Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kutaka wizara ya afya kutokukimbilia chanjo ya Corona, Shirika la Afya Duniani WHO imeitaka nchi hiyo kujiandaa na chanjo ya Corona kama mataifa mengine duniani.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, mkuu wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshdiso Moeti amesema kuwa Tanzania inatakiwa kutumia mwanya wa upatikanaji wa chanjo kwa faida ya wananchi na kanda ya Afrika Mashariki kwa ujumla.
''Tumeanza kuwasiliana upya na ngazi za juu za uongozi, na tunatoa mchango wetu kama ilivyokua hapo mwanzo, na tunataka kushirikiana na Tanzania, kwa niaba ya watu wa Tanzania, nchi jirani na dunia kwa ujumla. Sehemu ya mawasiliano yetu na Tanzania ni kukumbusha serikali kuwa, hii ni sehemu ya makubaliano ya kanuni za afya za kimataifa ambapo nchi wanachama wamekubali kwa pamoja kuzuia kusambaa kwa magonjwa'' anasema Dkt. Moeti.
WHO inasema kuwa imekua ikitoa mchango na kuwasiliana na serikali ya Tanzania kuanzia mwanzo wa janga hili la Corona. Shirika hilo pia limesisita Tanzania kutoa takwimu za mwenendo wa Corona nchini Tanzania ili iwe rahisi katika kupambana na kuzuia maambukizi mapya.
Naye katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus anasema anaunga mkono alichosema @MoetiTshidi, anatoa rai hatua dhabiti za kiafya kukabiliana dhidi ya corona zinapaswa kufuatwa na kujiandaa kupokea chanjo.
Takwimu ni suala la muhimu pia kwa Tanzania kuzitoa, tena baada ya kesi za miongoni mwa wasafiri na wageni katika miezi ya hivi karibuni.
Chanzo: BBC SWAHILI
Ishu ya chanjo hii ya COVID 19 inahusishwa na swala zima la IMANI kuwa chanjo hii ndani yake imebeba alama ya mpinga Kristo 666...
Mch. Josephat Gwajima ndiye mshauri mkuu wa Rais Magufuli kwa sasa kuhusu hili. Kwa lugha nyingine ni kuwa Rais Magufuli, ameamini na anafanya kila linalowezekana kwa kutumia mamlaka yake ya Urais kuwalinda watu wake na Mpinga Kristo na alama 666...
Anaihusisha chanjo ya COVID 19 na na alama ya mpinga Kristo 666 na kuwa yeyote anayeipokea chanjo hiyo anakuwa ameikubali namba na alama ya Mpinga Kristo 666 na kumkana Yesu Kristo...
Lakini swali kubwa ni hili: ATAWEZAJE? Na je, Biblia inasemaje?
Neno la Mungu liko wazi sana. Kwamba, wokovu unamfuata na kupokelewa na mtu mmoja mmoja kwa kadiri anavyosikia Neno la Mungu na kuliamini...
Kwa hiyo, Tanzania ina jumla ya watu wanaokaribia 60,000,000. Neno la Mungu linasema "....kila aaminie ataokoka...."
Neno la Mungu halisemi, "...amri au misimamo ya Rais wa nchi fulani itawaokoa watu wake..."
Rais naye ni mtu. Imani yake kwa Mungu aliye hai ktk Yesu Kristo ndiyo itakayomponya. Kwa hiyo kama anaamini, anafanya vyema sana, amechahua fungu sahihi na salama.
Anachotakiwa kufanya ni kutumia nafasi yake ya Urais kuihubiri injili ya Kristo ili watu waamini na kuchagua uhai badala ya kifo...
Aidha Neno la Mungu linasema, "... kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe. Baba hatachukua dhambi za mwanaye, vivyo hivyo mwana hatabeba dhambi ya wazazi wake...."
Ninachotaka kusema ni hili, kuwa, chanjo ya COVID 19 itaingia Tanzania. Rais Magufuli hawezi kuzuia hili...
Kama ni kweli, chanjo hiyo imebeba alama ya mpinga Kristo 666, basi uamuzi wa kuipokea au kuikataa unabaki wa mtu mmoja mmoja kwa kadiri ya imani yake...
Maana, Mungu anasema hivi; "....Tazama nimeweka LAANA/MAUTI na BARAKA/UZIMA mbele yako. Chagua uzima ili uishi..."
Uchaguzi (choice) uko kwa mtu mwenyewe binafsi kwa kadiri ya kuamini kwake...