Shirika la Posta laanza biashara ya mabasi mikoani

Shirika la Posta laanza biashara ya mabasi mikoani

Naona wanatengeneza njia ya kupiga pesa kupitia hii biashara ya mabasi. Story zitaanza fulani kanunua spea kwa bei kubwa, leo abiria hawakuwepo tulienda kwa hasara wakati ukweli ni kuwa gari ilijaa pomoni, gari haijaharibika utaambiwa tumenunua spea njiani, nk.
Technology inajibu changamoto zote ulizo zitaja.
 
ajabu sanaa... sasa mizigo na mabasi wapi na wap..?? au vifurushi watu ndo walengwa?? mie sion umuhimu hapo unless iwe target ni abiria
 
Shirika la posta ni shirika kubwa la usafirishaji vifurushi toka zamani.Shirika hili lilianza kupotea kwa kule kuzubaa kwao na kutoendana na teknolojia.Hawajitangazi yan kuwa la serikali basi kila kitu ni wateja wajiongeze.Hii mpaka leo ukimuuliza mtu kuhusu posta watakuambia ni mambo ya kutuma barua kitu ambacho technolojia ilishahama huko.Kwa baaz ndio walikuwa wakituma vifurush nalo tatizo likawa usafiri yaani kucheleweshewa na mbaya zaidi kupotea kwa vifurushi.Tatizo la kupotea kwa vifurushi kwa sasa limepungua kama sio kukoma.Changamoto ya usafiri naona ndio wanapambana nayo na kuna siku nilisoma kwamba Shirika linataka kununua ndege drones) kuyafikia maeneo korofi.Kipindi nafungua account posta mhudumu aliniambia hivi sasa masanduku ni dili yani kila leo watu wanachukua.Hii ni taarifa nzuri kwa taifa kikuwa ni wawe wanawajali wateja na kuwa waaminifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina hakika sana kama hiyo picha ni Tanzania kwa sababu zifuatazo.

1. Hayo mazingira yaliyopo hayo magari. (Inaonekana yako yard au indoor parking, kibongo ni ngumu).

2. Rangi ya hayo mabasi (Ni nadra sana kwa taasisi ya Umma hapa Tz kuwa na colour choice nyekundu).

3. Maandishi ya Kiingereza ubavuni mwa basi (Yaani washindwe hata kuandika hapa kazi tu! Wasiweke picha ya bendera ya Tz!)

4. Mantiki ya kuanzisha hiyo biashara (Haingii kabisa akilini)
Critical thinking....! Nakuunga mkono
 
yatasafirisha vifurushi mwezi tu...mwezi unaofata na mwendelezo yatabeba vifurushi Watu na mwisho yataanza kupaki stand ya ubungo moja moja na Mpk 2020 itakua rasmi serikali kuanza biashara ya usafirishaji Watu mikoani.
Lini utakua positive na nchi yako?
 
Leo karibu kila mtu anasifia hili swala la kuwepo kwa haya mabasi, ikitokea baada ya mwaka mabasi kama manne yawe hayapo barabarani kwa sababu ya ubovu au ajali, hawahawa waliosifia wataanza kuponda hii idea kuwa ilikuwa ni kutumia vibaya hela za serikali kununua mabasi.

Wabongo wenzangu tuwe wavumilivu pindi changamoto zikianza.
Kama yataharibika kabla ya muda uliotarajiwa lazima tuseme mkuu.
Iwapo kampuni A yenye mabasi aina hiyohiyo yanadumu kwa miaka 10kwanini hayo ya SU yaharibike ndani ya mwaka mmoja?
 
hii kitu ilikuepo though haikua mkoa kwa mkoa,nilikua naona post bus lilikua linatoka mtwara kwenda masasi kila siku kwa siku za jtatu mpaka ijumaa,abiria walikua wanalipenda sana.Sina hakika kama posta mtwara wanaendelea
Hata Dar-Iringa-Mbeya,yalikuwepo!
 
Thread ya 2019 sidhani hata kama yalianza kazi ...labda maharage aufufue mradi

Wakumbushe ilivyokua UDA.
Magari yalikua yananunuliwa mapya baada ya muda huyaoni barabarani, yanaagizwa mengine na hausikii mtu amewajibishwa.
 
Back
Top Bottom