Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Don255,
Nimepima last week naitafuta 85 naumia lakini ratiba yangu nayo haina muda wa kutulia!!..
Mwenye kujua kupungua bila zoezi msaada tafadhali!!.. Huo ugoigoi poa tu
 
Mm mazoezi siwezi zaidi ya kutembea kwenye mizunguko ya kazi
Nimefatisha lishe sahihi tu kutoka 95 kgs mpaka 72-75 sizidi hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo nimecheki BMI bado nasomeka niko overweight inasoma 29. Inabidi nipunguze uzito hadi kgs 72. Duuh!
Jitihada inahitajika from 79 - 72 kupunguza kilo 7.

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
Mkuu BMI inatumika vipi nielekeze niefahamu kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jambo pekee linalonisaidia ni kula pale ninapojisikia njaa tu.

Kuna siku zingine nagombana na wife usikui kapika na mimi sina njaa namuambia nifanyie tangawizi tu anamaindi anataka nile japo kidogo.

Ila kikubwa kula unapojiskia njaa.

Mimi nina wiki ya pili saivi sijawahi kula chai ya kueleweka asubuhi na kunywa maji lita moja sijiskii njaa mpaka mchana.

Na sijui lini nimefanya mazoezi ila ukiniona unaweza hisi kama nafanya mazoezi.ila nina mda mrefu sijafanya mszoeiz.

Foluma ni kula utakaposikia njaa basi.

Na hapo utakuwa huru kula chochote kile hata chips haina shida na ule kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishu ni kula unspojisikia njaa tu.

Pitia hapa huu uzi



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu BMI inatumika vipi nielekeze niefahamu kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kiufupi BMI (Body Max Index) Ni kipimo ambacho kinatoa mlingano baina ya uzito wa mtu kwa urefu wake, ambapo uzito katika SI unit yoyote itakayokuwa lakini urefu uwe square.
Mfano:
Uzito ukiwa kg = urefu m²
Uzito ukiwa pound = urefu inch²
Ambapo kipimo hiki hutoa majibu ya kuanzia 18-24.9 Kawaida, 25-30 Uzito mkubwa na 30 na kuendelea ni Uzito uliopitiliza. Sio kipimo cha kutambua rasmi afya ya mtu, isipokuwa ni kwa ajili ya kuangalia uzito kulingana na urefu.

cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
 
Don255,
Hongera sana.Umeandika vizuri na kutia hamasa.

Binafsi nilikuwa na kilo 92 wakati kwa mujibu wa BMI yangu nilitakiwa kuwa na kilo 81.

Nilianza kuitwa bonge.Na nilianza kupata matairi kiunoni Kangi.

Kilichonisaidia ni mazoezi ya kukimbia.Nilikuwa nakimbia dakika 30 walau mara nne kwa wiki.Pia nilikuwa naingia kufanya weight lifting na sit ups.Nilipunguza kabisa ulaji wa chips.Nilipunguza pia unywaji bia isipokuwa weekend.

Ndani ya miezi mitano nilifikia lengo la kuwa na kilo 81.Size ya kiuno ilipungua kutoka futi 36 mpaka 34.Sasa ivi nina six packs.Shinikizo la damu lilianza kuninyemelea ila kwa sasa halipo tena.

Mazoezi ni njia pekee.
 
Dah nimetoka kapa.

Sijaelewa mkuu.

Nielekeze namna ya kutumia baada ya kudownload

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna haja ya kudownload, hata online vipo search BMI, utakuta kuna sehemu ya kuingiza urefu wako, na sehemu ya kuingiza uzito na kuna sehemu ya matokeo

cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
 
Dah nimetoka kapa.

Sijaelewa mkuu.

Nielekeze namna ya kutumia baada ya kudownload

Sent using Jamii Forums mobile app
Pima uzito wako katika kg na urefu wako kwa cm

Kisha ingia hapa

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…