#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

Watu wengi hamna taarifa za kutosha. Unajua kwamba ukishapata chanjo bado utaendelea kuvaa barakoa na tahadhari zingine?

Ni vema mjitahidi kupata taarifa sahihi kabla ya kuweka ushabiki kwenye afya zenu. Kumbuka uhai hauna shamba kwamba utavuna tena. Ukiondoka haurudi. Nakuwekea hapo chini baadhi ya taarifa za CDC. Soma mwenyewe kama lugha ya wenyewe inapanda, amua mwenyewe kwa kuwa na taarifa sahihi
Kuwa HIV + hakukufanyi kutokujikinga kwa kuvaa Condom unapo-sex.

Hilo pia lita apply hata kwenye covid19 hata baada ya kupata chanjo, virus wenyewe wanabadirika chief.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mwisho wa siku hii chanjo tutapewa bure huku wengine wakiinunua kwa gharama mara mbili!

Saa nyingine mikwara ya JPM inasaidia sana.
😅😅😆
 
Kuwa HIV + hakukufanyi kutokujikinga kwa kuvaa Condom unaposex.

Hilo pia lita apply hata kwenye covid19 hata baada ya kupata chanjo, virus wenyewe wanabadirika chief.
Tatizo unaongea unavyowaza sio uhalisia ulivyo. Maadam afya ni yako uamuzi ni wako. Hakuna chanjo ya gonjwa jipya ambalo hata wataalam hawajalijua vyema inatoka ndani ya muda mfupi. Kila la kheri katika kuwasaidia kufanya majaribio.
 
  1. Wazee zaidi ya miaka 64 ni 3.8% 2.3M
  2. Miaka 36-63 ni 16.6% 10.2M
  3. Miaka 15-35 ni 35.5% 21.8M
  4. Miaka chini ya miaka 15 44% 27.1M
Jumla watu 61.5M. Tunahitaji chanjo kwa watu kuanzia miaka 36 kwasababu chini ya hapo wanaweza kuhimili huu ugojwa na hakuna rekodi ya vifo kubwa. Hivyo tunahitaji chanjo milioni 12.5M. Ambao hawataki zitakuwa akiba.
 
  1. Wazee zaidi ya miaka 64 ni 3.8% 2.3M
  2. Miaka 36-63 ni 16.6% 10.2M
  3. Miaka 15-35 ni 35.5% 21.8M
  4. Miaka chini ya miaka 15 44% 27.1M
Jumla watu 61.5M. Tunahitaji chanjo kwa watu kuanzia miaka 36 kwasababu chini ya hapo wanaweza kuhimili huu ugojwa na hakuna rekodi ya vifo kubwa. Hivyo tunahitaji chanjo milioni 12.5M. Ambao hawataki zitakuwa akiba.
Kachanjwe ww na familia yako! Wengine tunayo kinga tayari!
 
Upumbavu kama huu unakera sana; Uingereza vifo vimeongezeka maradufu (kwa mujibu wa BBC Jana, labda kama waongo).

Saivi wanataka kuleta chanjo kwetu, siwakawa chanje watu wao kwanza? Who told them that Tanzanian corona situation needs such emergencies?
 
Bado sijaelewa hii chanjo ni hiari ya mtu au ni lazima kila mwananchi anatakiwa apate
 
Democrasia mabeberu wasitulazimishe sisi hatutaki izo chanjo zao. Kwann ya lazima. Corona yenyewa, yakutafuta tu, imebuma, haipo. Chanjo zao wapeleke Kwao
 
Serikali lazima ikubali kupokea chanjo na kama inakataa lazima kuwa na hoja za msingi sana za kushawishi kuwa sio chanjo bora au ina shida. lakini kuikataa tuu haitawezekana kwa sababu uchumi wetu na kila kitu kinategemea muingiliano wa watu ni lazima chanjo tukubali kwani hili ni jambo jema kwani tuna chanjo nyingi sana tumezikubali na zimeonesha ufanisi mkubwa....
Naona mmeanza kupata akili
 
Hatuangalii historia we mtu mwetu mweusi. Huyuu ndo atakuwa wa kwanza kushinda hao waume zako beberuru..alaf kizaz chako cha vilaza ndo kitaanza kutambua kuwa kuna rais wa africa aliewah kuahinda beberu.
Atashinda vipi ikiwa hta bunduki anasubiri atengenezewe na beberu!?
 
Mimi
Yako itakuwa akiba! ndugu yako akibanwa kifua kwa ugojwa ukianza kulia chanjo itakuwepo. Ukibanwa kifua utasahau hata kusali uliza ambao wana pumu mbaya!
Mimi na watanzania hatutabanwa kifua! Labda wewe na familia yako kama mnatamani saana kubanwa na kifua kabebeleeni hizo chanjo msijaze kwenye majokofu kwa akiba! Aliyekuambia zina tibu ni nani huyo!? Jidunge sumu tu urudishe namba mapema!
 
Dunia ni Kijiji, vyema tupate hizo chanjo ili kuruhusu watu waendelee na biashara zao hasa za kusafiri bila kuwekewa vikwazo vya kusafiri.

Tukikaidi kupewa chanjo hakuna Mtanzania ataruhusiwa kusafiri nje ya Mipaka.
Kwani hio Chanjo kazi yake ni nini?
 
"Chanjo hazifai kama Wazungu wangekuwa na uwezo wa kuleta chanjo, hata chanjo ya UKIMWI ingekuwa imeshaletwa, chanjo ya kifua kikuu ingekuwa kifua ingeshaondoka, hata chanjo ya malaria ingekuwa ishapatikana hata chanjo ya kansa ingekuwa imeshapatikana, lazima watanzania tuwe waangalifu kwa mambo ya kuletewa letewa,” Nukuu
 
Kama tuliweza kufuata dawa huko madagasca.

Tena waziri akapiga kikombe hadharani.

Kisha tukaambiwa zitafanyiwa utafiti ambao hadi leo hatujapewa majibu.

Wala hatufahamu yale maboksi ya dawa bado yapo,wamekunywa wao ama yalimwagwa baharini.

Kama tuna wasiwasi,kipi kinatushinda kufanyia utafiti hizo chanjo?

Tuyachukue yale mapapai,mbuzi wenye corona,kisha tuwapige chanjo.
 
Back
Top Bottom