Shuhuda: Chanzo cha moto soko la Karume ni mateja, waliangusha mshumaa wakati wanatengeneza mihadarati

Shuhuda: Chanzo cha moto soko la Karume ni mateja, waliangusha mshumaa wakati wanatengeneza mihadarati

mishumaa ni hatari sana imeshasababisha majanga kama hayo mengi sana. ndio maana siku hizi wenye nyumba wengi wanapiga marufuku matumizi yas mishumaa baada ya koroboi za mchina kuwa nyingi

Nafahamu mkuu madhara yake...ila huyo jamaa sio kuwa anatupanga tu?

Chanzo cha moto waliopaswa kukitaja ni jeshi la polisi/zimamoto...
 
Cloudsfmtz "Chanzo cha moto ni mateja ambao tupo nao sokoni Karume ambao wao wanajihusisha na kuuza viatu , unajua pale sokoni kuna moja ya banda ambalo wao huwa wanalitumia kutengeneza mihadarati yao ambayo huwa wanatumia mishumaa kuitengeneza na siku hiyo mshumaa ulianguka na kuanza kuungua " Thomas Benedicto , Mfanyabiashara na shuhuda wa moto soko Karume #PowerBreakFastView attachment 2085884
Naona "Mateja" wanawatetea "Mateja", ni mwendo kuteteana.
 
Huu ni upuuzi na ujinga, huyo mtu katumwa na nani akatoe hiyo kauli?'kwanini asisubiri majibu ya ripoti ya tume?

Ukweli umeanza kuwachoma, siri zao zimejulikana, ni wao ndio huchoma hayo masoko moto usiku, huyo kibaraka waliemtuma Clouds apuuzwe.
 
Cloudsfmtz "Chanzo cha moto ni mateja ambao tupo nao sokoni Karume ambao wao wanajihusisha na kuuza viatu , unajua pale sokoni kuna moja ya banda ambalo wao huwa wanalitumia kutengeneza mihadarati yao ambayo huwa wanatumia mishumaa kuitengeneza na siku hiyo mshumaa ulianguka na kuanza kuungua " Thomas Benedicto , Mfanyabiashara na shuhuda wa moto soko Karume #PowerBreakFastView attachment 2085884
Clouds Fm ni tawi la CCM, hapa wanatumia Watu kujikosha, si tume imeshaundwa, atulie uchunguzi ufanyike. Clouds na TBC usiziamini kamwe
 
Cloudsfmtz "Chanzo cha moto ni mateja ambao tupo nao sokoni Karume ambao wao wanajihusisha na kuuza viatu , unajua pale sokoni kuna moja ya banda ambalo wao huwa wanalitumia kutengeneza mihadarati yao ambayo huwa wanatumia mishumaa kuitengeneza na siku hiyo mshumaa ulianguka na kuanza kuungua " Thomas Benedicto , Mfanyabiashara na shuhuda wa moto soko Karume #PowerBreakFastView attachment 2085884
Huu ushahidi unafikirisha sana, moto umeanza saa 7, hao mateja wakat wanadondosha huo mshumaa huyo shuhuda ye aliangalia tu na asiende kuzima huo mshumaa? Ushuhuda huu km sio wa michongo! Mi acha nishukie hapa japo sijafika kituo changu

Sent from my TECNO BC2c using JamiiForums mobile app
 
Bwana Thomas Benedicto kwanza i guess sio jina lk halisi, lkn je wakati huo yy alikuwa wapi? yy pia ni teja? mateja hufanya haya kwa kujificha yy Benedicto alikuwa amepiga pose wapi kusubiri mshumaa uwe chanzo cha moto huo? Inafikirisha!!!
Mara anadai yeye ni Mlinzi na wakati mwengine anajisahau anasema yeye ni mfanyabiashara. Huu ni Ushuhuda wa MCHONGO na umejaa UHUNI
 
Muda huo shuhuda huyo alikuwa wapi!! Huyu jamaa wala siyo mfanyabiashara ni type ya yule mwandishi aliyefariki kwenye mazishi akaagwa kijeshi anajaribu kutengeneza mazingira ya kuonyesha siyo serikali iliyohusika na uchomaji wa soko kama watu wengi walivyodai
Ndio mimi nimeuliza swali hilo hilo, kwamba alishuhudia tu mshumaa bila kuuzima au kutoa taarifa?
 
Back
Top Bottom