Shirikisho la Soka Afrika CAF yataja Klabu ya Simba SC nafasi ya 5 kwa utajiri Barani Afrika

Shirikisho la Soka Afrika CAF yataja Klabu ya Simba SC nafasi ya 5 kwa utajiri Barani Afrika

Status
Not open for further replies.
Kweli mkuu, ni wakuwaacha tu!
Usikubali kushikwa akili mkuu. Kwa unataja Azam, je kwenye Klabu yenyewe unajua bakharesa kaweka bei gani? Umetaja udhamini je NMB inashinda Sports Pesa? Je bajeti ya simba SC kwenye usajili sawa na Azam FC?
 
Kwa hiyo yanga anitwa chura sometimes kuzaliwa Tanzania raha ukiachana na ujinga wa wanasiasa
 
AC Milan na Inter Milan zina utajiri mkubwa lakini hazina viwanja, hivyo kiwanja si kigezo kikubwa cha kupimia utajiri wa klabu. Kuna timu zingine ukiodoa mapato ya viingilio vyanzo vingine vya mapato havijulikani, hivyo kwa nje unaweza kujua timu ni tajiri kumbe choka mbaya.
Haya mambo mbona yapo Liverpool na Everton walikuwa wakitumia kiwanja kimoja hapo zamani.
 
Hivi we unataka ujibiwe ki namna gani? Mbona una kichwa kigumu namna hiyo.

Haya umeng'ang'ana na Ofisi tu, hiyo hapo chini ni nini? View attachment 713144
yanga-akilimali.jpg
 
Yanga hawamo Top 15 hata, dah!
Hii kitu itawauma. Ndio maana mapato ya mechi za mwisho za kimataifa kuna gepu kubwa kati ya hizo timu mbili.
 
Awa caf wehu sana.team haina hata uwanja eti inaipiku utajiri zamaleki

Au wamehesabu utajiri wa Mo wakaufanya ndio wa mikia.
Wewe ndo mwehu sasa, kama Hujui vigezo vinavyotumika ni bora ukauliza.

Ni hivi, club is valued according to her value on the market by that time.
Sasa Simba SC ilijiongezea thamani kwa kuuza hisa za kwa 50% kwa mwekezaji zenye thamani ya bilioni 20 na ukumbuke hii 20bn ni dhamana ya uwekezaji.

Kumiliki uwanja sio kigezo cha timu kuwa tajiri...... Mfano United ni club tajiri zaidi duniani si kwa Sababu ya OT bali ni value of the brand on market lakini AC Milan na Inter hawana viwanja vyao binafsi lakini utajiri wao unapanda na kushuka kutokana soko kwa wakati husika.

Utajiri wa Mmiliki hautambuliwi kama ndo utajiri wa club, vinginevyo Man City na PSG vingekuwa Vilabu tajiri zaidi duniani.

Natumaini umenielewa, kama bado Basi hilo ni tatizo lingine inabidi daktari wa afya ya akili ahusike.
 
utazungumzia lile jengo la kibiashara pale msimbazi ;sindio!! unajua fadha yake inakwenda wapi? kama mtu kuwezi kufanya saving, huwezi kuwalipa wachezaji wako mpaka ulielie kwa wafadhili then utasema uana rasilimali?
Wao wanaangalia hiyo asset ipo sehemu gani, unaweza kuiuza kiasi gani au unaweza kukusanya pango kiasi gani.

Pili wanaeneo la kujenga uwanja mpya Bunju.

Uwekezaji wa MO ndio umewapa credit zaidi kama umezingatiwa ktk vigezo walivyotumia kukokotoa.
Kwa mfumo wa hisa Simba wanaweza kuingiza club yao soko la hisa wakatengeneza fedha zaidi.

NB: Uwekezaji wa MO hawajaipa Simba thamani kubwa sababu ya fedha binafsi za MO.

Yanga nasisi tubadilike tuingize club ktk mfumo wa kumiliki hisa na tununue eneo jingine la ujenzi wa kiwanja na huduma zingine za club tutakuwa juu zaidi ya Simba ukizingatia timu yetu ndio yenye shabiki wengi zaidi.
 
Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam imetajwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuwa klabu namba 5 kwa utajiri Barani Afrika.

Simba SC imetajwa kuwa na utajiri wa karibu Paund milioni 10.35 ambayo ni sawa na Bilioni 32.3 kwa shilingi ya Tanzania.

Katika orodha hiyo Al Ahly kutoka Misri inaongoza ikiwa na utajiri wa Paund milioni 19.25 ikifuatiwa na Esperance Sportive de Tunis 12.75M na Club Africain 11. 8M zote kutoka Tunisia.

Ya nne Kaizer Chiefs ya kutoka nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inatajiri karibu Paund milioni 10.48.

Klabu tajiri zaidi Barani Afrika View attachment 712984

Chanzo: MwanaspotiApp

Kawadanganye mbumbumbu wenzako huko! Kwenye hiyo Mwanaspoti App, mbumbumbu yeyote anaweza kuposti chochote.

Website ya CAF (CAF - Home) haina kitu kama hicho. Hata hivyo ukweli ni huu hapa:

Who is No.1? Here are the top ten RICHEST football clubs in Africa

Kwa kupitia orodha hiyo hapo juu, utagundua kuwa figures zote kuanzia Klabu ya 1 - 8 ni zile zile kama zilivyowasilishwa na mleta mada.

Tofauti pekee ni Klabu namba 5 ambapo mleta mada katuambia ni Simba wakati kiukweli ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Baada ya kubadilisha Klabu namba 5 akaendelea na ukweli kuanzia Klabu na 6 - 8, What a shame to mikia fc!

Huu ni upotoshaji mkubwa wa taarifa na kuifanya JF ikose heshima yake.

CC. Invisible - Kwa hatua za kinidhamu dhidi ya mleta mada.
 
w
Awa caf wehu sana.team haina hata uwanja eti inaipiku utajiri zamaleki

Au wamehesabu utajiri wa Mo wakaufanya ndio wa mikia.
amehesabu utajiri wa Mo...Huu ni uthibitisho tosha kuwa data nyingi za taaisisi hizi za kimataifa kama FIFA, CAF, World Bank na kadhalika huwa zina kasoro kubwa
 
Kawadanganye mbumbumbu wenzako huko! Kwenye hiyo Mwanaspoti App, mbumbumbu yeyote anaweza kuposti chochote.

Website ya CAF (CAF - Home) haina kitu kama hicho. Hata hivyo ukweli ni huu hapa:

Who is No.1? Here are the top ten RICHEST football clubs in Africa

Kwa kupitia orodha hiyo hapo juu, utagundua kuwa figures zote kuanzia Klabu ya 1 - 8 ni zile zile kama zilivyowasilishwa na mleta mada.

Tofauti pekee ni Klabu namba 5 ambapo mleta mada katuambia ni Simba wakati kiukweli ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Baada ya kubadilisha Klabu namba 5 akaendelea na ukweli kuanzia Klabu na 6 - 8, What a shame to mikia fc!

Huu ni upotoshaji mkubwa wa taarifa na kuifanya JF ikose heshima yake.

CC. Invisible - Kwa hatua za kinidhamu dhidi ya mleta mada.
Naona Vyura FC umepanik.. Kujiona mjanja kumbe mjinga tu, andamana basi hadi JF
 
Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam imetajwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuwa klabu namba 5 kwa utajiri Barani Afrika.

Simba SC imetajwa kuwa na utajiri wa karibu Paund milioni 10.35 ambayo ni sawa na Bilioni 32.3 kwa shilingi ya Tanzania.

Katika orodha hiyo Al Ahly kutoka Misri inaongoza ikiwa na utajiri wa Paund milioni 19.25 ikifuatiwa na Esperance Sportive de Tunis 12.75M na Club Africain 11. 8M zote kutoka Tunisia.

Ya nne Kaizer Chiefs ya kutoka nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inatajiri karibu Paund milioni 10.48.

Klabu tajiri zaidi Barani Afrika View attachment 712984

Chanzo: MwanaspotiApp
Wazee wa kufoji!

Baada ya kukubuhu katika kufoji mikataba ya wachezaji sasa wameanza kufoji data za Kimataifa:

1. Al Ahly (Egypt) – Market Value : € 19,25 m
2. Esperance Sportive de Tunis (Tunisia) – Market Value : € 12,75 m
3. Club Africain (Tunisia) – Market Value : € 11,80 m
4. Kaizer Chiefs (South Africa) – Market Value : € 10,48 m
5. Mamelodi Sundowns (South Africa) – Market Value : € 10.35 m
6. Zamalek SC (Egypt) – Market Value : € 10,30 m
7. USM Alger (Algeria) – Market Value : € 9.65 m
8. E.S Setif (Algeria) – Market Value : € 8.6 m
9. Raja Casablanca (Morocco) – Market Value : € 8.13 m
10. T.P MAZEMBE (DRC) – Market Value: € 7.70 m

Chanzo: Who is No.1? Here are the top ten RICHEST football clubs in Africa

Alichokifanya Ghazwat ni kuchomoa Klabu ya Mamelodi Sundowns (kwenye nyekundu, namba 5) na kupachika Simba SC. Hii haikubaliki, ni forgery mbaya sana yenye lengo la kupotosha ukweli. Hii ni Zaidi ya kufoji mikataba ya akina Singano na wenzake!
 
Naona wakina Manara washaona Ubingwa wa Bara hawaupati wameamua sasa kuja na hili ili kuwapumbaza Mambumbumbu wao ili wapate kitu cha kujisifia msimu huu.
 
Wazee wa kufoji!

Baada ya kukubuhu katika kufoji mikataba ya wachezaji sasa wameanza kufoji data za Kimataifa:

1. Al Ahly (Egypt) – Market Value : € 19,25 m
2. Esperance Sportive de Tunis (Tunisia) – Market Value : € 12,75 m
3. Club Africain (Tunisia) – Market Value : € 11,80 m
4. Kaizer Chiefs (South Africa) – Market Value : € 10,48 m
5. Mamelodi Sundowns (South Africa) – Market Value : € 10.35 m
6. Zamalek SC (Egypt) – Market Value : € 10,30 m
7. USM Alger (Algeria) – Market Value : € 9.65 m
8. E.S Setif (Algeria) – Market Value : € 8.6 m
9. Raja Casablanca (Morocco) – Market Value : € 8.13 m
10. T.P MAZEMBE (DRC) – Market Value: € 7.70 m

Chanzo: Who is No.1? Here are the top ten RICHEST football clubs in Africa

Alichokifanya Ghazwat ni kuchomoa Klabu ya Mamelodi Sundowns (kwenye nyekundu, namba 5) na kupachika Simba SC. Hii haikubaliki, ni forgery mbaya sana yenye lengo la kupotosha ukweli. Hii ni Zaidi ya kufoji mikataba ya akina Singano na wenzake!
Hii ni ya tar 16/07/2017 sio ya sasa hivi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom