Shujaa wa Taifa au alikuwa Kiongozi wa kiimla?

M
Magufuli ilikuwa awe ni kiongozi mzuri sana kwa Tanzania, kama angejishusha kidogo tu na kuacha kiburi, kujiona yeye anajua kila kitu.
Kikubwa zaidi kinachomnyima heshima Magufuli ni kutojali HAKI za watu; kujiamlia tu kufanya anavyojisikia yeye nje ya taratibu, sheria na hata Katiba.

Huwezi kamwe kuwa kiongozi mzuri, hata ufanye mazuri kiasi gani unapominya uhuru wa watu; haki za watu kujichagulia viongozi wao wanaowataka wao.

Hakuna mambo ya msingi katika maisha ya binaadam yeyote kama kuwa na HAKI, kuwa huru.

Mbaya zaidi, kiongozi anayetafuta sifa kwa kugawa katika makundi raia anaowaongoza, kamwe hawezi kuwa kiongozi mzuri.

Magufuli alitaka watu wamuelewe kuwa kiongozi anayepigania maslahi ya 'WANYONGE', bila hata ya kuwatambua wanyonge ni akina nani hasa?

Hata hivyo, haizuii kiongozi kupigania maslahi ya nchi, mradi mapambano hayo yanaendeshwa chini ya misingi ya kisheria, bila ya uonevu na kuumiza yeyote, kama kukomoa au kulipa visasi.

Ujenzi wa miradi? SAWA

Upambanaji na ufisadi? SAWA

Nidhamu maofisini? SAWA

Mradi haya yote yanafanyika kwa taratibu zinazoeleweka kisheria

Magufuli hakuwa na subira, ndio maana hakuvumilia mahakama iliyo huru; bunge lililo huru..., badala yake vyote hivi kaviweka chini ya mamlaka yake ili akandamize anavyotaka yeye. Huo sio uongozi bora, hata kama kisingizio cha kufanya hivyo ni kuwanufaisha wanyonge.

Magufuli katawala nchi kwa kutumia mabavu ya polisi, uhamiaji, takukuru na vyombo mbalimbali ambavyo alipaswa kuvitumia ili vifanikishe kazi za serikali kwa wananchi, yeye kavigeuza kuwa vya kukandamiza wasiokubaliana naye na kuwanyamazisha.

Alichoamini Magufuli ni kwamba uongozi wake haukuhitaji "USHAWISHI" katika baadhi ya mambo ili mafanikio yapatikane. Yeye aliamini nguvu zaidi badala ya ushawishi katika baadhi ya mambo.

Kufanya mambo kwa kutegemea maguvu tu mara kwa mara unapokwama unakosa nafasi ya kurudi kwa wale ambao ungekaa nao na kuwashawishi mkafanya jambo kwa maafikiano.

Kutumia maguvu hata katika mambo yasiyohitaji, ni ishara ya udhaifu mkubwa kwa kiongozi.

Nilitamani sana Magufuli afanikiwe, hasa katika kupigania maslahi ya Tanzania kwa faida ya wananchi wake wote.
Huko mwanzo, alipoanza, 2015 na baadhi ya 2016, nilikuwa naye sana, hata kama baadhi ya aliyoyafanya njia zake hazikuvutia.

Mwisho 2021, hakukuwa na jambo lililonitia woga zaidi ya Magufuli kuendelea kuwepo madarakani baada ya 2025! Hili liliniogopesha sana.
Mkuu, umemaliza.
Duniani hapa hakuna jema kuliko haki za watu!
 
Alikuwa shujaa wa taifa au dikteta?
 
Ifike muwe na soni, basi kama sio machoni hata mioyoni mwenu. Angalieni huyu mnayemwita muuwaji ni watu wangapi wanahangaika kuuona mwili wake hata kwa mbali tu. Dunia nzima kesho inaomboleza kifo chake. Narudia tena dunia nzima benderaza UN zitapepea nusu mlingoti, hakuna rais alishapewa hii heshima
 
Mkuu hili ni bandiko lenye swali kama hakuwa dikteta tupe maelezo.

Ila kuna watu wanadai kuwa chini ya utawala wake ndugu zao walitekwa, waliuliwa na wengine kupotezwa. Hao waseme nini sasa?
 
Miaka ya tisini nikiwa bado kijana mchakalikaji nilikuwa mtu wa kusafiri sana na katika safari zangu nje ya nchi nilikuwa na kutana na raia wa nchi mbalimbali na mojawapo ni nchi ya Kenya. Siku moja nilikuwa na napiga story na wakenya juu ya raisa wa kenya wakati huo Daniel Arap Moi. Na mimi nilimsifia sana Moi hasa juu kuwa kiongozi aliyekuwa anasomesha watoto maskini bure na kugawa maziwa shule za msingi na awali. Na nilimsifia zaidi niliposikia kuwa ana shule inaitwa Kabarak na husomesha watoto maskini.

Lakini kwa mshangao mkubwa baadhi ya wakenya waliniambia kuwa Moi alikuwa muuaji mkubwa na dikteta na inasadikiwa hata alimuua Robert Ouko. Mimi nilikaa kimya na sikuamini.

Je, kiongozi wetu ambae tunaomboleza kifo chake ,kila mtu anajua amefanya makubwa kujenga taifa la Tanzania. Yupo kundi kama la akina hayati Moi?
Jibu la swali lako la kipuuzi lipo hapa: Magufuli alikuwa dikteta wa Mabepari, wala rushwa, na maharamia ya rasilimali zetu ameyakomesha kwa kuwekeza fikra zake kwa Dunia ya Wanaoonewa
 
Mkuu hili ni bandiko lenye swali kama hakuwa dikteta tupe maelezo.

Ila kuna watu wanadai kuwa chini ya utawala wake ndugu zao walitekwa, waliuliwa na wengine kupotezwa. Hao waseme nini sasa?
Chuki zako zinaweza kuwa za kweli kama wewe ulikuwa fisadi wakati wa JK na familia yake. Ulikuwa huna sifa za kufanya kazi serikalini au mzazi wako alitumbuliwa. Juzi nilikueleza kuwa maendeleo huwa yana athari zake, na hii inakubalika katika utawala. Pole sana jaribu tena unaweza kufanikiwa
 
Miaka ya tisini nikiwa bado kijana mchakalikaji nilikuwa mtu wa kusafiri sana na katika safari zangu nje ya nchi nilikuwa na kutana na raia wa nchi mbalimbali na mojawapo ni nchi ya Kenya. Siku moja nilikuwa na napiga story na wakenya juu ya raisa wa kenya wakati huo Daniel Arap Moi. Na mimi nilimsifia sana Moi hasa juu kuwa kiongozi aliyekuwa anasomesha watoto maskini bure na kugawa maziwa shule za msingi na awali. Na nilimsifia zaidi niliposikia kuwa ana shule inaitwa Kabarak na husomesha watoto maskini.

Lakini kwa mshangao mkubwa baadhi ya wakenya waliniambia kuwa Moi alikuwa muuaji mkubwa na dikteta na inasadikiwa hata alimuua Robert Ouko. Mimi nilikaa kimya na sikuamini.

Je, kiongozi wetu ambae tunaomboleza kifo chake ,kila mtu anajua amefanya makubwa kujenga taifa la Tanzania. Yupo kundi kama la akina hayati Moi?
Comments reserved
 
Jiongelee wewe mbwaku mkubwa, lini umekuwa msemaji wa watanzania?? na hili ndilo tatizo la binadamu kutumia akili ya ngedere
JPM hakuwa na mzaha dhidi ya wavuruga amani , majizi, wanaharamu, vibaraka na kwa hilo watanzania tulimpatia baraka zoooote!!!
 
Kila kitabu na zama zake.
July.17.20.Magufuli.and_.his_.Advisers-595x450.jpg
 
Ifike muwe na soni, basi kama sio machoni hata mioyoni mwenu. Angalieni huyu mnayemwita muuwaji ni watu wangapi wanahangaika kuuona mwili wake hata kwa mbali tu. Dunia nzima kesho inaomboleza kifo chake. Narudia tena dunia nzima benderaza UN zitapepea nusu mlingoti, hakuna rais alishapewa hii heshima
Hivi kuna dikteta ambaye watu wengi walienda kwenye Msiba wake kama Stallin wa Urusi?

Unadhani ni kwa sababu alikuwa anapendwa?

Hell no.

Hiyo sababu yenu ya kwamba watu wakijaa msibani ndio wanakupenda ni ya kipumbavu.
images (24).jpg
 
Back
Top Bottom