Maeneo kadhaa huko Mbopo, Kinondo na sehemu fulani huko Mabwepande shirika la DDC linadaiwa kuvamia raia na kuyapora maeneo wakidai ni ya kwao. Nyumba zinavunjwa viwanja walivyonunua wananchi kwa taratibu kabisa na uwepo wa wajumbe wa maeneo husika lakini wanakuja kuwapora huu ni uvunjifu wa HAKI za binadamu na haikubaliki kunyanyasa raia wa nchi hii.
Ombi kwa serikali kuu ingilieni mtafaruku huu utasababisha uvunjifu wa amani pasipo sababu zozote. Muda wote walikuwa wapi hao DDC wakavizia wananchi wameuziwa na kujenga nyumba kisha waende kupora ardhi na kuvunja nyumba zao bila fidia?
Mada iko mezani wadau na wanasheria jitokezeni kukomesha uonevu huu. Mbunge wa Kawe yuko wapi?
Mabwepande, Mbopo-Kawe
Jumamosi, 1/7/2023
Mkutano wa RC-DSM na wananchi
Ngoma nzito
Jumapili, 2/7/2023
Mkutano wa M/kiti CDM Tundu A. Lissu na wananchi
Maswali magumu yaibuliwa
1. 1981 uongozi wa Dar kipindi hicho ulikataa maombi ya DDC kupewa ekari 1,931 mabwepande
2. 1984 DDC walifanya namna wakapewa hizo ekari 1,931 ikijumuisha mtaa wa Mbopo
Maswali magumu
1. Serikali au DDC ilitoa taarifa kwa wakazi wa eneo hilo kabla halijatwaliwa?
2. Kuna mthamini wa ardhi kutoka katika taasisi ya serikali alitumwa kwenda kutathmini thamani ya ardhi ambayo ilitakiwa kupewa DDC na wakazi wake wakalipwa fidia?
3. Ni mkazi gani wa eneo la Mabwepande na Mbopo alilipwa fidia kwa kutwalia eneo lake?
4. Je, DDC walifuata taratibu za umiliki ardhi ya ekari 1,931?
5. Je, nyaraka walizonazo DDC kuhusu umiliki la eneo la Mbopo Mabwepande ni halali?
6. Je, kuna tangazo la serikali au tamko la Rais la kufuta kijiji cha Mbopo Mabwepande na kuwaa eneo lao kwa matumizi ya umma?
7. Je, DDC wana miliki ardhi ya ekari 1,931 kwa kuzingatia sheria na taratibu katika kijiji cha Mabwepande na mtaa wa Mbopo?
Kama maswali hayana majibu kwa ushaihidi usio na shaka basi DDC hawana ardhi Mabwepande na Mbopo.