Shirima wa Rombo jela miaka 30 kwa dawa za kulevya

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Mahakama ya wilaya ,wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro ,imemhukumu kwenda jela miaka 30 Festo Richard Shirima baada ya kupatikana na hatia katika shitaka la kupatikana na dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilogramu 17

Mshitakiwa huyo alikamatwa Mei 6, 2026,saa 11:50 jioni katika eneo la Kiboro, Kijiji cha Kelamfua, Kata ya Kelamfua Mokala, Tarafa ya Mkuu, Wilaya ya Rombo, akiwa na bunda 33 za majani ya mirungi zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa salfeti, pamoja na mabegi madogo mawili.

Baada ya kukamatwa, alifikishwa mahakamani Agosti 18, 2026, na shauri lake kusikilizwa hadi Oktoba 29, 2026.
Mshitakiwa huyo alikutwa na , hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela chini ya kifungu cha 16(1) na 2(c) cha sheria ya kudhibiti dawa za kulevya sura ya 95 kama ilivyofanyiwa iliyofanyiwa marejeo mwaka 2023.

Hukumu hiyo inaonesha hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi ya makosa yanayohusiana na dawa za kulevya.

IMG-20261029-WA0341.jpg
 
Ukiwakuta wanavyoyala kama mbuzi
Hayaui ushawahi sikia wapi mtu amekufa kwa kula hio Mirungi? Shida ni kwamba halipi kodi ndio serikali inaona ni biashara haramu sababu haipati kitu ndio maana inamfunga kwa sababu anafanya hio biashara

Mrungi una tofauti gani na kijogoo au kisungura kinachouzwa kwa mangi zote si zinalewesha tu tena hivyo vijogoo vinaweza vikawa na madhara zaidi kuzidi hio Mirungi kwanini wanaouza vijogoo hawafikishwi mahakamani? Sababu serikali inachukua kodi
 
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Mahakama ya wilaya ,wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro ,imemhukumu kwenda jela miaka 30 Festo Richard Shirima baada ya kupatikana na hatia katika shitaka la kupatikana na dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilogramu 17

Mshitakiwa huyo alikamatwa Mei 6, 2026,saa 11:50 jioni katika eneo la Kiboro, Kijiji cha Kelamfua, Kata ya Kelamfua Mokala, Tarafa ya Mkuu, Wilaya ya Rombo, akiwa na bunda 33 za majani ya mirungi zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa salfeti, pamoja na mabegi madogo mawili.

Baada ya kukamatwa, alifikishwa mahakamani Agosti 18, 2026, na shauri lake kusikilizwa hadi Oktoba 29, 2026.
Mshitakiwa huyo alikutwa na , hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela chini ya kifungu cha 16(1) na 2(c) cha sheria ya kudhibiti dawa za kulevya sura ya 95 kama ilivyofanyiwa iliyofanyiwa marejeo mwaka 2023.

Hukumu hiyo inaonesha hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi ya makosa yanayohusiana na dawa za kulevya.

View attachment 3701103
 
Attachments

  • 1790929942246.png
    1790929942246.png
    465.3 KB · Views: 4
  • 172519.jpg
    172519.jpg
    63.2 KB · Views: 4
  • 20260930_221723.jpg
    20260930_221723.jpg
    57.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom