Shirika la Posta laanza biashara ya mabasi mikoani

Shirika la Posta laanza biashara ya mabasi mikoani

Aisee!
Kwahiyo kwakuwa walikuwa na coaster wakisafirisha abiria na sasa wameleta mabasi makubwa biashara inabadilika au imekuwa?
Kuna muda kumuelewa mtanzania inahitaji remedial class ya unafiki tu!

Posta haijawahi kusafirisha abiria kwa Coaster acha uongo!

Coaster za Posta ni za mfumo wa fuso kusafirisha parcels na magazeti upcountry!

Na yalikua yanakosa mafuta kama yote!

Uchafu ule!Na walikua na gari ngapi?Gari chache kama zote!
 
Wanatuona mapoyoyo tukisema posta hamtakiwi huko hats km mliwahi mnajua KWA nn mlikufa?

Mmeshindwa kuboresha huduma mkafikia dhl bado mnayumba, basi imarishen benki na teknolojia mnakuja kuhangaika n oil
 
Vibasi 10 vya posta unavitungia ushetani?
Mkuu sikuelewa,wamevitungia masheria ya kizamani au nini?maana kiukweli ushindani wa mfano kabila fulani la kaskazini hata VAT ako allergic nayo na hawalipi, receipt hawatoi, mafuta wanajua wanayapata kwa bei gani, na upande wa pili wanakuamkia Shikamoo Mzee, kifurushi wanaweza hata wakakikuletea hata nyumbani kwa bodaboda, hapo ndio wasi wasi wangu labda kama itoke sharia kuwa vifurushi na mizigo ya serikali yote wapewe wao….
 
Rangi ya nyonya damu

Nina Imani hawa jamaa nao wanasoma hapa, kama walifanya research wanajua maana ya rangi, mimi sijui lakini nahisi walizitoa kwenye logo yao lakini mbona kuna rangi nyingi ambazo hazileti mtafaruku?maana hii rangi inaweza hata ikaleta hata ushabiki wa team za mpira. Ila pamoja na kuwa ni rangi ambayo huonyesha mapenzi lakini pia kuna sehemu nimekuta imeandikwa maneno ambayo unaweza usiyapende Red is the color of fire and blood, so it is associated with energy, war, danger, strength, power
 
Hayo mabasi ni injini mbele au nyuma

Ova
 
safi , siyo eti wachina wanakuwa na mabasi na ndio makondakita.

Shirika la Posta Kudos!!
 
Yaan bado yapo China hayajafika bongo
Sina hakika sana kama hiyo picha ni Tanzania kwa sababu zifuatazo.

1. Hayo mazingira yaliyopo hayo magari. (Inaonekana yako yard au indoor parking, kibongo ni ngumu).

2. Rangi ya hayo mabasi (Ni nadra sana kwa taasisi ya Umma hapa Tz kuwa na colour choice nyekundu).

3. Maandishi ya Kiingereza ubavuni mwa basi (Yaani washindwe hata kuandika hapa kazi tu! Wasiweke picha ya bendera ya Tz!)

4. Mantiki ya kuanzisha hiyo biashara (Haingii kabisa akilini)
 
Mkakati wa kuua biashara za watu binafsi umeanza siku nyingi, biashara ya malori imekufa, mabasi nayo kwishine
 
Wazo Zuri ila naona kama ni Project ambayo haitakua effective sana, Kuna Train ya Umeme inakuja why msiingie ubia na TRL mkanunua Behewa Moja likawa linasave Mikoa ambayo Train itapita, Lets Say Morogoro, Dodoma, Singida , Tabora, Mwanza Shinyanga, Kigoma,
 
Hili ni wazo zuri, japo POSTA wangejikita kubuni biashara ya kusafirisha vifurushi kuliko kuingilia biashara ya abiria.
Tusije tukaanza kusikia kampuni binafsi zinanyimwa leseni.
Kwani biashara ya abiria ina watu maalum wa kuifanya?
 
Magari yake yatakua na namba SU hata kama yanafanya biashara.

Kwangu naona ni IDEA nzuri kuounguza gharama za kusafirisha vifurushi.View attachment 1194462
Wazo lina nia njema.. Utekelezaji, usimamizi wa muda mrefu utawapa shida.... Kutegemea vifurushi kama chanzo kikubwa cha mapato si vyema..Upande wa usafirishaji wa abiria , watakuwa na changamoto, kiundeshaji, mfumo wa kishirika la umma, mwisho wa siku faida itakuwa ndogo..Wamuulize Sumry kwa nini ameuza mabasi Tanzania, nini kimetokea kwa Scandinavia, Kiswele, Air Msae na wengineo... Mabasi mengine unayoyaona, wamiliki wana biashara nyingine za msingi, ambazo zinaunga mkono biashara ya usafirishaji wa abiria ..Ni vizuri kuthubutu, lakini wangeweza kufikiri vyema zaidi.. Muda utatupa majibu... Muda ni mwalimu mzuri.
 
Yaani Mkuu Badala Ya Kuwaza Huduma Inaboreshwa Wewe Mwenyewe Umewaza Rangi?
Ulitaka Rangi Gani Sasa Ama Ulitaka Ile Ya Dhahabu 😃😄😅😂😁😁

Anataka kijanai na njano huyo..watu kama hawa akija kwako akakuta viti vyekundu anaweza hata kukaa chini..hahahha
 
SGR ikianza kazi malori mengi yatauawa kifo kibaya.
 
Tunapotaka kuingia kwenye biashara kama serikali nivyema pia tukafanya tathmini kwa wananchi wetu kwa maana ya mzunguko wa hela miongoni mwa wananchi, kufanya biashara kama hizi kwa serikali ni kuua sekta binafsi na kumfanya kila Mtanzania awe muajiriwa..

Ushauri kwa Serikali, Serikali ijikite kwenye biashara ambazo ni ngumu kwa raia wa kawaida kuifanya mfano Kiwanda cha kutengeneza Magari, Mitambo ya kusafisha mafuta, Ujenzi wa mabandari ya kisasa, uanzishaji wa shirika kubwa la Meli za mizigo to and out Tanzania.. Hizi biashara ndogondogo ziachwe kwa wananchi na ikiwezekana wawezeshwe wengi waweze kuzifanya na Serikali ibaki kuwa pivot tu..
 
Back
Top Bottom