kwanza wawashe umeme nchi nzima na waweke kila mahali maji ya bomba ndio baadae waanze kujenga hayo mavyuo ya soka.Tanzania inapoteza hela bure kutafuta makocha wa kigeni..fedha hizo zingetumika katika program nyingine za kukuza vipaji,kujenga vyuo vya soka,kuwafundisha wataalamu wetu wa kizalendo,ambao ndo wanajuwa mahitaji ya soka yetu na wanawajuwa vijana wetu,na wanaeleweka vizuri..tukakuza vijana tokea Juvenile...junior...central mpaka seniors...tukiwa na makocha hao hao akina Mashi na Mkwasa. Si tumeona Kombe la dunia la vijana U-17,Nigeria, watoto wa Kiswiss wanakanyaga gozi la ng'ombe kama watu wazima,wanasema watoto wale wamehamishwa makwao na wengi wapo katika vyuo vya soka wakikuzwa vipaji vyao...na U-swiss wanatarajia kuwa na timu tishio ya taifa kutoka na vijana wale muda si mrefu(wale wtoto si masikhara wanaujuwa hasa)..kwanini tusiwekeze kwenye program kama hizo...kama tumeweza kujenga uwanja kwanini tusijenge chuo cha michezo kukuza vipaji...wachezaji tulionao Stars wanacheza kama wamejifunza mpira ukubwani vile...hawana skills...hawafundishiki..ni aibu kusema timu ya taifa inafundishwa na kocha wa kigeni.
Junius ukiacha masuala ya Zanzibara na ud... unaongea pointi kwelikweli. Mafanikio yeyote yanaletwa na kuanzia chini kabisa.Tanzania inapoteza hela bure kutafuta makocha wa kigeni..fedha hizo zingetumika katika program nyingine za kukuza vipaji,kujenga vyuo vya soka,kuwafundisha wataalamu wetu wa kizalendo,ambao ndo wanajuwa mahitaji ya soka yetu na wanawajuwa vijana wetu,na wanaeleweka vizuri..tukakuza vijana tokea Juvenile...junior...central mpaka seniors...tukiwa na makocha hao hao akina Mashi na Mkwasa. Si tumeona Kombe la dunia la vijana U-17,Nigeria, watoto wa Kiswiss wanakanyaga gozi la ng'ombe kama watu wazima,wanasema watoto wale wamehamishwa makwao na wengi wapo katika vyuo vya soka wakikuzwa vipaji vyao...na U-swiss wanatarajia kuwa na timu tishio ya taifa kutoka na vijana wale muda si mrefu(wale wtoto si masikhara wanaujuwa hasa)..kwanini tusiwekeze kwenye program kama hizo...kama tumeweza kujenga uwanja kwanini tusijenge chuo cha michezo kukuza vipaji...wachezaji tulionao Stars wanacheza kama wamejifunza mpira ukubwani vile...hawana skills...hawafundishiki..ni aibu kusema timu ya taifa inafundishwa na kocha wa kigeni.
Point tupumaximo katumia cv ya nchi yake kupata kazi tanzania na sisi tulivyo wavivu wakumchambua mtu kabla hatujamuajili ndio maana tumeangukia kwake.
Una hoja hapa mheshimiwa yaani umejenga hoja kwa mfano. Tena kuna mbabaishaji mmoja anapinga hilo.huyo Maximo anatugeuza sisi kuwa kichwa ya mwendazimu..hana jipya wala nini...kashatuchukua sehumu ambayo uwezo wake inamruhusu...hana first 11 mpaka leo anakula mshahara ya bure tuu..TFF nayo wajinga wanamuogopa....maximo atuachie timu yetu...Mpeni Timu Patrick Phiri tutaona mwanga and timu itakuwa tishio...angalia simba alivyogeuza mwaka jana and mwaka huu ni moto ya kuotea...go away maximo and leave our team to the ones who love it with their hearts....
sasa unataka uchukue wachezaji wa Toto Africans waliokataliwa na timu zote?Nakuunga mkono mkuuuulu
Mpira some times ni vichwa vya wachezaji tu kama kaujuzi ni mafundisho madogo sana kwa wachezaji wetu vinginevyo tuko poa tu na hiyo TFF nayo ifanyiwe reshuffle jamani wachezaji inao wachukuwa 100% ni simba na yanga au kwa kiswahili kingine ni wachezaji wa kutoka Dar tu,
Sijui tufanyenini hapo sasa. na tatizo sio kocha
Kwangu mimi sioni tatizo la Maximo. Bali naliona tatizo letu sisi kama watanzania, ambao kikweli hupenda kuvuna bila ya kupanda. Timu ya taifa ya taifa lolote sio mahali pa kukuza vipaji kama tunavyomtaraji Maximo afanye. Timu ya taifa iliyojengwa kwa misingi imara kutoka kwenye football academy ambako mtu akichaguliwa timu ya taifa kutokana na nidhamu ya kitaaluma aliyonayo ataona fahari na sio kufanya ubishoo kama wanavyofanya masupastaa wa bongo. Nakubaliana na msimamo wa Maximo ya kusisitiza nidhamu japokuwa sio kazi yake persee anajikuta analazimika kulifanya hilo kwa sababu halipo. Kiwango cha mchezaji wa team ya taifa hafundishiwi nidhamu katika timu ya taifa bali ni kwenye ngazi za chini alikotoka na mwisho kabisa ngazi ya vilabu.
Mziray ni lazima aseme kwa sababu mafanikio yoyote ya Maximo kwake kama kocha wa kitanzania ni mwiba. Mzirai sio mgana ni mtanzania tumekuwa naye hapa miaka dahari, amefundisha yanga ule mpira wa kesho mechi tukalale makaburini, mkienda Misri makaburi atawaonyesha nani?
Soka yetu kama walivyochangia wachangiaji wengine hapo juu inahitaji zaidi ya kocha mzuri. Tunahitaji maandalizi tuwe na vitalu kama mpango wa taifa wa namna ya kukuza vipaji na ajira, pili vilabu ama viwezeshwe au vione haja ya kuwa na yanga academy, simba academy, mtibwa nk.
Bila hivyo hata tukisubiri kocha bora ambaye timu ya taifa anayoiongoza ikimaliza kazi ya kuchukua kombe la dunia SA mwaka 2010 halafu tumchukue sisi tutaja mtusi hivihivi tunavyofanya kwa Maximo kwani hatuna maandalizi badala yake tunajiandaa kushangilia bila kuwa na mkakati wa ushindi.
Ili tuwe fair kama wananchi na wanamichezo, tumpongeze Maximo kwa hatua aliyotufikisha kwani hatukuwa hapa tulipo. Tujiulize kwanini hatutoki hapa tulipo mimi nina hakika kwamba tatizo letu ni kukosa mkakati wa maana kama taifa wa ushindi. Mambo mema hayataki haraka ati.
Mzirai toka maximo aingie hoja ni hiyo tu kumpinga basiMziray ni mnafiki mkubwa! hatumuhitaji kwenye timu yetu ya taifa hata kama Maximo ataondoka leo. Hana la maana zaidi ya kuchonga saaaaana.
he!, umesusa?sichangiiiiii
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kocha wa timu ya taifa, Marcio Maximo, ataendelea kuwa mwalimu wa Taifa Stars mpaka mkataba wake utakapomalizika na serikali imewataka 'wanaopiga kelele' kutaka afukuzwe, wamuache afanye kazi yake kwani gharama za kuuvunja mkataba wake ni kubwa mno.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kauli hiyo ya serikali ya kumtetea Maximo imekuja kufuatia shutuma mpya za mashabiki na wadau wengine wa soka kutaka kocha huyo Mbrazili ampishe mwalimu mwingine kwa madai kwamba uwezo wake 'umegota'. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza na Nipashe jana, Msemaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Jacob Tesha, alisema kuwa hakuna sababu ya wadau kumponda Maximo wakati amejitahidi kwa kiasi kikubwa kufanya mapinduzi kwenye soka la Tanzania.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tesha alisema kuwa ni jambo la busara kama wadau hao kumpa nafasi Maximo kutekeleza mikakati aliyojiwekea kabla ya kumaliza mkataba wake mwakani.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Jamani hebu tumuunge mkono Maximo, tunataka atufanyie nini? Amelikuta soka letu likiwa sehemu isiyo nzuri na ametufikisha hapa, tumpe nafasi ili akamilishe programu zake kabla ya kumaliza mkataba wake," alisema Tesha.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliongeza kuwa gharama za kuuvunja mkataba na kocha huyo kwa vigezo vya kutoridhishwa na uwezo wake ni kubwa kuliko inavyofikiriwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo Tesha alieleza kuwa si vibaya kwa wadau wa soka kutoa maoni yao lakini wanapaswa pia kuyangalia na mazuri aliyoyafanya kocha huyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shutuma mpya dhidi ya Maximo zimekuja kufuatia matokeo mabaya katika mechi tatu za kirafiki za kimataifa zilizofanyika nchini Yemen hivi karibuni ambapo Stars ilifungwa mechi mbili na kutoa sare moja.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika mechi ya kwanza dhidi ya mabingwa wa Afrika Misri, Stars ilizidiwa kila kitu na kulala kwa magoli 5-1, kabla kulazimisha sare 1-1 katika mechi ya pili dhidi ya Yemen. Katika mechi ya marudiano na Yemen Stars ililala 2-1, na kuamsha hasira za Watanzania.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Miongoni mwa shutuma zinazomkabili Maximo ni kuwaita kwenye kikosi cha taifa makipa ambao hukaa benchi kwenye timu zao na pia kuwaacha nyota wengine -- jambo ambalo mwenyewe ameshalitolea ufafanuzi mara kwa mara kwamba ni ukosefu wa nidhamu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati huo, Maximo amepata sapoti kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama cha makocha nchini (TAFCA) Eugean Mwasamaki ambaye amesema kuwa makocha nchini wanatakiwa kujifunza kutoka kwa Maximo juu ya msimamo wake wa kutosikiliza maneno ya nje.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kocha anatakiwa kuwa na misimamo yake hasa kwenye suala la ufundi, makocha hawatakiwi kusikiliza maneno kutoka nje kama wanataka mafanikio, wafanye kazi kwa misingi ya kazi na taratibu waliyojiwekea wao na si kusikiliza kele za mashabiki, alisema Mwasamaki.[/FONT]
pia amesema wanamsubiri Tenga ktk uchaguzi awaeleze taifa Star chini ya Maximo imefanya nini huku ikiwaacha wachezaji ambao kimsingi TFF wanatakiwa wakae nao na wasikilize matatizo yao.
hawana nidhamu lakini hatuambiwi kivipi, kwa sababu haohao wanaoonekana hawana nidhamu taifa stars vilabuni mwao wanapiga fresh tu pamoja na kwamba wanafundishwa na makocha wakigeni pia.