Ukiwa mzembe unasemwa tu, ndio desturi yetu hapa Kenya, haturembi wala kumumunya maneno, yaani nimewahi kumualika Mtanzania kwenye kikao cha Wakenya kazini, dah aliogopa sana maana humo tulikua tunaambiana kama ilivyo, baadaye sote tunakutana kunywa chai na kucheka.
Hata hapo Tanzania nimewahi kuwa kwenye kikao ambacho tulikutana Wakenya kila mmoja anawakilisha kampuni ya Kitanzania, aisei Watanzania walitushangaa sana, yaani kila kitu kinawekwa mezani, unaanikwa na kuambiwa wazi wazi udhaifu wako. Baada ya kikao sote tunapiga stori za kwaida na kucheka.
Tatizo ujamaa uliwaharibu sana nyie, ndio unaona hata spika wenu anavurugika kiakili kisa CAG amesema bunge lina udhaifu, hamjazoea kuambiwa na mtu asiye mnafiki.