SHIVJI: Serikali tatu ni kuvunja muungano

sisi wazanzibar tulishasema zamani hatuutaki muungano ila nyinyi wabongo ndio mnangangania sasa hatujui kitu gani mnachotaka kutoka zanzibar so mnaonaje mkaenda kaburi kwa babayenu laanatullaah nyerere mkamwomba akubali mpewe tanganyika yenu na sisi tubakie na zanzibar yetu.
 
Shivji anatakiwa aelewe hiyo ya mwenye nguvu anapata zaidi ni law of the nature, ukiangalia USA na Pueta Rico is the same kwamba mwenye nguvu ni usa, ukiangalia uhusiano wa USA na Europe utaona usa ndio wenye ku dictate zaidi , Hata Nguli Sengonda Mvungi aliwahi kuwauliza akina Jussaa na wenzake, watengeneze hiyo formula ya kuweka usawa katika ya watu million 40 na watu milllioni 2, proportionality yake ipoje? iwe kiuchumi , kimadaraka .
 
Na jambo moja la wazi lillilo na mapungufu katika Muungano huu ni uwiano wa wabunge, katika watu 10,000.00 Zanzibar kuna Mbunge , ukija bara unaweza kukuta wastani wa watu 100,000. hata katika nafasi za ubalozi nk, na hapo bado hatujaingia katika masuala ya contribution ya nchi hizi mbili katika kugharamia shughuli za Muungano. lakini bado kelele nyingi toka upande wa pili, mi nafikiri Zanzibar wangeomba muungano na Comoro, ndio wataelewana zaidi na proportionality yao ipo sawa.
 

Matola, kama Nyerere angependekeza serikali moja unadhani Karume angekubali? Mtu mwenyewe alishawishiwa saaaana na bado akasema Muungano ni kama koti likikubana unalivua. Unahitaji mtu mmajumuni wa Afrika kwelikweli kama Nkrumah au Ghadaffi kukubali kuunganisha nchi mbili kuwa moja na serikali moja. Afrika ilikuwa na viongozi zamani lakini sasa hivi hakuna kitu! ooh, where are great sons of Africa?
 

Huyu Mzee Unyerere unamsumbuwa. Anajitahidi kufanya kile alichoshindwa Nyerere juu ya Muungano. Unapokataa kuzungumzia Serikali una maana gani wakati nchi yoyote inaongozwa na Serikali? Tusizungumzie Serikali wakati ndiyo inayopanga hiyo mipango yote katika maisha ya nchi husika?
Malalamiko ya kila upande yanaletwa na mfumo wa serikali unaowaongoza katika utekelezaji wa shughuli zote. Mfumo wa Serikali wa zamani umeshindwa sasa tubaki nao? Kwanini tunataka tubadilishe katiba? Bila shaka umepitwa na wakati na imeshindwa kutuvusha hapa tulpo.
Mfumo wa Muungano nao umeshindwa kutuletea umoja tunaoutaka hivyo lazima tutafute mfumo mwengine. Professa anaposema kuwa labda ni kutatuliwa kwa matatizo ndio kupewe umuhimu, matatizo hayo yatatatuliwa vipi kwa mfumo ule ule ulioshindwa awali?
 
kama kuna mtu ana clip yake atuwekee tupime ana hoja, au na yy mwenzetu kaamua kututeka kielimu
Ni kawaida ya wasomi wetu tu kuwachia wenzao wafanye kazi na wao kuangalia mapungufu na kuyafanyia bezo.
 
Wazanzibar kamwe hawawezi kukubali serikali moja i can bet one billion dollars, solution ya kudumu ni kuuvunja huu Muungano wa Nyerere na Karume. fullstop

Hata Karume hakuwa tayari. Kauli za hawa Wanaotuzuga zinapingana kabisa na matendo halisi ya Karume. Karume hakuwahi hata siku moja kuchukulia nchi mbili hizi kuwa moja!
 
Huyu shijvi naye kapewa bichwa sana mpaka anapotea sasa, maoni yake juu ya muungano hayana uhalisia, ni wazi kwamba wazanzibar kwa sasa wanataka kuendesha baadhi ya mambo kwa kujitegemea, kwa maana nyingi kuwabana na serikali moja kwa misingi ya kulinda muungano huo ni udikiteta,
Pia shijvi anajaribu shawishi tukwepe democracy kwa kuogopa ghalama!!! hii ni ajabu mtu kama huyu kuna siku anaweza sema tusiwe na uchaguzi kwa kupunguza ghalama, ukweli ni kwamba kwa sasa maoni ya wananchi ndio kitu cha msingi, sioni sababu za kuendelea na serikali ya JMT na SMZ wakati Tanganyika haina serikali, matokeo yake inachanganya sana kujua ni yupi kiongozi wa Muungano na ni yupi wa Tanganyika,
Tukisema raisi wa JMT anasemami mambo ya Tanganyika pia huo ni upuuzi maana kura zake zinajumuisha watu wa zanzibar.
ni ngumu kwa sasa kuepuka Tanganyika maana kuna mambo ya msingi tunatakiwa kufanya, na zanzibar wafanya mambo yao, sio mbaya kama Muungano utavunjika kwa sababu tumeshindwa kaa meza moja, maana hakuna kitakacho haribika kwa muungano kuvunjika
 

Haijawahi kwa mkoloni kuachia koloni kwa hiyari yake. Hilo ndilo tatizo!
 

Shivji anazungumzia vikosi ikiwamo Polisi. Unajuwa Watanganyika watajifunza kwa wenzao Zanzibar. Zanzibar wana vikosi na bado vinafanyakazi kwa ushirikiano na polisi na jeshi la Muungano. Au hata Tanganyika mbona kuna mgambo JKT, magetreza vyote vina silaha lakini kila kiosi kina kazi yake na kinashirikiana na jeshi na Polisi za Muungano?
 
Serikali ina maana kila serikali itakuwa na jeshi kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa nchi

KWANZA TUSOME RASIMU ya katiba mpya kabla ya kutoa maoni yetu. Rasimu inasema kutakuwa na JESHI MOJA AMBALO LIPO SERIKALI YA MUUNGANO.

Rais wa Muungano ndiye mmiliki wa majeshi yote hivyo suala la mgongano halipo sana.
 

Umeongea vema... Pia alisema kwamba kuwa na serikali tatu maana yake ni kuwa serikali ya muungano itaendeshwa na michango ya nchi washirika.. Kwa kulinganisha uchumi wa Tanganyika na Zanzibar ni dhahiri kuwa mchango wa Tanganyika kwenye serikali ya Muungano utakuwa mkubwa zaidi kuliko wa Zanzibar; na kama zisemavyo methali za kiswahili, aliyemlipa mpiga zumari ndiye huchagua wimbo.

Muungano utakuwa kwenye hatari na hatimaye kuvunjika kabisa kwa kuwa serikali ya Muungano itampendelea zaidi mshirika mwenye mchango mkubwa.
 






Kumbe CDM kung'ang'ania serikali 3 ni kama tabula rassa
 

The ruling elites in Zanzibar are a stumbling block to the union.
 
Huu upuuzi Serikali tatu unakera. Ilipaswa tuzungumzie 1 au kubaki na .2. Shivji is right let's talk of maendeleo and stop this muungano nonsense!
 
Huyu mzee anazeeka vibaya kwanza sio mzawa atuachie Tanganyika yetu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…