Shughuli za Vyama vya Siasa nchini Mali zimepigwa marufuku

Shughuli za Vyama vya Siasa nchini Mali zimepigwa marufuku

Kiongozi sio mpiga domo ,hakuna kiongozi anaweza kukuletea maendeleo ,tufanye kazi kwa sababu wanasiasa ni matapeli.
Sasa hao viongozi wanakuwepo wa nini kwa nini nchi zisikae tu bila viongozi na watu wapige tu kazi.
 
Serikali ya kijeshi ya nchini MALI imetangaza kusitishwa kwa shuguli zote za vyama vya kisiasa nchini humo hadi hapo itakapotangazwa tena. Tangazo hilo limetolewa tarehe 7 May 2025 kupitia televisheni ya taifa.

Tangazo hilo limekuja ikiwa ni siku chache tangu serikali hiyo ilipotangaza azimio la kupunguza idadi ya vyama vya siasa hadi kubakia vitano pekee na kusitisha utoaji ruzuku kwa vyama hivyo.
Hivyo basi nchini Mali kwa sasa, chama cha siasa au kikundi chochote kinachojihusisha na masuala ya kisiasa hakiruhusiwi kufanya shughuli zake

CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la habari la Mali( ORTM)
Kazi kweli kweli
 
Tunakata mfumo wa kifalme na kichifu sio ujinga wa kufuata wazungu.
Ufalme Afrika haiwezekani atajilimbikizia mali na kunyang'anya watu wake zao na kuua wanakosoaji wake.

Huo mfumo ulishafeli kitambo Afrika na hakuna namna ataweza kupatikana.
 
Ufalme Afrika haiwezekani atajilimbikizia mali na kunyang'anya watu wake zao na kuua wanakosoaji wake.

Huo mfumo ulishafeli kitambo Afrika na hakuna namna ataweza kupatikana.
Bora kuliko kutumia bilion za kufanya uchaguzi na ruzuku
 
Bora huyo mwamba anata vibaki vyama vitano, kuna mwamba alitaka kibaki kimoja na hicho kimoja kusiwe na ushindani kwenye ile nafasi kubwa, wakati wa fomu inaandaliwa fomu moja pekee.
 
Huyo mfalme atapatikanaje..? Hizo ni ndoto za kulewa viroba tu.
Naona umelanduka ,ukoo mmoja unashikilia nchi hata milele na wengine tunapiga kazi ..Hapatokuwa na ujinga wa siasa wala kutekana.
 
Naona umelanduka ,ukoo mmoja unashikilia nchi hata milele na wengine tunapiga kazi ..Hapatokuwa na ujinga wa siasa wala kutekana.
Hakuna kitu kama hicho, hatuwezi kurudi kwenye karne ya 18 hata waarabu tu unaona sasa hivi wakipata fursa tu wanakimbilia nchi za magharibi ili kukwepa kuishi kwenye dunia ya karne ya saba.
 
Demokrasia ni bangi mbaya sana Africa 🌍, tukiiacha tutapiga hatua ya maendeleo
 
Hakuna kitu kama hicho, hatuwezi kurudi kwenye karne ya 18 hata waarabu tu unaona sasa hivi wakipata fursa tu wanakimbilia nchi za magharibi ili kukwepa kuishi kwenye dunia ya karne ya saba.
Dubai na sisi wenye demokrasia hapa Afrika hivi ni nani yupo karne ya saba?
Na hizo nchi za Magharibi mbona zenyewe bado zina wafalme. Uingereza hauwezi kuwa waziri mkuu hadi uidhinishwe na mfalme tena kwenye makaratasi inasomeka umeteuliwa na mfalme. Viongozi wa Australia wanaapa kumtii mfalme wa Uingereza. Uhispania kuna mfalme, Uholanzi kuna mfalme, Sweden kuna mfalme. Hao wafalme wanakula bure tu kwenye makasri na hawafanyi chochote wala hawana mamlaka yoyote?
 
Hakuna kitu kama hicho, hatuwezi kurudi kwenye karne ya 18 hata waarabu tu unaona sasa hivi wakipata fursa tu wanakimbilia nchi za magharibi ili kukwepa kuishi kwenye dunia ya karne ya saba.
Hapa ndio ujinga unapoanza ,umeanza kuandaliwa kuwa mjinga kuanzia ulipoanza darasa la kwanza ..Pole sana!
 
Back
Top Bottom