Shughuli imemalizika pale Qatar, Argentina ya Lionel Messi inaenda kubeba Ubingwa wa Dunia 2022

Tumekuwa na wakati mzuri sana kuangalia kombe la dunia na sasa tunakaribia kufika mwisho. Kila timu imevuna ilichopanda. Argentina ndio timu bora zaidi kwenye michuano hii.

Lionel Messi anaenda kuwa kinara baada ya mchezo mkali dhidi ya Ufaransa. Atastaafu kwa heshima kama mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu.

Nafasi ya tatu nampa Croatia na pongezi za pekee kwa Morocco kuweza kufika nusu fainali. Hawa wajifunze kuepuka ubaguzi ili miaka ijayo wafike mbali zaidi.
mimi sijaelewa jamani Morocco walimbagua nani?
je siyo kweli kwamba wao siyo waafrica?
je siyo kweli kwamba 90% ya raiya wa moroko ni waislam?
Tusikasirike, tuandae timu za kuweza kushindana na morocco
 
Basi kubahatisha matokea siku moja tayari umeshakuwa sheh yahya.
 
Ticket iliyowapeleka huko WC ni ya wapi kama si Africa ?! Wangeenda kwa Ticket ya bara Asia nani angewa mind ?.

Timu za Africa nyingi zinailemea hiyo Morocco. Na wao wanajua
 
laana la kuku halimpati mwewe. tuandae vya kwetu mkuu
 
mimi sijaelewa jamani Morocco walimbagua nani?
je siyo kweli kwamba wao siyo waafrica?
je siyo kweli kwamba 90% ya raiya wa moroko ni waislam?
Umewahi kusikia Brazil wakisema huu ushindi ni wa Brazil, Latin America na wakatoliki? Hawatamki hivyo kwasababu mashabiki wake wapo dunia nzima na wana asili mbalimbali na itikadi tofauti.

Mpaka hapo utakuwa umeelewa.
 
Basi kubahatisha matokea siku moja tayari umeshakuwa sheh yahya.
Dogo hebu soma nyuzi nilizoanzisha tangu kombe la dunia lianze.

Umewahi kusikia Brazil wakisema huu ushindi ni wa Brazil, Latin America na wakatoliki? Hawatamki hivyo kwasababu mashabiki wake wapo dunia nzima na wana asili mbalimbali na itikadi tofauti.

Mpaka hapo utakuwa umeelewa.
Hivi ulishawahi kujiuliza kwann Argentina hakuna watu weusi? yaani nchi inapakana na nchi zenye watu weusi halafu kwao hamna weusi ni 0.37% tu ya watu weusi, kama hampendi ubaguzi mbona hata jezi zao zipo madukani na watu wananunua?
Argentina wanachinja watu weusi kabisa na tunawashabikia, sembuse waarabu tena waliozaliwa na kukulia ulaya wakijiita Wamorocco?
Soma historia ya Argentina na watu weusi
 
Hatuwezi kushabikia mpira kwa kuangalia historia kwasababu hata uingereza ligi yao tutatakiwa kuiacha.

Katika miaka hii hatujawahi kusikia Argentina wakitangaza ubaguzi sehemu yoyote wala kuwabagua watu weusi.

Huyo Messi mwenyewe rafiki yake mkubwa ni Neymar ambaye ana asili ya weusi. Mentor wake pale Barcelona alikuwa Ronaldinho ambaye ni black.
 
Hivi ulishawahi kujiuliza kwann Argentina hakuna watu weusi? yaani nchi inapakana na nchi zenye watu weusi halafu kwao hamna weusi ni 0.37% tu ya watu weusi, kama hampendi ubaguzi mbona hata jezi zao zipo madukani na watu wananunua?
Argentina wanachinja watu weusi kabisa na tunawashabikia, sembuse waarabu tena waliozaliwa na kukulia ulaya wakijiita Wamorocco?
Soma historia ya Argentina na watu weusi
Mbona moroko hamna wazungu wakati imepakana na hispania kabisa?
 
Namwona Lisandro Martinez akicheza kama kiungo mkabaji sambamba na viungo wengine kama depaul, Mac alister na Enzo. Ila kwa game la ufarans kiungo kama Paredes ni muhimu sana why?? Paredes ni mkabaji pia anauwezo wa kupanikisha mpinzani ana ukabaji flan hv wa kukera ambao kupata kadi ni ngumu. Coach ampange Martinez kama kiungo mkabaji badala ya Paredes dogo anakaba vzr kama Otamendi hatacheza coz ya kadi bhs akae beki ila wasiruhusu cross maana Giroud atawaua
 
France ni kumkaba Messi tu, kazi yao kubwa ipo hapa. Hakuna kazi nyingine kubwa kwao zaidi ya hii. Na ili ufanikishe hili walau uwe na viungo wakabaji wenye mapafu ya punda kama Ngolo Kante, Kroos n.k

Sioni namna France wanavyoweza kumzima Messi pale kati. Yule dogo Alvarez ni moto mwingine, huyu Varane aliyeanza kuflop Madrid na kwenda Man U sioni kama anaweza akamzima huyu dogo.

All in all, kioengele ni Messi. Kumshika huyu jamaa ni kufanya viungo wako wote wawe attention kwake, na hapo ni kama unabet tu sababu wanaweza wakamuweka chini ya uangalizi na bado wasimuweze.
Huyo jamaa hakabiki.

Ukikaza fuvu kujifanya unataka battle ya kukaka utakula yellow au umeme na wao watapewa penalty

Wanacheze nae kwa akili wasilte ujuaji

Yule jamaa umri umeenda lakini Yuko vile vile kama zamani so usimchukulie poa yule kazaliwa kwa ajili ya mpira.
 
Kwa sehemu kasi amepungua na hii ni kutokana na umri. Messi alikuwa na uwezo wa kuchukua watu kadhaa na kwenda kuweka mpira wavuni ila kwa sasa hawezi akipindua watu ila kasi ya kukimbia haipo tena kwa sehemu kubwa.
 
Namwona Lisandro Martinez akicheza kama kiungo mkabaji sambamba na viungo wengine kama depaul, Mac alister na Enzo. Ila kwa game la ufarans kiungo kama Paredes ni muhimu sana why?? Paredes ni mkabaji pia anauwezo wa kupanikisha mpinzani ana ukabaji flan hv wa kukera ambao kupata kadi ni ngumu. Coach ampange Martinez kama kiungo mkabaji badala ya Paredes dogo anakaba vzr kama Otamendi hatacheza coz ya kadi bhs akae beki ila wasiruhusu cross maana Giroud atawaua
Mechi za fainali kadi za njano huwa zinafutwa labda kama utaratibu umebadilika siku hizi.
 
Ngoja nichukue siti hapa na kombe (mug) langu la kahawa na bakuli la mbegu za maboga ili nishuhudie huu mtanange.
 
Back
Top Bottom