Style ya Morocco haina utofauti mkubwa na Argentina. Wote wanaruhusu uwafikie langoni mwao kisha wakupoke mpira na wafanye counter attack.
Jana Ufaransa alikuwa anapigwa hata goli 5 au 6, hii ilitokana na ubutu wa umaliziaji ndani ya box kwa Morocco. Kwa namna hii, kwa defence hii ya France, kwa mids zile za Ufaransa. Sijui nisemeje.
Messi ashuke chini kusaidia viungo wa Argentina. Wale madogo wawe wanapanda juu punde Messi anapokuwa na mpira, sioni kama Ufaransa itapona. Argentina akiwa karibu na box au akiwa ndani ya Box ni hatari saaaana.
Karata pekee ambayo France anayo ni kumtengenezea mazingira mazuri Mbape. Dembele ana kasi ila hana madhara makubwa, Griezmann ni wa kawaida kwa soka la sasa, hawa wanaweza wakakabika ila Mbape ni kipengele.
Binafsi karata yangu naitupa kwa Argentina japo lolote laweza kutokea.