Shujaa wa Taifa au alikuwa Kiongozi wa kiimla?

Shujaa wa Taifa au alikuwa Kiongozi wa kiimla?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,480
Reaction score
7,443
Miaka ya tisini nikiwa bado kijana mchakalikaji nilikuwa mtu wa kusafiri sana na katika safari zangu nje ya nchi nilikuwa na kutana na raia wa nchi mbalimbali na mojawapo ni nchi ya Kenya. Siku moja nilikuwa na napiga story na Wakenya juu ya Rais wa Kenya wakati huo Daniel Arap Moi. Na mimi nilimsifia sana Moi hasa juu kuwa kiongozi aliyekuwa anasomesha watoto maskini bure na kugawa maziwa shule za msingi na awali. Na nilimsifia zaidi niliposikia kuwa ana shule inaitwa Kabarak na husomesha watoto maskini.

Lakini kwa mshangao mkubwa baadhi ya Wakenya waliniambia kuwa Moi alikuwa muuaji mkubwa na dikteta na inasadikiwa hata alimuua Robert Ouko. Mimi nilikaa kimya na sikuamini.

Je, kiongozi wetu ambae tunaomboleza kifo chake ,kila mtu anajua amefanya makubwa kujenga taifa la Tanzania. Yupo kundi kama la akina Hayati Moi?
 
Hatari na nusu kashaenda sasa hakuna namna maana walitaka aongezewe muda waendelee kula keki ya taifa kwa kusifia Mungu fundi sana aisee wameumbuka na wakuwalipa buku saba ili wapige porojo mitandaoni hakuna tena watu wameishi kama mashetani kwa muda sana sio wafanyakazi sio wafanyabiashara aende tu
 
Ndio Udikteta uchwara wenyewe huo
Lala ukitambua kwamba Rais wa jamhuri ya muumgano wa Tanzania ni amiri jeshi mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Utani, mdhaha dhidi yake ni kujitafutia matatizo.
 
Hata na mashangazi pia hakuwa na mzaha nao na naamini mlimpatia baraka zote pia dhidi yao.
JPM hakuwa na mzaha dhidi ya wavuruga amani , majizi, wanaharamu, vibaraka na kwa hilo watanzania tulimpatia baraka zoooote!!!
 
Hakuwa tayari kufanya mzaha katika kuongoza nchi. Na ndio maana hakuona msanii wala mgeni asiekuwa na manufaa akienda ikulu. Ni kazi juu ya kazi.
Mbona Babu Seya na Papii walikwenda Ikulu?

Hebu rekebisha kauli yako.

1616614589386.png
 
Hakuwa tayari kufanya mzaha katika kuongoza nchi. Na ndio maana hakuona msanii wala mgeni asiekuwa na manufaa akienda ikulu. Ni kazi juu ya kazi.
Wajinga wajinga kama wewe na mambumbumbu kama wewe mmekuwa na mpo wengi sana nchi hii na hasa baada ya jamaa yenu kupewa nchi hoja hujibiwa kwa hoja sio mtutu wa bunduki bwashee

ndio maana mwenyezi mungu kaona kabisa hizi hanari za kutekana mara kupigana risasi mara vitisho hazikuwa tabia asili za watanzania akaona isiwe tabu amtwae tuu huyo bwana ili nchi ipone, maana mipango yake ilikuwa sio ya kutoka ikulu kwa hiyari na mikakati ilikiwa inasukwa kwa ustadi mkubwa sana na hesabu kibwa kweli kweli ila mdo hivyo tena bwashee poleni na msiba ni mapenzi ya mola.
 
Je, kiongozi wetu ambae tunaomboleza kifo chake ,kila mtu anajua amefanya makubwa kujenga taifa la Tanzania. Yupo kundi kama la akina hayati Moi?
Magufuli ilikuwa awe ni kiongozi mzuri sana kwa Tanzania, kama angejishusha kidogo tu na kuacha kiburi, kujiona yeye anajua kila kitu.
Kikubwa zaidi kinachomnyima heshima Magufuli ni kutojali HAKI za watu; kujiamlia tu kufanya anavyojisikia yeye nje ya taratibu, sheria na hata Katiba.

Huwezi kamwe kuwa kiongozi mzuri, hata ufanye mazuri kiasi gani unapominya uhuru wa watu; haki za watu kujichagulia viongozi wao wanaowataka wao.

Hakuna mambo ya msingi katika maisha ya binaadam yeyote kama kuwa na HAKI, kuwa huru.

Mbaya zaidi, kiongozi anayetafuta sifa kwa kugawa katika makundi raia anaowaongoza, kamwe hawezi kuwa kiongozi mzuri.

Magufuli alitaka watu wamuelewe kuwa kiongozi anayepigania maslahi ya 'WANYONGE', bila hata ya kuwatambua wanyonge ni akina nani hasa?

Hata hivyo, haizuii kiongozi kupigania maslahi ya nchi, mradi mapambano hayo yanaendeshwa chini ya misingi ya kisheria, bila ya uonevu na kuumiza yeyote, kama kukomoa au kulipa visasi.

Ujenzi wa miradi? SAWA

Upambanaji na ufisadi? SAWA

Nidhamu maofisini? SAWA

Mradi haya yote yanafanyika kwa taratibu zinazoeleweka kisheria

Magufuli hakuwa na subira, ndio maana hakuvumilia mahakama iliyo huru; bunge lililo huru..., badala yake vyote hivi kaviweka chini ya mamlaka yake ili akandamize anavyotaka yeye. Huo sio uongozi bora, hata kama kisingizio cha kufanya hivyo ni kuwanufaisha wanyonge.

Magufuli katawala nchi kwa kutumia mabavu ya polisi, uhamiaji, takukuru na vyombo mbalimbali ambavyo alipaswa kuvitumia ili vifanikishe kazi za serikali kwa wananchi, yeye kavigeuza kuwa vya kukandamiza wasiokubaliana naye na kuwanyamazisha.

Alichoamini Magufuli ni kwamba uongozi wake haukuhitaji "USHAWISHI" katika baadhi ya mambo ili mafanikio yapatikane. Yeye aliamini nguvu zaidi badala ya ushawishi katika baadhi ya mambo.

Kufanya mambo kwa kutegemea maguvu tu mara kwa mara unapokwama unakosa nafasi ya kurudi kwa wale ambao ungekaa nao na kuwashawishi mkafanya jambo kwa maafikiano.

Kutumia maguvu hata katika mambo yasiyohitaji, ni ishara ya udhaifu mkubwa kwa kiongozi.

Nilitamani sana Magufuli afanikiwe, hasa katika kupigania maslahi ya Tanzania kwa faida ya wananchi wake wote.
Huko mwanzo, alipoanza, 2015 na baadhi ya 2016, nilikuwa naye sana, hata kama baadhi ya aliyoyafanya njia zake hazikuvutia.

Mwisho 2021, hakukuwa na jambo lililonitia woga zaidi ya Magufuli kuendelea kuwepo madarakani baada ya 2025! Hili liliniogopesha sana.
 
Back
Top Bottom