Shukrani za Jamal Emil Malinzi kwa wana JF

Shukrani za Jamal Emil Malinzi kwa wana JF

Huyu Malinzi ndo boya namba moja,huyu ndo kaja kuua mpira wetu,kila ukienda uwanjani mtu unajiandaa kisaikolojia kufungwa tu,tunafungwa na kila timu,poor Malinzi Jamal
Hivi kwa sura, tabia na historia unaweza kumfikiria Leodgar Tenga kuwa ni mtu wa chuki na visasi? Mimi simuoni hivyo. Jitihada za TFF yake kuainisha udhaifu wa Jamal Malinzi zililenga kweli kwenye kuliokoa soka letu. Bahati mbaya wanahabari uchwara kama kawaida yao wakakejeli jitihada hizo na kumtetea Malinzi mpaka akaukwaa Urais. Haya ndiyo matokeo yake sasa.
 
Ndugu zangu nashukuru uchaguzi tumemaliza salama na mimi nimeshinda. Nichukue fursa hii kuwashukuru wapenzi na wadau wote wa mpira miguu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kwenye mchakato.

Siku chache zijazo nitafungua thread hapa nikiomba maoni na mapendekezo yenu kuhusu ni jinsi gani tutaimarisha timu yetu ya Taifa kwa ajili ya AFCON qualifiers Novemba mwaka ujao.

Tafadhali jiandae kuchangia.

Malinzi

Tapeur
 
Ni aibu na fedheha kubwa sana unapoutaka uongozi kwa gharama zote huku ukijua kabisa huna uwezo huo! Tunaopenda soka la nyumbani Tz umetunyonga na kamba ya plastic na kututupa kisimani!

Soka la Tz kwa miaka sasa linachezwa zaidi kwenye magazeti, vipindi vya sports kwa radio na tv only, wachezaji ambao kwa kiasi kikubwa mzee Tenga alisaidia kuwapa status ya heshima sasa wengi wao wamefulia, uongozi wa TFF na Clubs za soka almost zote hazina Vision wala Mission, timu zinachezea majina tu sasa na sio ubora wa soka! Vijana mamia kwa maelfu wanakosa ramani kwa soka la ndondo mchangani, hawana thamani wamebaki kutumika na wajanja wachache wanaoanzisha vi league mshenzi ili kukusanya mapato!!

It is a disgrace sekta ya michezo Tz, ipo kama Mgonjwa aliyesuswa na Ndugu!
**Wahaya kuandamana muhimu mno, kuna mtu kawachafulia CV ya uchapa kazi!
 
We Jamal vipi mbona unafanya hivi,unazungukazunguka nini?!,ok.tunashukuru pia kwa shukrani zako lakini unapaswa kwenda mbaali zaidi ya hapa ikibidi tuandalie hata LUNCH kwa sababu kazi tuliyofanya ni kubwa Mno!!
Nyie ndiyo mnaomtukana baada ya kuwanyima lunch...
 
mkuu Crashwise, kama ulivosema kwenye ule uzi mwingine, jf sasa inajivunia kuwa na member aliyechaguliwa moja kwa moja kushika nafasi ya juu na kampeini zake kwa kiasi fulani zikiwa zimepitia hapa hapa jamvini.
omujubi jamaa katugeuka analalamika kuwa tunamtukana...
 
Da jamali malinzi bana
inasemekana umetujaza sisi wahaya TFF sasa nakuomba utuondoe haraka maana ni aibu kwa sisi wahaya..kisha na wewe utoke
Amejaza wahaya wenye upeo na weredi wa SOKA, Jamal Malinzj bhana,sasa ndo namkumbuka Mtinginjore na kamat yake walimchinja huyu jamaa
 
Jamal Malinzi ni moja ya majanga makubwa kabisa kupata kutokea katika mchezo wa mpira wa miguu. Na hili nliwah kulisema hapo mwanzo nikatoa na maelekezo mengi sana nikafungiwa maisha humu JamiiForums na thread yangu kunyofolewa kwa hasira ikiwa imeonwa na wachangiaji wa3.

Nilisikitika sana na sikujua ni nani na kwa maslah ya nani aliinyofoa na kuichana chana thread ile kisha kuichoma moto na kusaga saga majivu kwa hasira, huku naye akisaga meno na kutoa maneno ya maapizi kwa lugha zote alizowahi jifunza toka utoto. Leo hii maneno yale nliyokuwa nikisema yametimia.

Malinzi hakuwahi kuwa na nia thabiti kwenye kuendeleza michezo. Hiki ni kipindi ambacho soka letu linazidi kudidimia ndani na nje ya nchi. Upangaji matokeo limekuwa ni jambo la kawaida kuanzia ligi kuu mpaka huko mchangani.

Maamuzi ya kipumbavu kwa baadhi ya team. Nasema ya kipumbavu si ya kijinga. Na ashakum si matusi upumbavu ni sifa. Asije akasema mtu ametukanwa mimi ni msomi wa lugha.

Tumeona madudu yanayofanyika kwenye uongozi huu na sasa amebakiza muda wa kupiga pesa za kujiandaa na uchaguzi ujao. Nalisikitikia sana soka la nchi hii.
 
Back
Top Bottom