Short course gani ilibadili maisha yako?

Short course gani ilibadili maisha yako?

Wakuu, habari za muda na wakati huu.

Katika harakati za maisha na kujitafuta unakuta umesoma Elimu nyingine ila mpenyo wako ulipata ulipo amua ku step up nakusoma kishort kozi kikakutoa jalalani.

Nilikua napenda nijui ni short kozi gani ziliwafungulia milango ili na sisi wengine tupate kuokota mawili matatu.
Nilikua mvuvi mwenye mafanikio kibiashara, mala viwanda vikafungwa fungwa, nikaibiwa nyavu pia na Machine zangu, nikaingia mjini nikazama kwenye magari, nikapiga course pale NIT, na nikawa Driver wa mashirika, japo kwa mbinde lakini mpaka leo hii nagonga Land Cruiser DFP toka 2009,na kazi hiyo ndo imenifanya kujenga, kununua usafiri tofauti tofauti, kulea familia yangu, full Michele na mikaa huko barabarani, watoto wanakua kwa uwezo wake Jaaliya

Maisha ni kuchagua na siyo muonekano kwa watu
 
Nilikua mvuvi mwenye mafanikio kibiashara, mala viwanda vikafungwa fungwa, nikaibiwa nyavu pia na Machine zangu, nikaingia mjini nikazama kwenye magari, nikapiga course pale NIT, na nikawa Driver wa mashirika, japo kwa mbinde lakini mpaka leo hii nagonga Land Cruiser DFP toka 2009,na kazi hiyo ndo imeniganya kujenga, kununua usafiri tofauti tofauti, kulea familia yangu, full Michele na mikaa huko barabarani, watoto wanakua kwa uwezo wake Jaaliya

Maisha ni kuchagua na siyo muonekano kwa watu
Asante mkuu kila hatua dua
 
Ufundi gypsum na ceiling in general, hii nilijifunza site moja kwa moja nilipoanza kibarua baada ya life kunichapa juu kati na chini, nikaingia site nikakutana na hizi mbishe wana wanapiga nikajiunga sijawahi kujutia na hakuna kurudi nyuma, natamani hata ningemaliza tu 4 ningekuja pande hizi
 
Back
Top Bottom