Kwa hapa tulipofikia ili twende na Kasi ya wakati huu wamabadiliko ya mifumo na vitu vyote nasema vitu vyote nikiwa na maana vitu vyote Vimeondoka kwenye teknolojia ya zamani na kuingia teknolojia mpya Sasa kwa vile sisi tulibaki kwenye mifumo ya zamani ambayo haitatuletea tija zaidi ya kutukomba hela za wanyonge ili kulipia uendeshaji usiolipa na hata kuzibadili kwa vipato vidogo hatuwezi maana tutafika tumechoka na tufika kwa vichache tutakuta mifumo imebadilika Tena, Sasa ili tufike bila kuumia inabidi hii mbinu ya uwekezaji ndo itumike kila chenye hasara na mifumo ya kizamani kiwekezwe ili tuweze kwenda na dunia na biashara za kisasa ila tunachopaswa kufanya nikuomba hiyo mikataba iwe wazi ili watanzania wajue Nini watachofaidika nacho.
Huko nyuma kidogo Kuna thread zilikuja kutushitua tujiandae na mabadiliko ya kimfumo ili tuendane na ulimwengu lakini watu walisema ni mbali sana Sasa ndo hivyo umbali umeondolewa kwa njia ya uwekezaji, mfano hili shirika la posta linajiendesha kwa mfumo wa kizamani Tena wa kizembezembe tu na huku operation zinahitaji hela ambayo inatoka kwenye Kodi, njoo hiyo TTCl yaleyale vocha hata kwenye miji mikuu hakuna, mwendokasi nao hivyohivyo hakuna magari ya kutosha Wala hawapo kwenye mikoa mikubwa, Sasa nchi ikiacha watu wake waishi kizamani yaani kikalekale unadhani hela zitatoka wapi si ndo mambo yakuuza korosho chafu ukizani unauzia watanzania wenzio kumbe unauza kwenye mataifa yenye teknolojia nzuri nao wanakurudishia bidhaa zako zisizo na viwango , haya tulizuia viwanda vya nguo Kuja kisa mafundi cherehani watapata shida Sasa Leo nguo za nchi nyingine ndo zinavaliwa huku mzigo wa nguo ukifatwa mbali kiasi Cha kufanya Bei iwe kubwa, Sasa ndo tunaona madhara ya kukumbatia mifumo ya kizamani.