Shukrani za Jamal Emil Malinzi kwa wana JF

Shukrani za Jamal Emil Malinzi kwa wana JF

Hongera sana japo sikuwa nakuunga mkono, lakini sasa wewe ndio rais wetu tuko pamoja.
 
Hongera sana, tuna matarajio ya mabadiliko. Lakini, pamoja na kuwa utaweka sredi ya kuomba maoni ya wadau, lakini na wewe lazima ulikuwa na vipaumbele vyako ulivyokuwa umeshajiwekea na unavyojua unataka kuvisimamia, ili hata siku muda wako ukitoka tukukumbuke kwa hayo.

Kwa mtizamo wangu, ukiainisha vipaumbele vyako kwenye uzi huo, nasi wadau tukaweka maoni yetu jinsi ya kufikia vipaumbele hivyo inakuwa rahisi zaidi. Unaweza kuwa na kipaumbele A, wadau tukatoa maombi ya kipaumbele D. Kuvichanganya inaweza kufanya u-divert energy yako afu matokeo yawe hafifu.
 
Ndugu zangu nashukuru uchaguzi tumemaliza salama na mimi nimeshinda. Nichukue fursa hii kuwashukuru wapenzi na wadau wote wa mpira miguu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kwenye mchakato.
hongera sana tunategemea mengi mazuri kutoka kwako ili soka letu lisonge mbele
 
hongera sana sana Jamal Malinzi, kwa nafasi uliyoipata. Mimi kuna uzi nimeweka ninachokiona kinahitaj kuboreshwa lkn pia sitak kusema kabla ya muda kufika hivyo naomba ni reserve hizo comments hadi utakapoweka uzi wako.

istoshe kaa Kongosho alivyoshauri ni vyema ukatuwekea vipaumbele vyako ili isije ikawa tunarudia yale ambayo tayari wewe ulishayapanga.

Otherwise Malinzi tunahitaj kupiga hatua kisoka tumechoka kila siku kuwa vibonde tumechoka kubebeshwa makapu ya kushindwa, tumechoka tumechoka tumechoka, tumekupa uongozi kwakua tunaimani na wewe. usituangushe tafadhali.

pia ukae ukijua kwamba siku ukiboronga tutakuja kukuchana live hapa hapa jamvini...............
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana maana umeanza kwa uwazi na umemaliza kwa uwazi.
Kilichonifurahisha na hasa kutoka kwenye uzi uliouweka hapa (dakika 90 za kujibu maswali), mizengwe yote wadau waliyotarajia imeonekana na umeivuka.
Umeiheshimu jf na yenyewe imekuheshimu na nina imani itakupa ushirikiano nawe kama gt. Asante sana kwa hili na tunakuombea Mungu vile vikwazo vyote vitakavyokutokea katika kutimiza vision yako viyeyuke kama mizengwe ya kwenye uchaguzi ilivyoyeyuka.
Mwenyewe unajua kuwa Tanzania karibia kila sehemu ni fitina na usaliti, ukivikalia vizuri hivyo vitu viwili kwa hakika utatusogeza kwenye ngazi nyingine kimpira.
 
Hongera Jamal Malinzi na tunasubiri kwanza huo uzi wako tujue tunajipangaje na tunaomba vile vile uwe unatembelea humu mara kwa mara kutupa mrejesho wa yale utakayoulizwa
naunganga na gfsonwin katika kusubiri utupe mikakati uliyo nayo haswa kwa vilabu vyetu na timu ya taifa tuache kuwa wasindikizaji kila mashindano na tuone tunavuka kwenda hatua za fainali tuache kuishia huku chini kila mashindano
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nategemea kiwango bora kabisa toka timu zetu hasa ya Taifa...ipandishe bhana kwenye viwango vya FIFA...Once again hongera sana!! Jaribu kubalance sheria, manake nyingi zina mkanganiko sana hasa kipindi cha uchaguzi!! Hata Wambura analijua hili!!
 
Hivi federation mpaka inaanzishwa kazi zake ni zipi????!!!!!!

Why vipaumbele tuweke sisi na Rais??!!!!!!

Ufafanuzi please
 
Hongera Jamal Malinzi na tunasubiri kwanza huo uzi wako tujue tunajipangaje na tunaomba vile vile uwe unatembelea humu mara kwa mara kutupa mrejesho wa yale utakayoulizwa
naunganga na gfsonwin katika kusubiri utupe mikakati uliyo nayo haswa kwa vilabu vyetu na timu ya taifa tuache kuwa wasindikizaji kila mashindano na tuone tunavuka kwenda hatua za fainali tuache kuishia huku chini kila mashindano
ni kweli kabisa ndugu yangu tumechoka sana kuwa wasindikizaji tuuuuuuu miaka nenda miaka rudi sasa hebu huyu memba mwenzetu alifanyie kazi swala hili
 
Ndugu zangu nashukuru uchaguzi tumemaliza salama na mimi nimeshinda. Nichukue fursa hii kuwashukuru wapenzi na wadau wote wa mpira miguu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kwenye mchakato.
Siku chache zijazo nitafungua thread hapa nikiomba maoni na mapendekezo yenu kuhusu ni jinsi gani tutaimarisha timu yeTu ya Taifa kwa ajili ya AFCON qualifiers Novemba mwaka ujao.Tafadhali jiandae kuchangia.
Malinzi

Napenda kukupongeza kwa kuwa Rais wa TFF.
Kubwa kabisa la kwanza ambalo linaangusha mpira nch hii ni kitu kinaitwa Simba na Yanga?Je utakua tayari kuweka unazi wako wa yanga pembeni na kufanya maamuzi bila upendeleo wa timu hizi.Hakikisha pia unasimamia suala la Rushwa kwa waamuzi ili tupate maamuzi ya haki.Sitaki kuongea mengi ila pale utakapo hitaji ushauri na mapendekezo JF kuna kila kitu.

Mwisho kabisa hilo la timu ya Taifa ,tuliishafundishwa kwamba timu yetu inashindwa kwa sababu ya maandalizi mabovu na yasiyo ya kutosha.Tuna mwaka mzima sasa,ni wakati wa kuaandaa timu ,ianze maandalizi mapema.Ijapokua wachezaji wetu ni wagumu kama miti,kwa maandalizi ya muda mrefu wanaweza kufanya kitu.

Nikutakie kila la kheri katika majukumu yako mapya.Hopefully utatusaidia tupunguze kuangalia mpira kwenye Luninga.
 
Hongera sana Jamal Malinzi tumekupigania mwanzo mwisho kwa kumtanguliza Mungu mbele na Mungu amesikia kilio chetu wana Football Family kazi iliyopo mbele yako ni kubwa mtangulize Mungu ili uweze kuyashinda majaribu yote yatakayo kupitia. Kwa sasa ukisha kabidhiwa ofisi tunaomba uombe msaada kwa CAG aje akague hesabu zote ili tuweze kujua kilichopo na kilicho tumika na wewe unaanza kazi kukiwa na kiasi gani ofisini.
 
Last edited by a moderator:
Hongera Sana Jamal Malinzi.Mungu azidi kukupigania ufanye kazi kwa bidii.
 
Hebu tuondolee huyo Sunday Kayuni hapo TFF kwanza ndio tuongee mengine.

Jitu limekaa linadumaza mpira eti ndio mkurugenzi wa ufundi! Ufundi upi!

Fagia uchafu wote TFF na tunataka auditing report kwanza. Halafu lile zee Ashlod Mamelodi kutoka Botswana ni sehemu ya mtandao wa kifisadi wa kina Tenga kutafuna pesa za FIFA hatumtaki.
 
Back
Top Bottom