SHIVJI: Serikali tatu ni kuvunja muungano

SHIVJI: Serikali tatu ni kuvunja muungano

Huu upuuzi Serikali tatu unakera. Ilipaswa tuzungumzie 1 au kubaki na .2. Shivji is right let's talk of maendeleo and stop this muungano nonsense!

tubaki na Mbili ??ipi na ipi? kwa nini inakuwa rahisi sana kusema kuwa serikali moja Zanzibar inamezwa na muungano lakini inakuwa vigumu kusema ndani ya mfumo wa sasa serikali ya Tanganyika ilimezwa kwenye muungano??Huu muungano ili usiendelee kuwa wa kulazimishana ipigwe kura ya maoni tuamue hatima ya muungano maana naona viongozi kwa sababu wanazozijua wao wanaulazimisha muungano lakini wenye nchi zao (wananchi) hawajaulizwa kama wanautaka muungano au la!!
 
Kumbe CDM kung'ang'ania serikali 3 ni kama tabula rassa

Nafikiri hujui maana ya tabula rasa otherwise kwa utumbo huu wewe mwenyewe ndio tabula rasa! Unataka kuaminisha umma kuwa maoni ya wananchi kutaka kuundwa serikali tatu yalikuwa ya chadema tu? Basi kama ndio hivo nchi nzima chadema pamoja na tume yote ya Warioba!!Maoni ya Shivji ni yake sio ya kila Mtanzania,..na sio kila siku akisema Shivji yupo sahihi, wengi wamedai serikali tatu ndio maana zikawekwa kwenye rasimu,.sasa huyu Shivji anataka kujiona yeye anafahamu zaidi na kuwa ana kura ya turufu ?? akapige kwao India sisi hapa serikali ya Tanganyika ni lazima iundwe !!!Otherwise serikali ya Mapinduzi Zanzibar ifutwe kuwe na moja tuu!!!
 
Kuifuta zanzbr sahau,labda mfufue tanganyika yenu na hiyo ni hiari yenu wenyewe watanganyika.
 
Walifanya kosa kukataa serikali tatu wakati nyalali alipopendekeza. Rasimu isipokiwa na serikali tatu itakataliwa na pande zote mbili. Wote tunajua kitakachofuata.
 
....Tanganyika Tanganyika,nakupenda kwa moto wote....
....nchi yangu Tanganyika,jina lako ni tamu sana....!!!!

Ninaisubiria kwa hamu siyo hiyo ambayo TANGANYIKA itakuwa taifa huru tena lenye mamlaka kamili!!
Mungu ibariki TANGANYIKA,mungu ibariki AFRIKA!!
 
Nguli wa sheria afrika Prof. Issa Shivji amesema kuunda serikali tatu hapa tz ni kuvunja muungano. Amesema si wakati muafaka sasa kulumbana kuhusu idadi ya serikali bali tulumbane kuhusu maendeleo ya nchi.

Amesema tunahitaji katiba mpya haraka lakini tuwe makini na baadhi ya mapendekezo yaliyopo kwenye rasimu ya katiba iliyotolewa hivi karibuni.

Source: taarifa za habari ktk vituo vya radio na television na magazeti mbalimbali hapa nchini pamoja mitandao ya kijamii

Pamoja na kuheshimu weledi wa prof.nataka nimwambie kwamba maendeleo yoyote katika jamii hayawezi kutenganishwa na mfumo wa dola.Manung'uniko dhidi ya serikali ni mengi kiasi kwamba yamezaa kitu kinaitwa KERO ZA MUUNGANO.Nadhani jambo la msingi angependekeza ni aina gani ya Muundo wa Muungano angetamani uwepo ili tudumishe Muungano.KWANGU MIMI SULUHISHO NI AIDHA SERIKALI 1 AU 3.MUUNDO ULIOPO NI MGUMU SANA FOR SUSTAINABLE URT.
 
WAKATI hoja ya serikali tatu iliyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba Mpya ikiwagawa Watanzania, mwanazuoni Profesa Issa Shivji, naye amepinga muundo huo kwa hoja kwamba ni mwanzo wa safari ya kuvunja Muungano. Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akitangaza azma ya kung’atuka katika nafasi yake ya uenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, alisema anaamini uwapo wa dola mbili ni njia pekee itakayoendeleza Muungano wa Tanzania.

Akiichambua kwa undani Rasimu ya Katiba Mpya, alisema Muungano hauhitaji idadi ya serikali tatu, bali ni uboreshaji wa mazingira ya demokrasia kwa wananchi.

“Kwa udhani wangu baada ya kuichambua rasimu hii, naona ndani ya Tume ya Katiba kulikuwa na mvutano mkubwa hivyo kutuzalishia rasimu ya maelezo na sio mapatano ya mwafaka.

“Siku zote maelezo ya makubaliano huzalisha jambo dhaifu na hili ndilo limezalishwa na Tume ya Jaji Warioba,” alisema Profesa Shivji.

Aidha, aliifananisha Rasimu ya Katiba Mpya na ganda lisilokuwa na tunda huku akiweka wazi upungufu kwa baadhi ya vipengele vilivyopo katika Rasimu hiyo.

Katika hatua ya muundo wa muungano wa serikali tatu, alielezea wasiwasi wake kuhusu mambo mbalimbali yatakayoleta utata na baadaye kuuvunja Muungano.

Alisema kutokana na baadhi ya vipengele nyeti kushindwa kuweka wazi lengo la kubana serikali washirika yakiwamo mambo ya ukomo wa mamlaka ya uhusiano wa Serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Akielezea kwa undani kipengele hicho, alisema kwa mfumo wa serikali tatu kama ulivyoainishwa ni lazima ionyeshe mipaka baina ya nchi washirika.

Alisema ikifika hatua ya kuwekeana mipaka baina ya nchi na nchi basi moja kwa moja kutazaa mgogoro mwingine mkubwa kwa nchi washirika ambao ni vigumu kusuruhishwa na Serikali ya Muungano.

“Sasa leo kuwapo serikali tatu, kama ilivyoainishwa katika rasimu ambapo Jamhuri ya Muungano itakuwa na umiliki wa mipaka yote ya nchi kavu, serikali washirika nikimaanisha Tanzania Bara na Zanzibar nao lazima wajiwekee mipaka, hapo kwa uzoefu wa mataifa yaliyowahi kuvunja serikali za mashirikisho suala la mipaka ni moja ya sababu zilizosambaratisha kwa hiyo hata katika mfumo huu tutegemee hili.

“Jamani athari ya kuvunjika kwa muungano ni kubwa zaidi kuliko mnavyofikiria, nadhani leo hii yanayotokea kati ya Sudani na Sudani Kusini mnayaona au jinsi Urusi ilivyogawanyika ambapo hadi leo kuna mapigano yasiyokuwa na ukomo,” alisema Profesa Shivji.

Kwa hisani ya Mtanzania.
 
kwani yeyè ni nan kila mtu afe na mzigo kazanzibar kadogo tu wabunge 75 bunge la jamhuri...kwa kweli nimeimic tanganyika..
 
Kukaa chini na kuanza kuelezea aina ya muungano ni kutaka kutouchimba mzizi wa tatizo halisia.

Kama anavyobainisha Prof. Shivji na kusema kuwa na serikali tatu ni chanzo cha kuvunjika kwa muungano. Kama matokeo yake ndiyo hayo, kuna kuwa na umuhimu gani wa kuingia gharama ya kuwa na serikali tatu wakati tunafahamu matokeo yake ni kaput.

Mzizi wa tatizo ni sauti ya wananchi kupitia kura ya MAONI (referendum) kujua kwanza kama watataka waendelee na muungano au waachane nao.

Kama wengi wataafiki kuwepo na muungano basi waseme wao wenyewe ni muungano gani wanataka uwepo ili kupata political Legitimacy and political justification kwa wanasiasa wetu kwa kile watakachokifanya baada ya kura ya maoni.

Ninachokiona hapa ni kuchelewesha muda wakati kinachokuja baadaye kinafahamika siyo kwa magwiji wa political science tu bali hata kwa watu wa kwenye vijiwe vya kahawa.

We just need REFERENDUM. Finito.
 
We need our TANGANYIKA back!blah blah nyingine katunzeni kwenye shelf zenu!!!
 
Huwezi kufanya kura ya maoni ktk nchi/Jamii ambayo hata ukiwauliza Wananchi wa TZ mmoja mmoja akuandikie neno MUUNGANO na kulisoma ni chini ya aslimia 30% wanaweza kufanya hivyo, achilia mbali kuelewa maana hata ya Muungano na kura ya maoni, sasa ya nini kupoteza fedha?
 
We need our TANGANYIKA back!blah blah nyingine katunzeni kwenye shelf zenu!!!

we need, wewe na nani? Jiongelee mwenyewe usitake kuwawekea Watz wote maneno Midomoni!
 
huyu jamaa ni walewale wa UDSM "matarumbeta ya kukodi"...watakuja kwa fujo na maelezo mengi yakipigiwa upatu ili waje iokoa CCM, na maslahi ya wazenj.
 
Huyu Nae ni mnafiki na hajulikani msimamo wake Yupo kupotosha watu mara hivi mara vile Yuko kutumikia Mabwana wawili
 
huyu si ndo alisema hukumu ya kesi ya lema imekosewa....watu wa kawaida tu wakampa shule au.....kwani jumuia ya ulaya wameungana hawajaungana...?
 
Katika hili hatuhitaji ushabiki wa kisiasa. Mimi nilikuwapo Nkrumah na hoja alizoziibua Shivji zinahitaji critical minds ili kufanya analysis ya kilichomo ndani ya rasimu. Kama unafocus miaka 50 and beyond, ni wazi kwa hoja madhubuti alizoziibua Shivji, hatutakuwa na kitu kinachoitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar!

Kwa maoni yake Shivji, kazi ya tume haikutakiwa iishie kuhesabu kwamba wangapi wanataka serikali moja, mbili au tatu. Tume kwa kuwa imesheheni watu waliobobea kwenye taaluma ilibidi mwisho ionyeshe UONGOZI. Aliainisha kuwa serikali ya uungano itaendeshwa kwa michango wa washirika, na kwa kulinganisha uchumi wa Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika itakuwa na mchango mkubwa zaidi na kama waswahili wasemavyo, aliyemlipa mpiga zimari ndiye huchagua wimbo.

Hatimaye Tanganyika itapendelewa zaidi, na zanzibar haitaridhika na upendeleo huo! Hatimaye muungano utavunjika. Katika hili, media hazijaripoti ipasavyo sawa sawa na hoja alizozitoa Shivji!
 
Huwezi kufanya kura ya maoni ktk nchi/Jamii ambayo hata ukiwauliza Wananchi wa TZ mmoja mmoja akuandikie neno MUUNGANO na kulisoma ni chini ya aslimia 30% wanaweza kufanya hivyo, achilia mbali kuelewa maana hata ya Muungano na kura ya maoni, sasa ya nini kupoteza fedha?
Mkuu, ninaona hoja yako unatengeneza kwa fikra tu ambazo hazibebwi na ukweli halisia.

Hii research ya Watanzania kuwa chini ya 30% wanaofahamu kusoma na kuandika sijui umeitoa wapi wakati research za kimataifa kama UNICEF na UNESCO zinagonga kwenye 70% na huwezi kuniambia kuwa nusu ya hawa hawajui kama kuna muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar.

Mimi nafikiri watanzania tumefikia katika level ya kujiamulia mambo yetu na mstakabali wa taifa kisiasa kama wananchi wote na ndiyo maana hata CCM wameliona hili na wakaamua kutoa maoni katika tume ya katiba kama wanaona ni lazima kuwepo na mgombea binafsi.
 
Back
Top Bottom