulu kwenda kidato cha tano

Shinyanga: Polisi wafanikiwa kuzuia ndoa ya binti aliyefaulu kwenda kidato cha tano

Acha kuchanganya mambo hapo,kilichozuiliwa hapo ni ndoa ya Mwanafunzi,uliwahi ona wapi polisi wakija kuzuia ndoa ya mtu mwenye zaidi ya miaka kumi na nane na ambae siyo mwanafunzi,huyo msichana hapo ni mwanafunzi,tena mwanafunzi wa sekondari,bora angekuwa chuo,na awe na zaidi ya miaka kumi nane,hakuna ambae angeenda kuzuia hiyo ndoa.

Huyo ni mwanafunzi wa shule gani?

Huyo binti kisheria sio mwanafunzi.

Maana ameshamaliza form 4 na bado hajaanza form 5. Hivyo sio mwanafunzi.

Na pia kwenda form 5 sio lazima ni uamuzi wake.

HAKUNA SHERIA YOYOTE ILIYOVUNJWA. NDOA NI HALALI
 
li mwanahabari lililotuletea habari sijui na lenyewe lili drop out of school kwenda kuolewa ???

hatujui binti ana umri gani

hatujui sheria inasemaje

hatujui tangazo la ndoa la wiki tatu lilipita pitaje wilayani, kanisani au msikitini

au kama lilikuwepo hilo tangazo ambalo huwa lina biographical particulars za wachumba

hatujui kama wamekaidi rejection letter ya serikali kupinga ndoa hii

hatujui hapo ni ngomani, bomani, kanisani, msikitini au kwenye kigodoro

tunajadli blindly tu, hatuwezi kuchambua mambo kiundani, ndio maana tunauzwa kwa Waarabu
 
Hovyo kabisa. Si mlisema wenyewe wakasome tu hata kama wamezaa? Mwacheni basi aolewe na shule ataenda tu na mimba yake, wa kulipa ada keshapatikana.
Magufuli hakika aliona mbali
 
Kila mtu na maisha yake na bahati zake wazazi wa bint X wa meamua kuozesha bint yao kwa kijana msomi kijijini kwao anae miliki maduka ya holiselo na kituo cha mafuta, ili amsaidie kuendesha biashara kama mwana familia kwa kulidhia pande zote mbili wazazi wa bint na wa kijana tajiri.

Inakua je police inakuja kuvamia shughuri za harusi na kupiga wazazi na bibi harusi watakua wamevunja sheria ipi? bint wengi wana elimu ya juu ila wengi wanakosa ajira na ndoa na wanatamani sanaa bora wapate ndoa.

kwani mtu akiwa anapenda kusoma mpaka chuo kikuu hawezi kujiendeleza akiwa kwenye ndoa, kupata ndoa ni ngumu kuliko kupata ajira siku hizi huyu bint kalata vyote kosa lake liko wapi? kwani police ina weza kupenda mwanao kuliko mzazi wa mtoto? Wakisema kulinda elimu ya mtoto wakike tunakalilishwa na kuondoa reasoning bint wa miaka 20 na kamaliza form 4 ana utashi (passion) zake, kwanini alazimishwe kusoma form five na six wakati yeye kaona mwanga kwenye kuolewa.
 
Huyo ni mwanafunzi wa shule gani?

Huyo binti kisheria sio mwanafunzi.

Maana ameshamaliza form 4 na bado hajaanza form 5. Hivyo sio mwanafunzi.

Na pia kwenda form 5 sio lazima ni uamuzi wake.

HAKUNA SHERIA YOYOTE ILIYOVUNJWA. NDOA NI HALALI
Swadakta kabisa. Wakiulizwa ni mwanafunzi wa shule gani watajibu nini? Wakipata mwanasheria mzuri hakika mkuu wa mkoa na wafuasi wake wataaibika sana.
 
Kila mtu na maisha yake na bahati zake wazazi wa bint X wa meamua kuozesha bint yao kwa kijana msomi kijijini kwao anae miliki maduka ya holiselo na kituo cha mafuta, ili amsaidie kuendesha biashara kama mwana familia kwa kulidhia pande zote mbili wazazi wa bint na wa kijana tajiri.

Inakua je police inakuja kuvamia shughuri za harusi na kupiga wazazi na bibi harusi watakua wamevunja sheria ipi? bint wengi wana elimu ya juu ila wengi wanakosa ajira na ndoa na wanatamani sanaa bora wapate ndoa.

kwani mtu akiwa anapenda kusoma mpaka chuo kikuu hawezi kujiendeleza akiwa kwenye ndoa, kupata ndoa ni ngumu kuliko kupata ajira siku hizi huyu bint kalata vyote kosa lake liko wapi? kwani police ina weza kupenda mwanao kuliko mzazi wa mtoto? Wakisema kulinda elimu ya mtoto wakike tunakalilishwa na kuondoa reasoning bint wa miaka 20 na kamaliza form 4 ana utashi (passion) zake, kwanini alazimishwe kusoma form five na six wakati yeye kaona mwanga kwenye kuolewa.
Tuache kuingilia maamuzi ya familia kwa sababu wanaelewa bint zao kuliko watu baki ila tujikite kwenye kuelimisha watoto wakike vijijini na kutoa muamuko kwa wazazi.
 
Ikiwa ni tofauti ya siku mbili tangu kuadhimishwa siku ya mtoto wa Afrika ilikwend ana kauli mbiu ya Mpe nafasi msichana boresha sheria ya ndoa na kuchagizwa na mabango yenye jumbe mbalimbali kama USINIPE MUME NIPE ELIMU.

Huko mkoani Shinyanga hali ni tofauti kabisa kwani imejitokeza tukio la kuozeshwa binti aliyefaulu na kuchaguliwa kwenda kidato cha tano. Wazazi wameona ni bora mtoto huyo akaolewe na kukatiza ndoto zake za kuendelea na maso.

=====
Jioni ya jana timu ya wataalam mbalimbali ikiambatana na Mhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christine Mndeme na vyombo vya DOLA wamefika katika kijiji cha Mwawaza na kufanikiwa Kuzuia NDOA ambayo Bi Harusi ni Mwanafunzi aliyechaguliwa kuingia kidato cha tano ila wazazi wake wakaamua KUMUOZESHA Sasa Hawa Wazazi watajua kuwa Shinyanga ya Mndeme ni ya ELIMU na SIYO kuoa WANAFUNZI.

Pumbafu wanaingilia maamuzi ya mtu ikifika kwenye swala la ajira wajitoa
 
Huyo ni mwanafunzi wa shule gani?

Huyo binti kisheria sio mwanafunzi.

Maana ameshamaliza form 4 na bado hajaanza form 5. Hivyo sio mwanafunzi.

Na pia kwenda form 5 sio lazima ni uamuzi wake.

HAKUNA SHERIA YOYOTE ILIYOVUNJWA. NDOA NI HALALI
Mwanafunzi haijalishi kuwa ameenda shule au hajaenda shule,taarifa inasema kwamba anatarajiwa kuingia kidato cha nne, kwa maana hiyo bado anahesabika kama mwanafunzi,kama angekuwa hayupo katika mahesabu ya kwenda shule, basi ungekuja kutetea hoja yako hii dhaifu.
Kama utasema huyo bado hajaenda shule,basi na hawa wengine wakiwa likizo tutasema hivi hivi kwamba bado hawapo shuleni, na kama kwenda shuleni ni hiyari, kwanini asingejitoa kwenye uanafunzi, lakini haiwezekani mtu bado upo kwenye mahesabu ya wanafunzi halafu aje mtu kusema kwamba eti shule ni hiyari,hivi unajua kweli kidato cha tano na sita bado ni wanafunzi ama na wewe tukupe mtihani wa uelewa
 
Hujajibu swali langu , Bibi harusi ni mwanafunzi wa shule gani ? Na anasoma kidato cha ngapi ?

Nijibu haya maswali ili tujue sheria gani imevunjwa
 
Hujajibu swali langu , Bibi harusi ni mwanafunzi wa shule gani ? Na anasoma kidato cha ngapi ?

Nijibu haya maswali ili tujue sheria gani imevunjwa
Uliza mwaswali yenye akili,taarifa inasema anakwenda kujiunga na kidato cha tano,wewe unakuja na maswali anakwenda shule gani.
Imetumika lugha tahisi sana, huyo ni Mwanafunzi,we unakuja kuuliza shule gani.
hii inaashiria hata uwezo wako wa kufahamu kidato cha tano ni kitu gani bado ni uwezo mdogo sana.
 
Usihamishe hoja ya maswali yangu.

Kuhamisha maswali sio sahihi maana Hiyo ni mbinu ya kushinda debate kitaalamu inaitwa strawman fallacy

Hakuna sehemu nilipoandika anakwenda shule gani ?

Maswali yangu ni haya hapa. Copy and paste sijabadili chochote

Bibi harusi ni mwanafunzi wa shule gani ? Na anasoma kidato cha ngapi ?

Nijibu haya maswali ili tujue sheria gani imevunjwa
 
Kama mtu anataka kudanga,adange tu,ila asiwe mtoto wala mwanafunzi,kusoma na kupata ajira ni ishu nyingine,muache asome,siyo unakuja kusema eti kwa sababu ajira hakuna basi asisome,kha ya wapi haya.
Halafu mbona unakomalia sana huyo mwanafunzi kuolewa,au na wewe ndo wale wale
Mtoto kwa huyo bint anamiaka mingapi…?

Afu kwenye harusi why polisi waje na mtutu wa bunduki…..yaani polisi wanajifanya intelligencia kwenye mambo ya ndoa wanashindwa kuwa kwenye mambo ya kiusalama……watu wanauliwa uko na watu wasiojulikana na polisi wapo..

Kwani ndoa ni kifo….?
 
Advance yaani form V na VI ni chuo? Kwani ukimpa mimba mwanafunzi wa form 5 au 6 hufungwi?
Eeh sifungwi…

Sema tu mfumo wa elimu bongo zero square,anaemaliza adv akifaulu anenda degree chuo na aliemaliza diploma chuo akifaulu anaenda degree chuo…..Apo ndo utajua advanc level na ordinary level
 
Nchi ya ajabu sana hii. Sheria ya ndoa ya Tanzania iansema wazazi wana haki ya kumuoza binti yao akishatimiza umri wa miaka 14.Mahakama kuu kupitia kesi ya Mwanaharakati Rebecca Gyumi ilishatoa hukumu kuitaka serikali kubadilisha hiyo sheria ya ndoa hadi binti atimize miaka 18mlakini mpaka leo serikali imeshindwa kupeleka mswada bungeni kuifanyia marekebisho sheria hiyo badala yake watendaji wake wamebaki kutengeneza maigizo kama hayo ya kuvamia ndoa za watu na kuzizuia ilihari serikali yenyewe inaziunga mkono ndoa hizo kupitia sheria zake yenyewe.Ndio maana huwezi kusikia muoaji wala wazazi wa bibi harusi kushitakiwa kwa kumuoza binti chini ya miaka 18 kwa vile hakuna kosa walilotenda kwa mujibu wa sheria.Ni muda sasa hawa watendaji wa serikali na serikali yenyewe kushitakiwa na kudaiwa mabilioni ya pesa watakapo thubutu kuvamia na kuvunja sherehe za harusi za watu zinazofanyika kihalali ili waache haya maigizo yao ya kipuuzi.Kama hawazitaki hizi ndoa kwanini mpaka leo serikali imeshikwa na kigugumizi kubadilisha sheria hiyo ya ndoa.
 
Huyo ni mwanafunzi wa shule gani?

Huyo binti kisheria sio mwanafunzi.

Maana ameshamaliza form 4 na bado hajaanza form 5. Hivyo sio mwanafunzi.

Na pia kwenda form 5 sio lazima ni uamuzi wake.

HAKUNA SHERIA YOYOTE ILIYOVUNJWA. NDOA NI HALALI
Ongezea apo mkuu na mwanafunzi Ana miaka 19
 
Timu ya Wataalamu wa msaada wa kisheria kutoka Mama Samia Legal Aid Campaign ikishirikiana na RC wa Shinyanga, Christina Mndeme na Jeshi la Polisi Shinyanga wamefanikiwa kuzuia ndoa ya Binti aliyefaulu kuingia kidato cha tano lakini Wazazi wake waliamua kumuozesha katika kijiji cha Mwawaza nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga.

Timu hiyo ilifika eneo la tukio na kushuhudia zoezi la uzuiaji na kukamata walengwa ambapo RC wa Shinyanga amesema ndoa hiyo ililenga kuzima ndoto za Binti huyo.

Mndeme amesema Mkoa wa Shinyanga hauko tayari kuona Watoto wa kike wanashindwa kufikia ndoto zao kwa ajili ya Wazazi wachache wenye tamaa ya mali, ambapo ameagiza Wazazi hao ambao wametoweka kufika Kituo Kikuu cha Polisi Mjini Shinyanga “Serikali ya Mkoa wa Shinyanga itasimamia Binti huyu apate haki ya msingi ya kupata elimu ili aweze kufikia ndoto zake”
 
Back
Top Bottom