Shughuli ya kuaga mwili wa Hayati Edward Lowassa Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam

Shughuli ya kuaga mwili wa Hayati Edward Lowassa Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam

Yule chifu,,usimchukulie kitoto amezaliwa mjini busara na hekima nyingi lakini ni mafia wewe muone akicheka cheka ukajua NI boya Fulani,,weka mbali na watoto,,Kagame wa demokrasia(Kisasa) achana na yule Kagame wa rwanda dikteta.
Wamesharudisha baada ya hutuba ya jakaya kupitia Je , ni Bahati mbaya AU walipanga iwe hivyo
 
Kweli,
msiba ni wataifa....mzee warioba nimependa speech yake kuzungumza vizuri sana..
Mzee Warioba is a "by the book" kind of guy. Stand up guy. Hapendi longolongo.

Ndiyo maana kasema ukweli kuhusu Lowassa bila aibu.

Alivyokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria, Nyerere alimuamuru amkamate na kumfunga mtu fulani ambaye alikuwa kaachiwa na mahakama, kwa kosa lile lile.

Warioba akamwambia Nyerere hilo jambo kisheria haliwezekani.

Nyerere akamuuliza, kwa nini?

Warioba akajibu kuwa, huyu mtu mahakama imeshamuachia, hawezi kukamatwa kwa jambo lile lile, hiyo ni "double jeopardy". Kisheria ni kosa.

Nyerere kila akitaka kubisha, Warioba anamletea vifungu vya sheria tu.

Mwishowe Nyerere akakubali kushindwa.

Wanasema Nyerere haambiliki, lakini kwa Warioba kwenye sheria alikubali kufunga breki mwenyewe.

Halafu hapo ndiyo ana heshima kweli kweli kwa rais. Ila kwenye facts hakutaka kupindisha.

Huyo ndiyo Warioba.
 
Ukizungumzia waasisi wa UFISADI ndani ya Taifa la Tanzania, huwezi kuacha kumtaja marehemu.

Apumzike panapostahili.
Sasa hivi yeye mpambanaji tena wabongo ni watu waovyo sana bure kabisa...yaani takataka
 
Kauli ya Warioba kuwa lowasa alikuwa na uchungu sana baada ya kuambiwa Nyerere ndiye alizuia urais wake 1995 imenifikirisha mengi kuhusu ugonjwa na kifo cha Nyerere.
Wabongo bhana....

Nyerere alikuwa binadamu pia, kuugua na hata kufa hakukwepeki kwa wanadamu.
 
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kwenye shughuli kuaga mwili wa Edward Lowassa inayofanyika leo tarehe 2/23/2024 katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.


Salamu kutoka kwa viongozi mbalimbali

Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye
: Tunayo mengi ya kumkumbuka Lowassa

Rais Mstaafu Ali Mohamed Shein: Lowassa alikuwa akinivutia kwenye utendaji wake.

Jaji Joseph Warioba

1995 Lowassa alinitafuta akiwa na uchungu sana baada ya kuambiwa Nyerere ndio aliyetia ugumu kuwania Urais. Nilimtia moyo, hakukata tamaa.

2008 Lowassa alinitafuta baada ya kujiuzulu, alisema hakutendewa haki, wamemuhukumu bila kumsikiliza, alinitafuta tukazungumza, nilimwambia haya ni mambo ya kisiasa, asikate tamaa.

Alikuwa alipenda elimu, ni mtu mwenye imani kuwa ana wajibu wa kutumikia taifa, hakuwa mangimeza, alikuwa mtu wa vitendo, pamoja na mapungufu yake hakuwa mtu anayependa kugombana na watu, alikuwa kiongozi mvumilivu, alikuwa ni kiongozi mwenye sifa ya kuwa kiongozi, mwenye maono.

Jakaya Kikwete atoe pole kwa familia kwenye msiba huu mkubwa.

Rais Hussein Mwinyi: Nimejifunza kutoka kwa Lowassa Uzalendo, uwajibikaji, ushirikiano na makundi mbalimbali na pamoja na kuweka mbele maslahi ya nchi.

Makamu wa Rais Philip Mpango: Alikuwa mtetezi wa maslahi wa wananchi wake wa Monduli, nasi tunapaswa kumuiga katika utumishi wetu

R.I. P kiongozi wetu
 
Back
Top Bottom