Miaka ya tisini nikiwa bado kijana mchakalikaji nilikuwa mtu wa kusafiri sana na katika safari zangu nje ya nchi nilikuwa na kutana na raia wa nchi mbalimbali na mojawapo ni nchi ya Kenya. Siku moja nilikuwa na napiga story na Wakenya juu ya Rais wa Kenya wakati huo Daniel Arap Moi. Na mimi nilimsifia sana Moi hasa juu kuwa kiongozi aliyekuwa anasomesha watoto maskini bure na kugawa maziwa shule za msingi na awali. Na nilimsifia zaidi niliposikia kuwa ana shule inaitwa Kabarak na husomesha watoto maskini.
Lakini kwa mshangao mkubwa baadhi ya Wakenya waliniambia kuwa Moi alikuwa muuaji mkubwa na dikteta na inasadikiwa hata alimuua Robert Ouko. Mimi nilikaa kimya na sikuamini.
Je, kiongozi wetu ambae tunaomboleza kifo chake ,kila mtu anajua amefanya makubwa kujenga taifa la Tanzania. Yupo kundi kama la akina Hayati Moi?