Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

The B,
Hisani ya kuja kufundisha soka katika nchi yenye kiwango kibovu cha soka kwa malipo karibu na bure kwa kocha anaetoka taifa lenye hadhi na heshima kubwa ya soka
Anaweza kuwa anatoka katika nchi ya aina hiyo. Je anamafanikio gani huko nyuma kabla ya kuifundisha Stars. Maximo amefanya kazi kwa muda wa kutosha sasa tena huku akipewa misaada lukuki kuliko makocha woote huenda kwenye historia ya nchi yetu. Lakini output hakuna. Ni vyema akakaa pembeni.
 
the b,
hisani ya kuja kufundisha soka katika nchi yenye kiwango kibovu cha soka kwa malipo karibu na bure kwa kocha anaetoka taifa lenye hadhi na heshima kubwa ya soka

hisani angefundisha bure...
Hakuna hisani...ni ama afanikiwe au ashindwe afukuzwe..
Anafukuzwa morinho itakuwa maximo????????
 
hisani angefundisha bure...
Hakuna hisani...ni ama afanikiwe au ashindwe afukuzwe..
Anafukuzwa morinho itakuwa maximo????????
Yaani unaongea nukta tupu, bro! Pia umemsahau Golan Erickson na Big Phil (Scolar)!
 
Nasikitika wewe ni msahaulifu kidogo. Kama ni habari ya professionals tulishakuwa nao: Km Njohole na wengineo. Maximo alichofanikiwa sana ni kuwafanya wachezaji kutalii nchi nyingi zaidi na kuwa na maisha nafuu. Lakini tuje uwanjani: Tulishakuwa na mafanikio makubwa zaidi kwa makocha wa kizawa tena kwa maandalizi hafifu ambayo huwezi kufananisha na maandalizi ya Maximo ambayo wachezaji sasa wanafahamu mandhari ya Kempiski na Hoteli nyinginezo za kifahari, yakoje! Pia udhamini unaofanywa sasa hivi kwa Taifa Staaz ni ya kufa mtu lakini matunda kidogo! Kwa mtaji huu mafanikio ni ya kimaandalizi na sio uwezo wa mwalimu uwanjani! Huo uwezo mdogo wa wachezaji ni matunda ya mwalimu mbovu!
Twende mbele turudu nyuma hivi bongo kuna wachezaji gani hasa mpaka mwamlaumu Maximo???hata akija Fergie au Wenger hatuwezi kwenda popote, wachezaji wenyewe lishe duni halafu wengi wao urefu kama wright Phillips hawawezi mikiki mikiki ya kina Drogba banaaaa.
 
Mpira wa Tanzania ata akija Hidink hautakua, hata akija kocha bora duniani hauta kuwa. Mpaka tuimarishe program zetu za lgi na pia mfumo wa vilabu vyetu. wachezaji wakuzwe toka wakiwa watoto na si kutaka eti ghafla mchezaji awe kama Ronaldo, wakati ajalelewa toka akiwa mtoto kisoka.
 
The B,
Mbona alishamaliza mkataba wake mkamramba nyayo aongeze mlikuwa mnafikiria nini?
 
hisani angefundisha bure...
Hakuna hisani...ni ama afanikiwe au ashindwe afukuzwe..
Anafukuzwa morinho itakuwa maximo????????
Boss
hii haijakaa vizuri kaka
Mpira wa Tanzania ni program, maximo mtambebesha dhambi zote lakini bila kuweka program sawasawa kuanzia football administration sehem zote mpaka kwenye vilabu, na program sahihi, hatutafika mbali kamwe mkuu. Hata akija kocha gani sijui, watakua wanakuja wanaondoka. Ulitaka Musa Mgosi apige mpira kama e'too?. E'too kaanza kulelewa toka akiwa mdogo ndo maana kawa vile kaka.
 
Mpira wa Tanzania ata akija Hidink hautakua, hata akija kocha bora duniani hauta kuwa.
Sasa kama hatuwezi kwenda popote hata akija kocha yeyote basi hakuna haja ya kuwa na Maximo, maana anaendelea kula fedha zetu kupitia kwa Mkulu bure! Naamini hata TFF wamemchoka lakini hawana ubavu wa kumpiga stop!
 
Tatizo ni sifa za jk.....
Tff walikuwa na mipango yao na kocha wao
kutoka ufaransa...
Kikwete akamleta maximo bila kushauriana na yeyote..
Sasa tff hawawezi mfukuza,,
wanaogopa kumuudhi jk.
 
The B,
Mbona alishamaliza mkataba wake mkamramba nyayo aongeze mlikuwa mnafikiria nini?

Uamuzi wa kumwongezea mkataba ni wa mtu mmoja tu, Mkulu, kungekuwa na jaribio la kuuliza maoni ya wananchi angetimuliwa siku nyiiiiingi!
 
Sasa kama hatuwezi kwenda popote hata akija kocha yeyote basi hakuna haja ya kuwa na Maximo, maana anaendelea kula fedha zetu kupitia kwa Mkulu bure! Naamini hata TFF wamemchoka lakini hawana ubavu wa kumpiga stop!
Soma content yote niliio ielezea. Nilisema hauwezi kukua kutokana na mfumo mzima wa mpira Tanzania kuanzia TFF, vilabu na ligi nzima. nikasema hapo juu akina Kaka na Messi hawakuja hivihivi hatuwezi tukawaweka akina chuji wakawa kama akina Shnaida.
Angalia akina Nando torres wametokea wapi, akina Rooney akina Messi yaani list haita isha.
Mpira ni program, tuanze kurekebisha kwanza program zetu.
 
The B,
Mbona alishamaliza mkataba wake mkamramba nyayo aongeze mlikuwa mnafikiria nini?
Ukweli wengi tunang'atang'ata maneno. Lakini ukweli ni kuwa Maximo ameshindwa kazi hata TFF wanaweza kukiri hivyo pembeni. Ila nani mwenye uwezo wa kumvisha paka kengele? Maana ameletwa na mwenye nchi. Mpaka order itoke Ikulu. Walifanya kosa kubwa sana kutokumuondoa baada ya mkataba kuisha. Sasa hivi labda mwenyewe ajiondoe na huenda hayo yatafuata baada ya kombe la Challenge. Au iwe kwa mutual konseti
 
Twende mbele turudu nyuma hivi bongo kuna wachezaji gani hasa mpaka mwamlaumu Maximo???hata akija Fergie au Wenger hatuwezi kwenda popote, wachezaji wenyewe lishe duni halafu wengi wao urefu kama wright Phillips hawawezi mikiki mikiki ya kina Drogba banaaaa.
Hapa umeongea kitu, siyo unamlaumu Mwalimu darasani kwa kufeli mwanao kwanza unatakiwa ujuwe kama je mwanao anafahamu, anadurusu masomo akeshasomeshwa na mwalimu..ana nidhamu,hapa nashangaa kuna mtu ananitajia Kaseja, mtu hana adabu hata za kuvalia nguo wa nini timu ya taifa, wenzake wanafanya kazi uwanjani wanafungwa yy anadhihaki anacheka...ndo mchezaji gani huyo...tanzania haina timu za maana za vijana kusaidia senior timu au hata hao walimu wanaofundisha timu za daraja la kwnza wengi wao wanafundisha kwa uzoefu tu halafu wachezaji hao hao apewe Maximo aanze kuwafundisha kupiga danadana, pasi, kumiliki mpira,kuzingatia, kubadilisha mchezo wakati wa kuzidiwa,uwezo wa kimwili..na mambo tele ambayo timu yake hayapati au hafundishwi anakuja yakuta timu ya taifa inakuwa kama mapya vile kwake...uje umlaumu Maximo baadae kwa uoza wa wachezaji wenyewe unamtendea haki???
 
Tatizo ni sifa za jk.....
Tff walikuwa na mipango yao na kocha wao
kutoka ufaransa...
Kikwete akamleta maximo bila kushauriana na yeyote..
Sasa tff hawawezi mfukuza,,
wanaogopa kumuudhi jk.
huyo kocha kutoka ufaransa unadhani angekuza mpira kwa staili ya mfumo wa mpira tanzania?
 
huyo kocha kutoka ufaransa unadhani angekuza mpira kwa staili ya mfumo wa mpira tanzania?

vyovyote vile
lakini tungekuwa na uhuru wa kumfukuza
kama angeshindwa..
Sasa huyu maximo tunashindwa kumfukuza
kwa sababu ya jk.
 
vyovyote vile
lakini tungekuwa na uhuru wa kumfukuza
kama angeshindwa..
Sasa huyu maximo tunashindwa kumfukuza
kwa sababu ya jk.
Wangemleta TFF lakini mambo yangekua yaleyale ya Lunyamila simtaki awe kwenye tim, Maximo ana weakness zake kama kocha yoyote duniani, ila ntaomba ukubaliane na mimi kwanza mfumo wa mpira wa tanzania unachangia asilimia 80 ya kiwango duni Tanzania. hata umlete nani, kwa mpango mzima mp[ira Tanzania hamna.ndo maana mekupa mfano wa akina E'too, au utaona wale watoto wa Ghana watakavyo shine baadae au wa switzerland.
 
Soma content yote niliio ielezea. Nilisema hauwezi kukua kutokana na mfumo mzima wa mpira Tanzania kuanzia TFF, vilabu na ligi nzima. nikasema hapo juu akina Kaka na Messi hawakuja hivihivi hatuwezi tukawaweka akina chuji wakawa kama akina Shnaida.
Angalia akina Nando torres wametokea wapi, akina Rooney akina Messi yaani list haita isha.
Mpira ni program, tuanze kurekebisha kwanza program zetu.
Nimekusoma mkuu, Maximo ni wa nini kwa sasa kwenye timu ya Taifa kama mpira ni program?
 
Nimekusoma mkuu, Maximo ni wa nini kwa sasa kwenye timu ya Taifa kama mpira ni program?
Maximo yupo kubadilisha attitudes za mpira wa Tanzania, Mfano nidham imeshaanza kuoneakana ni kitu muhim katika mpira wa Tanzania wakati zamani haikua culture yetu. Sasa unaona hata club zinawafukuza na kuwapa adhabu wachezaji ambao ni watovu wa nidham. Muache awepo ana experience ya nje ambayo ata import kwetu.
 
Acheni ukurumbizi huwo, kwanini msilaumu uwezo mdogo wa wachezaji wenu ambao hawafundishiki, vifuu tundu, hawafahamu. Kwanini mnakuwa watovu wa shukurani, ni wakati wa Maximo angalau Tanzania imeona 'profeshino' wawili wa tatu. Na halafu, si Maximo mwenyewe alipomaliza mkataba wake alitaka kuondoka kwanini muanze kupiga mbiu kama vile yeye anang'ang'ania, kwa lipi? Si TFF wenyewe waliomlazimisha abakie...mbona mnakuwa watovu wa hisani jamani!!!!!!!!!

Kwa nini anganganie timu ambayo inafungwa tuuuuu kila siku, sio kweli kwamba hii inaharibu CV yake. Makocha wastaarabu wakiona CV inaingia doa wanaacha au timu ikifungwa na wadau wakilalamikakufuatia kufungwa wanakubali kuachia ngazi. Huyu wetu ana nini anachongangania.
 
Back
Top Bottom