SHUKRANI!.....thank you JAMIIFORUMS

Hehehe jana nilipiga valeur mchana alafu ikayeyuka mpwa zipo feki siku hizi.
Unajua kuna watu hawapendi kuzaa mapema wanapenda wazae baada ya malengo flani kutimia.

dah mpwa itabidi turudi kwenye gongo ama inakuwaje sasa?

exactly mpwa hapo sawa, ndo tutauliza kama malengo yametimia au tuwape mwaka mmoja zaidiπŸ˜€

wapi baba Askofu!?
 
X-pin, tuweke uzungu na unafiki kando halafu tuseme ukweli wa Kiafrika... Umeoa Mke, amekaa mwaka mmoja hajapata mtoto, utaona eyebrows zinaanza kuinuliwa... na maswali kibao... mwaka wa pili ukipita inakuwa balaa... tusidanganyane...
Jamani ingawa hii ni kweli lakini tusisahau na kuanza kujivika joho la MUNGU. Watoto ni majaaliwa ya MUNGU.

Nina rafiki yangu aliyeolewa mwaka jana, after one month baada ya arusi akapata matatizo ya tumbo fibroid akaendapasuliwa itolewe madr si wakakosea wakakata vya kukata na kumsababishia kizazi kuharibika! Ndo hawezipata mtoto kabisa maana kilitolewa na ndio kwanza anatimiza 28 this december!

Haya kwa kibantu bado tutang'ang'ania ndoa ni lazima tupate watoto?! Au ndo mtasema itabidi mumewe atafute mke mwingine??
 
Haya kwa kibantu bado tutang'ang'ania ndoa ni lazima tupate watoto?! Au ndo mtasema itabidi mumewe atafute mke mwingine??

Ndoa sio lazima upate watoto.
Ndoa ni mwanamke na mwanaume kupata mtoto/watoto ni majaaliwa.
Kikuwa zaidi katika ndoa ni upendo, shibishaneni upendo ndani ya nyumba ndo raha ya ndoa na si watoto ambao kuwapata ni maajaliwa ya mwenyezi Mungu. Mkisha kuwa kitu kimoja kama mwili mmoja ni faraja kwenu wawili.
 
Sikatai. Nashtushwa kidogo kuwa je inapotokea hivyo kwa kuwa ni Mpango wa Mungu. Hiyo ndoa tuisarambatishe kijana akatesti zari kwingine?

Sasa hapa ndo tunarudi kwenye ile sredi nyingine ya Geoff... Arranged V/s Love Marriages... Kama ni arranged Marriage kule kwetu, Geoff angepewa mdogo wake Mshiki aendeleze familia...πŸ˜€
 
Mjukuu leo maona tutaimba wimbo mmoja.
Yeeeeesu kwetu ni Rafiiiiikiiiii
Akaaaye Mbinguniiiiii
Hutuombea kwa baaaaabaaaa............
 
Mpwa leo tukutane kwa ankal. Unanidai miksa ya valuu na safari!
 
Baba, Mama na Watoto

Watoto wanapokosekana si familia tena? Lets say Familia ya Askofu mlikuwa mume mke na watoto wawili. Bahati mbaya watoto wakatangulia mbele ya haki. Inakuwa tena si familia ya Askofu?
 
Sasa hapa ndo tunarudi kwenye ile sredi nyingine ya Geoff... Arranged V/s Love Marriages... Kama ni arranged Marriage kule kwetu, Geoff angepewa mdogo wake Mshiki aendeleze familia...πŸ˜€

Watu mnapotosha nyie.
Ndoa bana sio lazima mzae watoto mm hili nalikataa nina babu yangu kaishi na mke wake miaka yote na hawana mtoto hata mmoja na wanaenjoy life. Upendo wenu ndani ya nyumba ni zaidi ya kuwa na mtoto wengine wanafikiri kuzaa ndo kunaongeza upendo ndani ya nyumba sio kweli.
 
Sasa hapa ndo tunarudi kwenye ile sredi nyingine ya Geoff... Arranged V/s Love Marriages... Kama ni arranged Marriage kule kwetu, Geoff angepewa mdogo wake Mshiki aendeleze familia...πŸ˜€

Mi nikiwaambia huyu askofu feki watu wananibishia. Huyu ni askofu Mdumisha Mila mwenzetu! Senksi Askofu, unatumia bia gani vile?
 
Mpwa leo tukutane kwa ankal. Unanidai miksa ya valuu na safari!

Unajua leo namwaga point tupu mchumba yupo kama guest ananifanyia tathimini nisije nikapoteza si unajua ni mlokole.
 
MJ1, hatukatai kwamba haya yote yapo, either ni mapenzi ya Mungu au mapenzi ya shetani... lakini je? twende kwenye ukweli wenyewe... deep down kwa huyo mwanaume, unafikiri atajiona amekamilika bila kuwa na mtoto? tuache utani jamani... mtoto katika ndoa ni issue kubwa sana.
 
Mi bwana mpwa wewe leo bana lazima tukutane nikuongezee kanywaji. Hicho kichwa jana inaelekea kilipata safari za kutosha baada ya kusokomeza kongoro bomba kwa tumbo!
 
Hebu turudi kwenye katiba yaani BIBLIA. Kuna Sehemu yoyote kwenye biblia inayosisitiza hilo? Sakramenti bana ni mambo ya kimapokeo tu, mi nafuatilia BIBLIA zaidi!

Soma Mwa 1: 26-28, 2: 21-24. (agano la kale)

soma Math 19: 1-10, Mk 10:1-10, Lk:16:18 (agano jipya-injili)

hapo hatujagusa nyaraka.....inherent kwenye hilo ni msisitizo wa ndoa kama ilivyokuwa imeumbwa tangu mwanzo...manake mfano mafarisayo walitaka kumtega Yesu juu ya uhalali wa talaka...akaawaambia 'maandiko yanasemaje? wakasema kuwa Musa aliwapa ruhusa ya talaka.....akawaambia ilikuwa hivyo kwa sababu ya UGUMU wa mioyo yenu...ila tangu mwanzo ilikuwa mtu atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja...sasa ukisoma Mwanzo 1:26-28, Mungu aliwaagiza mwanamke na mwanaume kuwa "zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi".!

haya tuendelee jamani samahanini kwa maandiko yaliyo biased sina uzoefu wa quran tukufu!
 
Watoto wanapokosekana si familia tena? Lets say Familia ya Askofu mlikuwa mume mke na watoto wawili. Bahati mbaya watoto wakatangulia mbele ya haki. Inakuwa tena si familia ya Askofu?

Unapojitambulisha ugenini sehemu unasema "nimekuja na mke wangu" sio "nimekuja na familia yangu"
 
This is completely understandable MJ1,,,, hayo yapo mengi na huwa yanatokea,, na hata Mungu anaweza kuamua tu kwa jinsi anavopenda yeye.

Normatively, we expect them to have babies! hilo tusikatae..hatulazimishi, lakini hilo linategemewa ..kijamii. Sasando tunasema tutafanya audit mwaka mmoja baadaye, vipi kuna 'majibu' au la?πŸ˜€
 
Mi nikiwaambia huyu askofu feki watu wananibishia. Huyu ni askofu Mdumisha Mila mwenzetu! Senksi Askofu, unatumia bia gani vile?

Attitude uh!! Ni maoni yako... Lete Divai ya motoooooooπŸ™‚
 
Nasikitika nimesahau kale kabiblia kangu. Ntaipitia baadaye. Lakini ukweli ni huu: NCHI NA VYOTE VIIJAZAVYO NI MPANGO WA MUNGU NA NI MALI YAKE PIA.

Sasa wanandoa wanapokosa mtoto na talaka ndo imepigwa ban bado still tuna courage ya kumuuliza mtu MBONA HUJAPATA MTOTO na ndoa yako ina miaka miwili sasa?
 
Sasa hapa ndo tunarudi kwenye ile sredi nyingine ya Geoff... Arranged V/s Love Marriages... Kama ni arranged Marriage kule kwetu, Geoff angepewa mdogo wake Mshiki aendeleze familia...πŸ˜€

Baba Askofu, unajua mdumisha mila hawezi kusahau, hapo ndo maana amejisahau akatoa huo mstari na siye tumeuona, kumbe anaweza kumpeleka kitonga bondeni kabisa! Stuka!πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…