Pamoja na hasira tulizonazo za kuishuhudia timu yetu ikifungwa hatuna budi pia kutoa sifa kwa kocha timu inaposhinda. MAXIMO huyu aliipeleka Tanzania kwenye CHAN, pia aliiwezesha timu kuwa walau inapata matoeo ya kuridhisha against timu za west Africa e.g Ushindi dhidi ya Burkina Fasso, Draw against Cameroon, Ghana, Senegal.
Nafikiri tatizo letu sio MAximo, bali ni mfumo wa soka letu kwa ujumla. Tujiulize maximo anapata wapi wachezaji? Mostly ni Simba na Yanga; zitazame hizi timu kwa miaka mitatu nyuma niambie zimeshinda mashindano gani ya kimataifa au kuifunga timu gani bora hapa Afrika Mashariki na Kati?Kwa miaka miwili mfululizo ligi kuu Bara, mfungaji bora amekuwa ni mchezaji kutoka nje ya Tanzania (hatuna wachezaji wenye uwezo wa kufunga magoli??). Na sio kweli kuwa timu ya maximo inabadilika wachezaji wa timu ya Taifa stars ni wale wale , First eleven imepungukiwa na hawa wafuatao tu Kaseja(alionyesha upuuzi mwenyewe, hastahili mshamaha; huwezi kushangilia timu yako mwenyewe ikifungwa), Ivo Mapunda (kiwango kimepungua), Meck Maxime(kastaafu, kabadilishwa na Juma Jabu), Mwaikimba na Said Maulid (uwezo duni/Umri), Victor Costa(majeraha) na Deo Njohole (kiwango duni) Chuji, nidhamu mbovu(bangi). Hawa ndio walioondolewa ktk first eleven ya maximo na kuanza kuongeza chipukizi wafuatao, Juma Dihile, Jerry tegete, Mrisho Ngassa, Kiggi Makasi, Juma Jabu, nk Chipukizi hawa hatuwezi kubisha kuwa ni kati ya wachezaji bora kabisa waliopo katika ligi kuu ya Bara kwa sasa.
Bottomline is; tatizo liko kwetu tuliondoe, watakuja makocha wote bora tunaowajua hatutafika. Mliotazama michezo ya challenge; be honest na tuache ushabiki; magoli alitokosa MGOSI alaumiwe maximo?red cards za Kijinga hata kwenye mechi ya nusu fainali alaumiwe maximo?
I am just thinking aloud!