Bora hata Lukuvi! Japo na yeye ni mwana CCM yule yule lakini angalau mambl ya ardhi alikuwa anayaweka sawa kwa kiasi fulaniNinajua vizuri sana hili sakata na kesho nitakuja na Uzi kuhusu eneo hili ambalo aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwan Kikwete aliwauzia wawekezaji kutoka Uturuki bila uhalali Sasa mwekezaji aliyeuziwa anadai eneo lake anataka kujenga malls. Ridhiwan aliwadanganya Waturuki eti eneo hilo ni pori na akaliondoa kwenye ramani ya google. Dogo jizi sana.
Hivi hao DDC wanakuwa ni wazalendo wanapigania ardhi ya serikali au watendaji wana lao jambo?Mleta mada anaelekea ni mmoja wa wavamizi huko. Ni hivi DDC wana hati ya miaka 99 tangu miaka ya 1970. Mmeenda huko kichwakichwa mkauziwa mkapigwa na madalali wezi . Sasa DDC wanataka eneo lao haki yao wengi humo wamekaa miaka 5 HADI 7 tu hawana haki ya adverse possesion . DDC wamewapa nafasi ya kukubaliana mlipe kidogo mnakataa. Kwanza mlitakiwa mnyongwe wezi wakubwa kama Magufuli.
Hata pale wazo kiwanda cha cement ni hivo hivo. LIPA AU ONDOKA BAAASI.
Tatizo letu wa Tanzania Tunapenda Mteremko! Eneo ni la DDC walipewa miaka ya 70, Serikali ikijuwa kuwa mji wa Dar utapanuka! Mfano pale palipojengwa Hosp ya Mlonga nzira Serikali ilipagawa kwa Muhimbili miaka mingi sana hiliyopita enzi ya Mwalimu Nyerere. Ukiwa smart unatakiwa nunua kiwanja kilichopimwa na sio skwata. Tuache kulia liaMaeneo kadhaa huko Mbopo, Kinondo na sehemu fulani huko Mabwepande shirika la DDC linadaiwa kuvamia raia na kuyapora maeneo wakidai ni ya kwao. Nyumba zinavunjwa viwanja walivyonunua wananchi kwa taratibu kabisa na uwepo wa wajumbe wa maeneo husika lakini wanakuja kuwapora huu ni uvunjifu wa HAKI za binadamu na haikubaliki kunyanyasa raia wa nchi hii.
Ombi kwa serikali kuu ingilieni mtafaruku huu utasababisha uvunjifu wa amani pasipo sababu zozote. Muda wote walikuwa wapi hao DDC wakavizia wananchi wameuziwa na kujenga nyumba kisha waende kupora ardhi na kuvunja nyumba zao bila fidia?
Mada iko mezani wadau na wanasheria jitokezeni kukomesha uonevu huu. Mbunge wa Kawe yuko wapi?
Wee mtu DDC ni Dar es Salaam Development Corporation-Shirika la Maendeleo la Dar es SalaamKirefu chake ni 'District Development Cooperation-DDC' likijumuisha wilaya zote za wakati huo za Dar Es Salaam ambalo lilianzishwa na serikali mnamo tarehe 18/5/1971 na miradi yake ilikuwa DDC Kariakoo, DDC Mlimani, DDC Magomeni, DDC Keko, Garage, Mashamba nk
Bora hata Lukuvi! Japo na yeye ni mwana CCM yule yule lakini angalau mambl ya ardhi alikuwa anayaweka sawa kwa kiasi fulani
Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Hilo suala la Mbopo, Mabwepande, Kinondo, Malolo na maeneo ya karibu na huko ni mfupa mgumu ambao Lisu na CHADEMA wameamua kuutafuna. Tusubiri tuone mwisho wake maana ndani ya huu mgogoro kati ya DDC na hao wananchi wa huko kuna mambo mengi yenye utata sana na hayaelezeki kabisa katika hali ya kawaida:-
Mfano mdogo tu ni:-
1. Juu ya hati ya hilo eneo ambalo DDC wanasema wanalimiliki kuna wananchi zaidi ya 100 wana hati halali. Hati juu ya hati tena 100 ni Mabwe pande, Mbopo, Malolo, Kinondo na meneo ya karibu na huko ndio pekee yake duniani unaweza
kukuta hili jambo.
2. DDC wanasema ni eneo lao lakini wakifika kwa watu ambao wanafanya kazi kwenye vyombo vya dola, wastaafu waliokuwa na dhamana serikalini na matajiri wanawaruka hawagusi ardhi zao badala yake wanaenda kupora ardhi ya wasio na uwezo.
3. DDC sio kampuni ya upimaji ardhi na hakuna sehemu popote inayoonyesha kuwa wao ni wataalamu wa mipango miji lakini inasemekana wao ndio wanapima ardhi na kupanga mji - kuna nini hapa?
4. DDC wanapima viwanja vya 20 X 20 ambavyo serikali kupitia waziri Mabula alikataa ukubwa huo wa viwanja wao wamepata wapi hayo mamlaka kwenda kinyume na waziri? Na ardhi iliyobaki wanaichukua wao baada ya kumuachia 20 x 20 waliyemkuta kwenyeneneo hilo. Kwa wale ambao hawajajenga wantwaa ardhi yote.
Hayo ni machache tu yapo mengi kwenye huo mgogoro na kubwa zaidi wale wote wenye dhamana wanauogopa huo mgogoro labda tungojee Mheshimiwa raisi Samia mwenyewe aje aingilie kati na kuutatua kwa kuwa wasaidizi wake wote wanauogopa. Na mbaya zaidi hata Gwajima na ujanja wake wote na ambaye ndiye mbunge wa hilo eneo japo aliingilia kati kwa mbwembwe baada ya kupewa vielelezo na kujiridhisha kuwa wananchi wana haki na yeye katulizwa ghafla.
DDC wana hati miliki hadi mwaka 2070 (miaka 99-1971 hadi 2070)na wanalipia,muda huu ndiyo wameamua kulitumia eneo lao suala la walikuwa wapi halihusiani.Nimepata taarifa hapa kuwa mkuu wa mkoa anaenda huko ijumaa hii saa nne asubuhi. Kama amepata taarifa sahihi na anakwenda kuumaliza huo mgogoro litakuwa jambo jema sana kwa wakazi wa huko hasa ukizingatia wao wapo hapo zaidi ya miaka 40 (tangu 1970). Je DDC alikuwa wapi muda wote huo zaidi ya miaka 40 mpaka aibuke sasa hivi?
Mabwepande, Mbopo-KaweMaeneo kadhaa huko Mbopo, Kinondo na sehemu fulani huko Mabwepande shirika la DDC linadaiwa kuvamia raia na kuyapora maeneo wakidai ni ya kwao. Nyumba zinavunjwa viwanja walivyonunua wananchi kwa taratibu kabisa na uwepo wa wajumbe wa maeneo husika lakini wanakuja kuwapora huu ni uvunjifu wa HAKI za binadamu na haikubaliki kunyanyasa raia wa nchi hii.
Ombi kwa serikali kuu ingilieni mtafaruku huu utasababisha uvunjifu wa amani pasipo sababu zozote. Muda wote walikuwa wapi hao DDC wakavizia wananchi wameuziwa na kujenga nyumba kisha waende kupora ardhi na kuvunja nyumba zao bila fidia?
Mada iko mezani wadau na wanasheria jitokezeni kukomesha uonevu huu. Mbunge wa Kawe yuko wapi?
Ameongea vizuri kitu gani kwa kuanza kutoa vitisho badala ya busara za kiuongozi?RC Chalamila ameongea vizuri sana juzi Na wananchi wamemuelewa.
Sasa mgogoro unaenda kuisha itabaki historia tu.
RC Chalamila songa mbele ktk kutatua mgogoro huo.
Ameongea vizuri kitu gani kwa kuanza kutoa vitisho badala ya busara za kiuongozi?
Kutaka wananchi walipishwe shilingi 6500/4000 kwa mraba wa mita analomiliki mwananchi?
DDC alimlipa fidia nani wakati anapewa kumiliki hekari 1,931?
Kipi kilitangulia kuwepo maeneo ya Mabwepande na Mbopo na umiliki wa ardhi kwa hati yenye shaka.Ameshasema kila mtu anajua mwenyewe namna alivyopata eneo pale maana wengine waliuziwa kwa bei chee sawa na bure,
Wengine walifanya kuvamia maeneo ya watu ,
N.k.
Sasa kama mtu aliuziwa kwa bei sawa na bure inabidi anunue kwa bei halali awe mmiliki halali.
Ndiyo maana nikauliza hivi;
Je serikali ingeamua kupima na kuuza maeneo kule Mbopo kuuzia wananchi ingeuza kwa shilingi ngapi kwa SQM kwa bei ya soko ?