Shujaa wa Taifa au alikuwa Kiongozi wa kiimla?

JPM hakuwa na mzaha dhidi ya wavuruga amani , majizi, wanaharamu, vibaraka na kwa hilo watanzania tulimpatia baraka zoooote!!!
Unazungumza KWA NIABA ya watz wote, nani kakupa idhini hiyo?!
au ni kimbele mbele chako tu kimekutuma.
 
Wale waliobomolewa nyumba kimara walikuwa mafisadi. Right?

Halafu Mwanza akasema. Msiwabomolee nyumba sababu walinipa kura.

Double standards.
 
Hahahahahaa. Kulia na kucheka yote ni makelele tu.
 
Wale waliobomolewa nyumba kimara walikuwa mafisadi. Right?

Halafu Mwanza akasema. Msiwabomolee nyumba sababu walinipa kura.

Double standards.
Faida ya kubomoa nyumba za kimara huioni mpaka leo. Ni kile nilichokisema kuwa ili maendeleo yapatikane lazima wengine waumie, wavunjiwe nyumba zao, watandikwe risasi 16, na wengine wawe silenced ili maendeleo yapatikane, hiyo ndiyo gharama ya maendeleo.
 
Magufuli alikuwa ni dikteta, muuaji katili, nwizi, mbaguzi wa kikabila na kikanda na muumini wa Shetani.
 

Umesahau kusema pia na yeye ilibidi afe ili maendeleo yapatikane vizuri, what goes around, always comes around!
 
Alimpoteza hata yule aliyejaribu kuhoji uhalali wa PhD yake.
Kafaya hakua na kifua kabisa cha kuvumilia maswali magumu dhidi yake! Nimemkumbuka Pascal mayala wetu!
 
Umesahau kusema pia na yeye ilibidi afe ili maendeleo yapatikane vizuri, what goes around, always comes around!
Inategemea unaongea kwa angle ipi, kama alikuzibia riziki lazima afe ili riziki zako uzifaidi, inakwenda both side. Hata kwa taifa si ajabu kuna vitu alikuwa anavikataa kuvipitisha vyenye manufaa kwa Taifa, hivyo kifo chake kinaweza kuwa nacho kichocheo cha maendele.
 
Haki za binadamu ambazo hakuzijali ni zipi? Au za makundi gani? Maana haki za binadamu ni pana mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina sikitisha sana kwamba mh. Magufuli akiwa rais yalitokea mambo ya ajabu ambayo hayakuwahi kutokea kabla ya uongozi wake. Jaribio la kumuuwa Lissu, kupotea Azori, Ben Saa8, etc, kuuwawa Mawazo, Mwangosi, Akwilina etc.

Pia maiti zilizookotwa, watu kutekwa eg Mohammed Dewji etc. Matukio haya na mengine hayakuchunguzwa na kutolewa majibu. Akiwa kiongozi mkuu alipaswa kusimamia haki uchunguzi wa maovu haya ufanywe na kila mhusika apate haki yake, na waovu waadhibiwe kisheria.

Tulishuhudia pia manyanyaso dhidi ya vyama vya upinzani, kuzuiwa shughuli halali za siasa, biashara haramu ya kununua wabunge na madiwani. pia uvurugwaji uchaguzi s/mitaa, chaguzi za marudio na uchaguzi mkuu.

Ubaguzi mkubwa wa kikanda. Mfano miradi mingi kutekelezwa kanda anayotoka rais hasa Chato, na maeneo mengine kusahauliwa. Pia teuzi kuegemea ukanda mmoja.

Mh. Magufuli hakuwa mnyenyekevu. Kauli zake zilijaa kiburi, eg ' mimi ni jiwe' 'mtalimia meno' 'mkae na mavi yenu' ' ninge wachapa shangazi zako' nk. Alikua mnafiki/mtu wa ndimi mbili: 'maendeleo hayana vyama' kisha 'mlifanya makosa kuchagua mpinzani' 'mimi ni rais wa watu wote' kisha 'msichanganye betri na gunzi tochi haitawaka'

Mungu ni mwaminifu. Ni mwenye huruma. Ndiye hakimu wa mwisho mwenye haki. Atatulipa sote kadiri ya matendo yetu tulipokuwa hapa duniani, ambapo tuko safarini na hatujui tutakufa lini/ktk mazingira gani. Tumuombe roho wake mtakatifu atuongoze ktk haki na utakatifu ili hatimaye tufike kwenye ufalme wake mbinguni.
 
JPM hakuwa na mzaha dhidi ya wavuruga amani , majizi, wanaharamu, vibaraka na kwa hilo watanzania tulimpatia baraka zoooote!!!
Semea nafsi yako ndugu. Kikao cha waTz wote kilfanyika lini/wapi?
 
Na Mungu amemtandika Fimbo Kama aliyopigwa Farao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…