Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Skendo inayomuandama msanii maarufu wa miondoko ya HipHop wa nchini Marekani, Puff Daddy a.k. P Didy, inazidi kupamba moto baada ya CNN kupandisha mitandaoni video inayomuonesha akimpiga vibaya mpenzi wake wa zamani, Cassie Ventura.
Video hiyo ilinaswa kwenye moja ya hoteli waliyoenda kwa mapumziko mwaka 2016.
----------------
Kipande cha video kilichonaswa kupitia kamera za CCTV kimeweka hadharani kupitia Kituo cha CNN kikimuonesha nguli wa Muziki wa Hip Hop, Sean "Diddy" Combs akimshambulia aliyekuwa mpenzi wake, Casandra "Cassie" Ventura hotelini Machi 5, 2016.
Baada ya video hiyo kuwekwa mtandaoni, Cassie hajatoa tamko lolote lakini Mwanasheria wake amenukuliwa akisema “Hizo ni baadhi ya tabia za Combs" wakati Mwanasheria wa Diddy hajatoa jibu
CNN imeeleza video hiyo ilirekodiwa katika moja ya Hoteli ya Los Angeles, Marekani, Cassie anaonekana akitoka chumbani kuelekea kwenye lifti kisha Diddy akiwa na taulo pekee anamfuata na kuanza kumpiga, anamvuta kwa kumburuza huku akionekana kutoa maneno kama anamfokea.
Mwendelezo wa video unaonesha Diddy anampiga mwenza wake huyo akiwa chini kisha anakusanya mizigo aliyokuwa nayo Cassie na kuondoka nayo.
Ofisi ya Mwanasheria wa Los Angeles imeeleza “Ikiwa ni tukio la Mwaka 2016 hatutaweza kushtaki kwa kuwa ni shambulio lililotokea nje ya muda unaostahili kufunguliwa mashtaka."
Inadaiwa kuwa Diddy alinunua video hiyo ya hotelini kwa Dola 50,000 alipobaini amenaswa kwenye kamera kwa wakati huo.