MSONGA The Consultant
Member
- Feb 5, 2022
- 38
- 60
Utafutaji wa fedha kwa ajili ya Taasisi yaani "Fundraising Process" ni jambo muhimu sana kwa ustawi wa Taasisi. Kupitia "fundraising process" Taasisi itaweza kupata fedha kwa ajili ya; kutekeleza miradi, kugharamia shughuli za uendeshaji n.k. Jukumu la utafutaji wa fedha kwa Taasisi nyingi za Kitanzania limekuwa likifanywa na mwanzilishi/waanzilishi ambao mara nyingi hushika pia nafasi za juu ndani ya Taasisi. Utaratibu huu umekuwa ukizorotesha kwa kiasi kikubwa juhudi za utafutaji wa fedha kwa Taasisi.
Jukumu la utafutaji wa fedha kwa ajili ya Taasisi linapaswa kufanywa na watendaji mbalimbali wa Taasisi kwa lengo la kukusanya nguvu ya pamoja, watu hawa kitaalamu tunawaita "A Fundraising Team". Ni dhahiri kwamba Taasisi nyingi, pindi zinapoanzishwa zinakuwa na uhaba wa rasilimali watu (staffers), katika hali hii si vibaya kwa watendaji wachache waliopo kuvaa kofia mbili (kuwa na nafasi zaidi ya moja) ili kuhakikisha majukumu yanafanyika kama inavyopaswa.
Kimsingi, timu ya watu ambayo inapaswa kubeba jukumu la kutafuta fedha kwa ajili ya Taasisi yaani "fundraising team" inatakiwa kujumuisha wafuatao;
- Mkurugenzi Mtendaji (Executive Director) Majukumu ya ED katika mchakato wa utafutaji wa fedha, ni kuhakikisha anawatambua wadau wanaoweza kuisadia Taasisi (organization's supporters/constituents), kukutana na watendaji wa Taasisi zinazotoa fedha, kupitia maandiko ya miradi (grant proposals) yanayotarajiwa kutumwa kwa wafadhili mbalimbali, kuzungumza kwenye matukio ya harambee, kuiwakilisha Taasisi kwenye matukio mbalimbali n.k. Utekelezaji wa majukumu haya unategemea na ukubwa wa Taasisi, ikiwa Taasisi ni changa, basi ED atapata muda wa kutosha kutekeleza majukumu haya, na ikiwa Taasisi ni kubwa, Afisa Rasilimali yaani " Resource Acquisition/Development Officer" anaweza kuajiriwa ili kumsaidia ED baadhi ya majukumu.
- Resource Acquisition/Development Officer (DO). Jukumu la DO katika mchakato wa "fundraising" ni; kuandaa mpango mkakati wa utafutaji fedha (Fundraising Plan). Kutambua vyanzo vya fedha kwa ajii ya Taasisi, Kuhakikisha mchakato wa utafutaji wa fedha unafanyika kama ulivyopangwa na kuleta matokeo tarajiwa. Kuandaa michanganuo ya Miradi. Kufanya mazungumzo na wafadhili n.k.
- Bodi ya Wakurugenzi (Board of Directors) sheria inazitaka Asasi za kiraia kuwa na Bodi ya Wakurugenzi ambayo inaundwa na Mwenyekiti wa Taasisi, Katibu, Mweka hazina, na wajumbe wengine, ambao wakati mwingine wanaweza kutoka nje ya Taasisi. Jukumu kubwa la chombo hiki ni kuisimamia Taasisi na kuhakikisha inafanya shughuli zake kwa mujibu wa taratibu na sheria. Katika mchakato wa "fundraising" Wajumbe wa Bodi wanapaswa kuwa wachangiaji wa kwanza wa Taasisi kabla ya kuwafuata wadau wengine, jukumu lingine la wajumbe wa Bodi ni kuiunganisha Taasisi na wadau mbali mbali (constituents) wanaoweza kuichangia Taasisi, Kuwaandikia barua binafsi wadau mbali mbali (consitituents) kwa ajili ya uombaji wa fedha n.k. Ili kupata wajumbe wa bodi ambao wataweza kutekeleza majukumu haya kikamilifu, HAKIKISHA Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi yako inakuwa na watu wenye sifa na vigezo, na SI bora watu.
- Wafanyakazi wa Kulipwa (Other Paid Staff). Majukumu ya kundi hili yatategemea na muundo wa Taasisi yako, ila katika mchakato wa utafutaji wa fedha, kundi hili litakuwa na majukumu kama; kuingiza taarifa za wadau wa taasisi "constituents" kwenye "database", kuandaa barua za shukrani (Thank You Letters) n.k
- Wanaojitolea (Volunteers) Katika nyakati za mwanzo, Taasisi huanza na watu wa kujitolea kwa lengo la kupunguza gharama. Upatikanaji wa watu wa kujitolea si mgumu sana, unaweza kuwapata kutoka kwenye Taasisi za elimu (kwa wale wanaotafuta sehemu ya kupatia uzoefu), cha msingi hakikisha unakuwa na utaratibu mzuri wa kufanya nao kazi (A Good Volunteering Policy). Katika mchakato wa utafutaji wa fedha, kundi hili linaweza kufanya majukumu kama ya; kuandaa barua, na kuzipeleka kwa wadau mbalimbali, kukusanya "inputs" kwa ajii ya uandaaji wa michanganuo ya miradi, kufanya "grant researching" n.k.
OMAR MSONGA (BA. PPM &CD)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA