Shujaa wa Taifa au alikuwa Kiongozi wa kiimla?

Magufuli alishindwa kula na Kipofu. Watanzania ni watu waelewa na wepesi sana kuwaongoza. Wewe fanya ufanyalo kama ni miradi sawa ila wape nafasi ya kuonyesha hisia zao. Kinachofanya Haji Manara apendwe Simba ni kucheza na hisia za Mashabiki wa Simba. Kuwapa nafasi ya kufurahi, kucheka na kuwadhihaki Yanga bila kupigana. Vivyo hivyo kwa mashabiki wa Yanga. Ndiyo maana wala mashabiki wa Yanga walioanza kuona mashabiki wa Simba ni maadui kiasi cha kuwadhuru walikemewa na viongozi wa Yanga na mashabiki wenzao wa Yanga. Mambo yakarudi kwenye mstari. Hata Kikwete aliwaambia Yanga waachane na chuki dhidi ya Morrison na Simba badala yake na wao wakamnyakue mchezaji bora wa Simba na siyo makelele tu kila kukicha. Sasa Huyu jamaa aliyetutoka alijenga dhana kwamba Chadema na upinzani ni maadui na akawaambukiza hata wafuasi wa CCM kuwashambulia wapinzani kwa mishale, shoka na mapanga huku yeye akifurahia maumivu ya wapinzani. Kumbe yeye angeacha watu wawe huru Kidemokrasia na kuacha siasa za ushindani ziendelee huku yeye akichapa kazi. Angejipatia sifa njema kila kona na kwa makundi yote. Sasa ona anatandikiwa kanga barabarani na wafuasi wa CCM tu.
 
JPM hakuwa na mzaha dhidi ya wavuruga amani , majizi, wanaharamu, vibaraka na kwa hilo watanzania tulimpatia baraka zoooote!!!
Mkuu lini utaacha uhongo, Kama binadam huwezi kosa mazuri, na huwezi kosa mabaya,so mazuri ya jpm yasemwe,na mabaya pia yasemwe
 
Haki za binadamu ambazo hakuzijali ni zipi? Au za makundi gani? Maana haki za binadamu ni pana mno

Sent using Jamii Forums mobile app
Huzijui?

Unataka niziorodheshe zote hapa?

Acha nikupe mfano mmoja mzito zaidi kati ya haki hizo:

Haki ya kuchagua viongozi wanaowataka wananchi bila ya kuingiliwa na yeyote ni haki ya msingi muhimu kwa binaadam yeyote. Unapomnyima haki hiyo mtu kwa njia mbali mbali, kama kuiba kura, au kuchafua uchaguzi kwa njia yoyote usiwe huru na wa haki, moja kwa moja umemnyima mwananchi huyo haki yake. Viongozi watakaowekwa madarakani watakuwa sio aliowataka wamuongoze.

Wewe hapo ninakujua vyema kutokana na michango yako humu.
Hilo swali uliloweka hapo sio kwamba hujui majibu yake. Kwa maksudi mazima nimekupa mfano huo, kama sehemu ya jibu kwa swali lako, hata kama najua nampigia mbuzi gitaa.
Kuna watakaosoma hapa na kuelewa.
 
 
Kilichobakia sasa ni kuvishughulikia vimalaika vyake viasi.
Wasiojulikana wote ni lzm wakavune maharage yao
 
Tutashitakiwa MIGAView attachment 1734175
 
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]pamoja na mapungufu yake yote usiseme hivyo,hajaenda likizo ujue
 
Dikteta Magufuli alikuwa mtu mkatili, muonevu na muongomuongo, asiyeheshimu haki za watu wala katiba ya nchi.
Pia alikuwa mpenda misifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…