Shughuli za Vyama vya Siasa nchini Mali zimepigwa marufuku

Strong ladg

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
1,357
Reaction score
3,114
Serikali ya kijeshi ya nchini MALI imetangaza kusitishwa kwa shuguli zote za vyama vya kisiasa nchini humo hadi hapo itakapotangazwa tena. Tangazo hilo limetolewa tarehe 7 May 2025 kupitia televisheni ya taifa.

Tangazo hilo limekuja ikiwa ni siku chache tangu serikali hiyo ilipotangaza azimio la kupunguza idadi ya vyama vya siasa hadi kubakia vitano pekee na kusitisha utoaji ruzuku kwa vyama hivyo.
Hivyo basi nchini Mali kwa sasa, chama cha siasa au kikundi chochote kinachojihusisha na masuala ya kisiasa hakiruhusiwi kufanya shughuli zake

CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la habari la Mali( ORTM)
 
Futa kabisa ujinga wa siasa ili watu wafanye kazi ,kila siku wanafuatilia watu ambao hawajengi zaidi ya meneno..Huku wanamsifia Tundu Lissu sijui ana nin cha maana cha kusifia bdala ya kusifia wagunduzi wakubwa kazi ni kushughulika na wapiga domo wa siasa kama simba na yanga.
 
Hii ndio Afrika ninayoijua mimi.

"Let us all agreed that Black people cannot rule themselves, Whites are born in order to rule and Blacks are born to be ruled."
Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
 
Futa kabisa ujinga wa siasa ili watu wafanye kazi ,kila siku wanafuatilia watu ambao hawajengi zaidi ya meneno..Huku wanamsifia Tundu Lissu sijui ana nin cha maana cha kusifia bdala ya kusifia wagunduzi wakubwa kazi ni kushughulika na wapiga domo wa siasa kama simba na yanga.
Na kusifia kwa kubandika mabango nchi nzima?
 
Kwa viongozi wanao jali maslahi ya nchi zao ni sawa tu kutokua na vyama vingi BUT kwa aina ya viongozi tulio nao Africa, vyama vingi ni muhimu sana. Kwa hizi nchi zilizo tawaliwa na France and then wazalendo wakapindua, ni sawa tu kufuta multipart system. Imagine IMF na WB wanatutaka tutoe ruzungu kwa vyama vya siasa lakini wanatuzuia tusitoe ruzungu kwa wakulima, halafu tukakubali. Sie ni wa kupimwa akili yaani
 
Kutoa ruzuku kwa Vyama vya Siasa siyo jambo la lazima, ni Uamuzi tu.

Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa vilivyo huru ni jambo la muhimu sana kuwepo katika nchi katika dunia hii ya Sasa.
 
Ajabu Wadanganyika watamsifia na wamemuelewa Traore kwa uamuzi huo, huu si ni uamuzi uliwahi pingwa hapa na wadanganyika hawa hawa miaka 5 nyuma?

Tena walisema, DEMOKRASIA ni SIASA, UHURU ni KUFANYA SIASA, MAENDELEO ni UANASIASA etc

Kama mkisema kile kiumbe hakieleweki, basi hamuwafahamu WADANGANYIKA
 
Serikali ya kijeshi ya nchini MALI imetangaza kusitishwa kwa shuguli zote za vyama vya kisiasa nchini humo hadi hapo itakapotangazwa tena. Tangazo hilo limetolewa tarehe 7 May 2025 kupitia televisheni ya taifa.

Tangazo hilo limekuja ikiwa ni siku chache tangu serikali hiyo ilipotangaza azimio la kupunguza idadi ya vyama vya siasa hadi kubakia vitano pekee na kusitisha utoaji ruzuku kwa vyama hivyo.
Hivyo basi nchini Mali kwa sasa, chama cha siasa au kikundi chochote kinachojihusisha na masuala ya kisiasa hakiruhusiwi kufanya shughuli zake

CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la habari la Mali( ORTM)
Yapo mengi ya kufutwa yaliyoletwa na wazungu mabepari.Vyama vya siasa ni mzigo kwa taifa na tanuri la kugombanisha watu.
 
Yapo mengi ya kufutwa yaliyoletwa na wazungu mabepari.Vyama vya siasa ni mzigo kwa taifa na tanuri na kugombanisha watu.
Yaani hapa wanasiasa wanakuwa popular kuliko hata wagunduzi na watu wenye tija ,wanashabikia wapiga domo ,utasikia wakili msomi ,hawa wengine kila siku kugombana na serikali ili watrend ...Wanataka watu waache kazi wafuatilie kesi zao

Siasa hazina tija ni ushabiki kama simba na yanga ..Ni kikwazi cha maendeleo.
 
Siasa ni Kitovu cha Umaskini kwa nchi za Afrika na zingine za calibre hiyo,,, Demokrasia ni utapeli na si kitu halisi, inatumiwa na watu kudidimiza wengine kirafiki..
Nchi zilizoendelea zimepitia mikono ya chuma..
Kwasababu wanasiasa kila siku wanawaza Uchaguzi unaofuata...
 
Ajabu Wadanganyika watamsifia na wamemuelewa Traore kwa uamuzi huo, huu si ni uamuzi uliwahi pingwa hapa na wadanganyika hawa hawa miaka 5 nyuma?

Tena walisema, DEMOKRASIA ni SIASA, UHURU ni KUFANYA SIASA, MAENDELEO ni UANASIASA etc

Kama mkisema kile kiumbe hakieleweki, basi hamuwafahamu WADANGANYIKA
Traore hayupo Mali, yupo Burkina Faso. Kiongozi wa Mali anaitwa Jenerali Assimi Goita
 
Kutoa ruzuku kwa Vyama vya Siasa siyo jambo la lazima, ni Uamuzi tu.

Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa vilivyo huru ni jambo la muhimu sana kuwepo katika nchi katika dunia hii ya Sasa.
Ukichukua pesa za IMF na WB, kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa ni mojawapo ya sharti yaani ni lazima. Lakini kutoa ruzuku kwa wakulima, wavuvi na wasiojiweza wanakukataza. Pia wanakwambia upunguze bajeti ya huduma za kijamii mfano elimu na afya. Wanakwambia upunguze idadi ya taasisi za kielimu na uruhusu bidhaa kutoka nje mfano mitumba ziingie bila vikwazo. Lengo ni kuua viwanda vyako na kukutengenezea utegemezi.
 
Ajabu Wadanganyika watamsifia na wamemuelewa Traore kwa uamuzi huo, huu si ni uamuzi uliwahi pingwa hapa na wadanganyika hawa hawa miaka 5 nyuma?

Tena walisema, DEMOKRASIA ni SIASA, UHURU ni KUFANYA SIASA, MAENDELEO ni UANASIASA etc

Kama mkisema kile kiumbe hakieleweki, basi hamuwafahamu WADANGANYIKA
Embu Kajikumbushe Vizuri Traore Ni Kiongozi Wa Nchi Gani Then Ndio Urudi Tena..Punguza Mikurupuko Dogo
 
Yaani hapa wanasiasa wanakuwa popular kuliko hata wagunduzi na watu wenye tija ,wanashabikia wapiga domo ,utasikia wakili msomi ,hawa wengine kila siku kugombana na serikali ili watrend ...Wanataka watu waache kazi wafuatilie kesi zao

Siasa hazina tija ni ushabiki kama simba na yanga ..Ni kikwazi cha maendeleo.
"Wagunduzi" ndio watu gani katika nchi hii lakini unataka mfumo gani utumike kwa watu kupata viongozi wao na akishapatikana kama ni fisadi wa kutupwa na genge lake unataka afanyweje..!?

Msiongee tu kama mapunguani bila kushauri njia mbadala, mnakuwa tu kama watu wa vijiweni.
 
Kiongozi sio mpiga domo ,hakuna kiongozi anaweza kukuletea maendeleo ,tufanye kazi kwa sababu wanasiasa ni matapeli.
 
Back
Top Bottom