Shule 24 zafungiwa kuwa vituo vya Mitihani kwa udanganyifu

Shule 24 zafungiwa kuwa vituo vya Mitihani kwa udanganyifu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limezifungia shule 24 kuwa vituo vya mitihani ya Taifa baada ya kuthibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

Shule hizo ambazo ni sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote vya mitihani nchini, ndani yake zipo shule maarufu ikiwemo ya Musabe ya jijini Mwanza na St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam na shule ya Rweikiza ya mkoani Kagera.

Hayo yameleezwa leo Desemba Mosi na Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2022.

Akizitaja shule hizo ni Kadama shule ya msingi iliyopo Chato- Geita, Rweikiza (Bukoba), Kilimanjaro shule ya msingi (Arusha) Sahare (Tanga), Ukerewe (Mwanza), Peaceland (Mwanza), Karume (Kagera), Al-hikma (Dar es Salaam)

Nyingine ni Kazoba (Kagera), Mugini (Mwanza), Busara (Mwanza), Jamia (kagera), Winners (Mwanza), Musabe (Mwanza), Elisabene (Songwe), High Challenge (Arusha), Tumaini (Mwanza), Olele (Mwanza), Mustlead (Pwani).

Pia zipo shule za Moregas (Mara), Leaders (Mara), Kivulini (Mwanza) na St Severine (Kagera).

“Vituo hivi vimefungiwa kwa mujibu wa kifungu 4(8) cha kanuni za mitihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya kitaifa,” amesema.

Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulihusisha watahiniwa zaidi ya 1.38 milioni nchi nzima.
 
Ni kufutiwa uchunguzi wa kitaalamu na kitaaluma ambao vyombo vya uchunguzi na na NECTA umebaini watoto hao walishiriki katika udanganyifu wa mitihahani mwaka huu.

Aidha shule kadhaa pia zimekumbwa na pamba hilo huku kesi za wizi wa mitihahani zikiwa mahakamani.

Awali shule hiyo inayomilikiwa na mbunge wa bukoba vijini ilikuwa ikiongoza matokeo kwa miaka mingi na kuwa kinara kwa mkoa wa Dar es salaam na taifa kwa ujumla

USSR
 
Walioshiriki ni walimu na wazazi, tusiwaonee watoto.
 
St.Anne Marie au St.Marie ?
Mbona hueleweki mzee
#Johnson Rweikiza hapa
Shule zenu zote kaka ile ya bukoba na hii ya hapa ubungu st Anne Marie na lweikiza zote zimefutiwa

USSR
 
Huwa nawaambia waislaam... Hakunaga shule ya kiislaam... Ni shule za wajanja wajanja tu ambao wanaotaka kuteka hisia za waislaam wajinga wakidhani wanaenda kujifunza uislaam... Wanawadanganya kwa mavazi ya kiislaam majalbiib... Wakati mavazi kama hayo yapo hata shule za serikali... Huo uislaam wenyewe unafundishwa kwa kuonja na wala haupewi kipaumbele.

Sasa ona hiyo AL HIKMA ya SHEIKH NURDEEN KISHKI... imefungiwa kwa udangangifu... (they always try to do so kunyanyua ufaulu waweze kujitangaza na kupandisha ada) alafu baadae wanageuka ETI WAISLAAM TUNAONEWA KWENYE MATOKEO... WAPUMBAVU WAKUBWA.

Nyingine ni hiyo JAMIA...

NINGEKUWA RAIS NINGEKATAZA KUITA SHULE KUINASIBISHA NA DINI... ETI ISLAMIC... NI UHUNI NA UTAPELI TU...
 
Ila hili swala ni kweli ni biashara sana Kuna mwaka fulani shule kibao zilifungiwa nyingi zilikuwa ni private.
 
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limezifungia shule 24 kuwa vituo vya mitihani ya Taifa baada ya kuthibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.
Musabe kwisha habari😂😂
 
Too bad waathirika wakuu ni watoto wadogo wasio na hatia.
NYIE SI MWAFUATA UFAULU SIJUI MNAITA UBORA WA ELIMU...

TELL ME SASA ALIYEPATA A NA ALIYEPATA C.... WANATOFAUTIANA NINI?
 
Nimesoma pale najua Kila kitu kuhusu pale Kuanzia primary up to Advance ..... Acha nicheke TU[emoji23] ...Mzee Kanasa
Kumbe nawe umepita Anne Marie, hivi yale Mabweni wamejenga mapya?
 
Back
Top Bottom