Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Hakuna kipindi Ambacho nimeshuhudia mafundi ujenzi wakiwa Bize mitaani kama awamu hii ya Rais Samia. Muda wote na siku zote unaona mafundi wakiwa katika site mbalimbali wakiendelea na shughuli za ujenzi. Ni wao tu kuchagua mahali pa kwenda kati ya miradi ya serikali au ya watu binafsi.
Ukipita mitaani unaona maeneo mbalimbali ujenzi wa Miradi ya shule ,zahanati na vituo vya afya ukiendelea kufanyika na kutekelezwa kwa kasi kubwa sana. Lakini pia ukija kwa watu binafsi nako mambo ni moto kwelikweli kwa sababu watu wanainua majengo na miradi mbalimbali kama uyoga. Hali inayopelekea mafundi kuwa Bize muda wote.
Hali hii imechochea hata mzunguko wa pesa kuwa wenye afya mitaani .kwa sababu biashara za vifaa vya ujenzi,chakula n.k.Vimekuwa na soko kubwa sana mitaani. Kila unakopita unaona nyumba ,magodown ,fremu za biashara,nyumba za kupangisha zikijengwa usiku na mchana.
Hiyo yote ni kutokana na sera nzuri za kiuchumi za Rais Samia ambaye ameamua kugusa na kujenga uchumi unaogusa Maisha ya watanzania moja kwa moja. Ndio maana kwa sasa husikii habari za vyuma vimekaza. Kwa sasa ni wewe tu kujituma kuchapakazi na kuamua kutokuchagua kazi.
Hii ndio maana kila mtanzania anaona nafasi ya yeye kutimiza ndoto zake wakati huu wa Rais Samia.ndio maana watu wanaunga mkono Rais Samia kuendelea kuongoza Taifa letu kwa muhula wa pili. kwa sababu wanaona nuru na tumaini mbele yao .
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.