SHIVJI: Serikali tatu ni kuvunja muungano

no research no right to speak, hauna hoja jombaa, shut ur domo-domo:yell:
 
Kwani ukivunjika kuna tatizo gani?
watanganyika wamechoka kuwabeba wazanzibari kwa upande mwengine Wazanzibari tumechoka kutawaliwa na watanganyika. sasa kama ukivunjika sio ndo kheri kwetu sote? wacha uvunjike wazannzibari tuaze maisha mapya kwa uhuru zaidi.
Shivij Profesa mnafiki aliyenanjama za kuendeleza ukololi wa kitanganyika kwa Wazanzibari.
 
unaweza ukawa nguli wa sheria lakini ukawa nguli wakukosa mipango.kama amependekeza mabunge matatu gharama ipo pale pale.kama anataka serikali mbili kwanini hakusema ni serikali za namna gani.je.ni mbili kama zilivyo,je,serikali ya zanzibar na tanganyika,serkali ya tanganyika na yamuungano ama serikali mbili za mfumo upi?kwa mfumo uliopo sasa wazanzibar hawataki na ndo wapinzani na ndo wanzilishi juu ya kujaribu kuondosha mfumo huu kwa kile wanachokiita zanzibar imenyimwa haki zake za msingi za muungano.na upande wa serikali moja wazanzibar waliowengi walahawatojaribu kuitupa nchi yao kwa kile wanachokiita kitendo cha kufanya serikali moja ni sawa na kuipoteza zanzibar katika ramani ya dunia kama ilivopotezwa neno tanganyika katika ramani ya dunia.katika hali halisi tokea muungano uasisiwe zanzibar inaonekana kudidimia kimaendeleo hali ya kua ni nchi ndani ya nchi wakati mikoa mingine ya jamhuri mbili zilizoungana zinaimarishwa na serikali za nchi mbili zilizoungana.katika hali hiyo iwapo serikali itakuwa ni moja tu hata hzo sekta chache za uchumi zilizopo zanzibar zitaendelea kufifia.serikali tatu ndio suluhisho la matatizo na kero za muungano.tume zote zilizoundwa hcho ndo walichopendekeza.ni serikali tatu ama uvunjwe kabisaaa
 

Yaani mimi nashangaa watu wameng'ang'ana na muungano,kama waasisi wake walikufa kuna shida gani
muungano kufa'
 
unaweza ukawa nguli wa sheria lakini ukawa nguli wakukosa mipango.kama amependekeza mabunge matatu gharama ipo pale pale.kama anataka serikali mbili kwanini hakusema ni serikali za namna gani.je.ni mbili kama zilivyo,je,serikali ya zanzibar na tanganyika,serkali ya tanganyika na yamuungano ama serikali mbili za mfumo upi?kwa mfumo uliopo sasa wazanzibar hawataki na ndo wapinzani na ndo wanzilishi juu ya kujaribu kuondosha mfumo huu kwa kile wanachokiita zanzibar imenyimwa haki zake za msingi za muungano.na upande wa serikali moja wazanzibar waliowengi walahawatojaribu kuitupa nchi yao kwa kile wanachokiita kitendo cha kufanya serikali moja ni sawa na kuipoteza zanzibar katika ramani ya dunia kama ilivopotezwa neno tanganyika katika ramani ya dunia.katika hali halisi tokea muungano uasisiwe zanzibar inaonekana kudidimia kimaendeleo hali ya kua ni nchi ndani ya nchi wakati mikoa mingine ya jamhuri mbili zilizoungana zinaimarishwa na serikali za nchi mbili zilizoungana.katika hali hiyo iwapo serikali itakuwa ni moja tu hata hzo sekta chache za uchumi zilizopo zanzibar zitaendelea kufifia.serikali tatu ndio suluhisho la matatizo na kero za muungano.tume zote zilizoundwa hcho ndo walichopendekeza.ni serikali tatu ama uvunjwe kabisaaa
 
Heshima zangu kwa prof kwa analysis ya kisomi, ingawa nayo ilikua na mapungufu kidogo, tunapenda kuona mijadala cnstructive kama hii, Nkuruma Hall imepata uhai wake tena, kuungana na prof, mtazamo wangu wakati tume ikiundwa ni kuwa , pamoja na kukusanya maoni ya watanzania, kama wasomi tuliowachagua watuwakilishe, tume ilikua na kazi ya kuyaweka hayo mapendekezo kitaalam katika mfumo ambao unatekelezeka, swala la kukusanya na kuyatoa jinsi yalivyo ni ukasuku na kutaka kujitua mzigo ambao hapo awali tuliwapa watusaidie, mpaka hapo tume imejiabisha kwa kuja na muundo usiotekelezeka
 
Tatizo huyu nguli wa sheria hajui kuwa kwa hali ya mambo ilivyo sasa mtu huwezi kuongelea maendeleo ya sekta nyingine nchini bila kwanza kutatua kero ya hili dubwana linaloitwa muungano. Bahati mbaya zaidi watu watanganyika na wa zanzibari sasa wanahusisha umaskini unaowakabili na hili dubwana la muungano.
 
Kwa Tension iliyopo sasa Serikali Moja ni ndoto ya Alinacha, sanasana ukiilazimisha utakuwa unakaribisha machafuko tu. Kama tunataka kuendelea kushirikiana na Wazanzibar basi suala la Serikali 3 haliepukiki kwa hili nipo pamoja na Jaji Warioba. Ingawa kama yangekuwa ni maamuzi yangu binafsi ningeuvunja tu huu muungano kwasasa mpaka labda huko mbeleni kama umuhimu wake utaonekana.
 
Shivji siungi mkono hoja yako?
Tueleze znz itajikwamuaje kwenye makucha ya watanganyika?
Huoni kuwa demokrasia unaikiuka?, madai ya wengi ni serikali tatu, wewe unasema laa, kwa faida ya nani?
My way serikali tatu, au kuwe na kipindi cha mpito cha kuvunja muungano ili, wa znz ambao wamekeza huku tanganyika. Wachukue vilivyokua vyao ili warudi znz.
 
Shivji pamoja na taaluma ya sheria aliyo nayo ana hofiu. Mtu mwenye hofu hawzi kfanya maamuzi yoyote ya kimaendeleo hata kama anaelimu kubwa. Suala la gharama sio tatizo kwa sababu hizi
1. serikali ya muungano haitakua serikali inayoshughulika ma mambo mengi ya nchi washirika wa muungano. Ni mabo saba tu yaliyoainishwa katk rasimu ya katiba mpya.
2. Wizara zitakua chini ya 15. Kwa rais atakayechaguliwa anaweza kuunda wizara kumi tu na sio zaidi ya hizo zenye wazi na naibu mmoja.
3. Bunge ni dogo kwa maana ya ukubwa wa majibo mfano dar itakua na. wabunge wawili tu na pia viti maalum vimeondolewa kwa serikali hii. Ni matumaini yangu kuwa na. serikali. za washiriki mabunge yao hayatakua na viti maalum kupunguza gharama. Ni matumaini yangu kuwa serikali za washiriki katiba zao zitaje idadi ya wizara ambazo serikali. hizo zinaruhusiwa kuunda.

jambo la pili na ambalo ni la msingi sana uwepo wa serikali tatu unahalalisha uwepo wa nchi zilizounda muungano huo. Na endapo Muungano utavunjika nchi washiriki zitaendelea kuwa na utawala wake. hivyo hakutakua na madhara makubwa ktika utekelezaji wa shughuli za kiserikali.

KIMSINGI
unaweza kujiuliza kulikua na ulazima wa muungano.?
kwa nini hizi nchi ziliungana?

Naweza kusema ni kwa ajili ya kujenga umoja na umoja huo ndio fahari ya Tanzania. Pamoja na kutokuwepo sababu za kujitosheleza za kuwa na muungano huu ni vema kuulinda.
Namshauri profesa aangalie upya mawazo yake juu ya muundo wa serikali. serikali tatu ndio suluhisho pekee.
 
kumbe ulimeliona hilo heeee! tunataka serikali ya Tanganyika ishike hatama tumechoshwa na propaganda za kisiasa hapa
 

Ndugu zangu mume mkoti vibaya shivji, shivji hajasema kabisa kwamba serikali 3 ni kuvunja muungano, amesema muungano ambao umeelezwa katika rasimu ya kwanza kama utakuwa hivyo hivyo basi utatengeneza migogoro zaidi baina ya washirika 2 Tanganyika na Zanzibar, akaelezea kwamba kuna mambo ambayo yamefanywa ya muungano kama uraia, haki za binadamu rasilimali na mipaka ya nchi za washirika wawili hayakupaswa kabisa kuingizwa katika muungano na kupendekeza kwamba haya yatolewe kwenye orodha ya muungano akafahamisha kila nchi ingekuwa na dola yake ata gharama ya hiyo serikali ya 3 zingepungua. hizo hizo serikali 3 kama zitaundwa kwa muundo alioupendekeza yeye basi hata nchi nyengine zinaweza kuja na kujiunga katika muungano huo, mana utakuwa unatowa haki sawa akafafanua kwamba hata ofisi za serikali ya shirikisho rasimu haikuziweka wazi jambo ambalo huenda likaweka migogoro kwa ufupi mm nimemfahamu kuna mambo yatolewe kwenye muungano ili kuepuka migogoro zaidi.
 

Prof. ni mwalimu wangu Lakini Hpo kachemka ama ana woga.
Muungano ni wa nani?
kwa maslahi ya nani?
nani aundeshe?
Kama si serikali Tatu then serikali Moja!! period!!! habari ya kudanganyana serikali mbili mzee Shivji umeisha, Iweje zanzibar ibaki na sovereignty yao na Tnganyika ife? Historia siku moja itatusuta. Na kama kama muungano wafa ufe halafu uzaliwe mzuri Muungano nao ujivue Gamba
 
Pungufu ya mamlaka kamili ya zanzibar wazenj hawa haja na dubwana muungano,zanzibr kwanza.
 

Chairman of the Mwalimu Nyerere Professorial Chair, Prof. Issa Shivi
The Chairman of the Mwalimu Nyerere Professorial Chair, Prof. Issa Shivi yesterday spoke against the proposed three-tier government earlier recommended in the newly launched draft constitution, arguing that the set-up would never resolve the existing union concerns.
Speaking at his last professorial chair debate titled, “the Silent Points in the New Constitutional Draft,” Prof. Shivji argued that recommendations on the three-tier government were purely political in nature and that it would lead to economic inequality.
Prof. Shivi commended that most terms in the draft constitution were a result of compromise rather than consensus, saying that formation of three governments would create more conflict in the two countries, leading to the break-up of the current union. He argued that union concerns could not be resolved by the number of governments but by democracy.
Prof. Shivji added that nobody would benefit, but all would suffer, from the break-up of the union — citing the example of Sudan where conflict followed immediately after the country split into two countries.
He noted that the people in Zanzibar had raised many complaints over the union, and that they had called for democratic ways of deciding their own affairs — not just the need for three government – hence the democratic factor in the current debate and not just the number of government which could ‘kill’ the union.
Instead of three governments now on the cards, Professor Shivji has proposed an alternative structure that could sustain the union – and proposes the formation of people’s as well national councils.
He noted that having three government would also mean having three presidents, and cautioned that trouble would begin if those three presidents come from different political parties.
He argued that in the process of forming three governments the mainland president would have a stronger voice because he would be ruling the bigger portion of the union.
Professor Shivji also wondered aloud why the police had been completely left out in all the seven issues of union – as is the case in the existing constitution.
On human rights, Prof. Shivji said the draft constitution had left out important issues such as the right to conduct demonstrations to demand their constitutional rights and justice at work.
The draft constitution which was unveiled this ye
ar by the Constitutional Review Commission (CRC) proposes, among many things, formation of three governments
 
Hayo ni mawazo ya shijvi, ni mawazo ya mtu mmoja yakipingana na mawazo ya wazanzibari na watanganyika walio wengi,wazeee wametufundisha wengi wape....kwahiyo Shivji mawazo yake hayana nguvu,huwezi kung'ang'aninia kitu ambacho kimeshindwa kufanya kazi kwa muda wa miaka 50, cha busara ni kuvunja mungano na kuunda chombo chengine chenye manufaa kwa wananchi
 
Yaani mimi nashangaa watu wameng'ang'ana na muungano,kama waasisi wake walikufa kuna shida gani
muungano kufa'

Kweli Mkuu,Mungano umeasisiwa na watu wawili Nyerere na karume bila ya kuwahusisha wananchiwa zanzibar na tanganyika,sasa kama wao wamekufa kwanini huu mungano nao usife,bibafsi naona huu mungano umeleta chuki baina ya watanganyika na wazanzibari,watu ambao walikuwa wanaishi kwa amani na starehe kabla ya mungano
 

Ni kweli karume na nyerere wamekufa lakini wameacha jini ccm,mpaka nalo life ndio tutapumua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…