Shonza: Siwezi kujibizana na Diamond

Shonza: Siwezi kujibizana na Diamond

nilitegemea kuona GT humu mkisema neno kumshauri Diamond kuwa super star hatakiwi kuweka video za uchi kiasi kile lakini nimeona wote mmepelekwa kimheko.
Jf member sasa ni bure kabisa.
 
Ukimsikiliza vizuri mond kuna baadhi ya vitu utavielewa,,,,kiuhalisia video ya nyimbo yake aliyomshirikisha rick ross ni uchafu haifai hata kutizama mbele ya wazaz
Kilichomkwaza zaidi huyu kijana si kufungiwa tu ila ni pald NW alipoenda mbali zaidi kusema wasanii mamuige ali ambaye ni hasim mkubwa wa diamond hapo amehisi kukosewa heshima
Wamefungiwa wasanii wengi lakini kwa nini diamond amekua akitoa kauli zisizo na uoga wowote? Ni ukweli ana back up ya big fish wanaompa kiburi na kumuona huyu mwanamama si lolote kwa kinachoendelea diamond yuko juu ya sheria.
 
Hio unayoiita 'hovyo' ndio tunayoikubali..
Wewe kama hupendi fyata mkia wako utulie
Tafuta sehemu nyingine tena nadhani nchi nyingine kusikilizia hiyo 'hovyo' yako. Serikali yetu pendwa kupitia mamlaka husika imeishatoa maelekezo juu ya nini cha kufanya kuhusu miziki ya 'hovyo'.
 
huyu shonza anatolewa hiko cheo anapewa ndumbaro hapo ndo atamjua bashite ni nani? ajue habishani na wcb anabishana na daddyyyyyyy
 
.
Screenshot_2018-03-20-23-54-24-2.jpg
 
Diamond angekaa kimya tu, hiyo nyimbo yake ya Haleluya imewasikitisha wakristo wengi sana, ni kwakua tu hawana utaratibu wa kulalama publicly ila umewakwaza watu wengi.
tuache ujinga jamani neno haleluya halimilikiwi na dini na maana yake ni sifa kwa mungu yaani kumtukuta kwa alichokifanya
kwani kuna ubaya gani kwa chibu kumtukuza mungu kwa kumuumba mwanamke mzuri jamani mbona tunakuwa na chuki za kijinga?
nna wasiwasi hao wendawazimu wanazifungia hizi nyimbo bila ya uhakiki wa wataalamu wa lugha
 
Kufuatia mwanamuziki wa bongo fleva kumlalamikia Naibu Waziri wa sanaa kuwa hawatendei haki wasanii kwa kuwafungia bila utaratibu, NW huyo ameibuka na kusema serikali haiwezi kujibishana na mtu aina ya Dimond na kwahiyo apuuzwe. Source mcl digital!
Kwa wote wawili, Diamond is of higher level as he has made life out of hard personal struggle and not like NW who has made fortune out of Usaliti kwa CDM.... and being awarded favour from "chakula cha wazee"
 
Ukiona Panya anamtania Paka, ujue shimo lake lipo jirani.

Sasa wengine wasiige anavyokunya huyo Tembo watapasuka.

Diamond ana backup, na huenda anaambiwa "mpashe huyo"
 
Fallacy Prediction!
Kazi yangu itakuwa ni kukukumbusha mpaka mwisho wa hili game.


WAZIRI MWAKYEMBE AKERWA NA KAULI ZA DIAMOND

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kumdharirisha naibu wake Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni.

Katika maelezo yake Mwakyembe amesema inaelekea sasa Diamond ameanza kulewa umaarufu sasa. Kuhusu hoja ya vikao anavyodai mwanamuziki huyo Mwakyembe amesema kuwa “kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, haijalishi nibmaarufu kiasi gani."

"Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake," amesema Mwakyembe.

Aidha Waziri Mwakuembe amemalizia kwa kumshauri mwanamuziki huyo kuwa "si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo."

Chanzo: DAR24
 
Ukiona Panya anamtania Paka, ujue shimo lake lipo jirani.

Sasa wengine wasiige anavyokunya huyo Tembo watapasuka.

Diamond ana backup, na huenda anaambiwa "mpashe huyo"
Diamond anaweza kuwa na Backup kuliko Manji?
 
Huyu dada mbona mswahili hivi? Hizi wizara zimevamiwa huyu toka aingie wasanii wanasutwa hadi wanalia machozi amekuwa kungwi nini?

Shida za manunuzi ya CCM wananunua hata matunda yalisiyoliwa. Yani huyu Juliana kwenye kundi la matunda basi ni ndulele [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom