Ngoja niwaambie kitu kuhusiana na Diet na kupunguza mwili...watu wengi wana amini ku acha kula mlo mmoja kunaweza kukakufanya upungue SIO KWELI
...Kama unaamua kufanya diet kwa ajili ya kupungua mwili fanya yafuatayo
...Punguza kula vyakula vyenye asili ya wanga na sukari...tumia kipimo cha ngumi yako(yaani kula ugali au wali saiz ya ngumi yako)...unatakiwa ule sana mboga za majani na samaki(nyama nyeupe)
...mboga za majani hazina madhara kula kwa wingi uwezavyo...kula sana matuda yatakusaidia kupata nyuzi nyuzi(fibers)...hizi husaidia kusaga chakula kwa haraka
Hujaelewa?...Fanya hivi
Asubuhi ukiamka jitahid upate grass moja ya maji ya uvugu vugu(ukiitia ndimi au tangawizi ni bora zaid)
...Chai yako unaweza kula siles ya mkate moja au chapat moja au andazi 1(shughuli enhee[emoji23] ndo unapunguza wanga hivo)
...Mchana kula ugali saiz ya ngumi yako na mboga za kutosha pamoja na matunda...ukijisikia njaa kila tena ,ukijisikia tena njaa kula(kula saizi ndogo ya chakula utakapojisikia njaa...usile mpaka ukashiba sna
...Sema hapana kwa chips
....sema hapana kwa soda
.....Sema hapana kwa nyama nyekundu(ya ng'ombe,mbuzi
.....Kunywa maji mengi
.....kula kuku(bila ya ngozi yale)
FANYA MAZOEZI ...narudia tena FANYA MAZOEZ
...Kwa wale ambao wanasema wanafunga kupunguz uzito ni kweli kufunga kunapunguza mafuta mwilini....kivip? Kipi unatakiwa ufanya check hpa[emoji1484]
...Kwa kawaida mwilinwa binaadam huchukua masaa 8 kumaliza chakula kilichopo tumboni na kuanza kutumia mafuta yaliyo mwilini(kwenye cell)....hivo kama unataka utumie funga kumaliza mafuta mwilini hakikisha unafungulia na vyakula vyenye virutubisho na si wanga
Kivip? MFano umekula daku saa 8 usiku....uka kaa na njaa mpaka saa 12 jioni maana ake kuna mafuta yashatumika mwilini hivo basi jitahid hiyo saa kumi na mbili jioni ufungua kwa maji ya uvuguvugu(umeona enhee huwa tunafakamia ya baridi hapa[emoji23])...futari yako iwe nyepesi kama ni viazi viwe viwili mboga za majani na matunda kwa wingi
Kwa nini watu wanafeli?...watu wengi wanafunga lakini wanafungua kwa futari nzito na soda mpaka tumbo lina jaa...huwezi KUPUNGUA...kwa leo ni hayo(unaweza nirekebisha pia maana mimi sio mtaalamu wa rishe) nimeshea tu uzoefu maana nilikuwa mnene wazee[emoji23][emoji23]...nkitembea hatua mbili tu jasho naweza hata mwagilia mchicha
...Nikipata mda ntakuja niwaambie kuhusu Supu ya kabichi na kupunguza unene(japo mm ilinishinda[emoji23][emoji23][emoji23])...wewe sikukatish tamaa....jambo la kuzingaitia USITUMIE MADAWA YA KUPUNGUZA UNENE....ntakuja hapa kuelezea madhara yake
Sent using
Jamii Forums mobile app